Pamoja na kumtumia Mengi mikakati 14 ya Wapiganaji CCM itawaangusha

Mbona nimesoma gazeti leo inaelezwa kuwa tiyari WAPIGANAJI wameshinda vita yao!! Lakini siyo gazeti la Mengi! na ukiongalia ni kweli fatilia Makamba huko Tabora ...............sijui Mwakipesile........ Guninita....
 
Vyote hawa vita vyao ni Madaraka, narejea makala ya ndugu yangu Kishoka, Wote kama kweli wana nia ya dhati basi wahamie vyama vya Upinzani, Ndugu yangu utaona kuwa mwakani hawa jamaa hawatapewa tena kugombea ubunge na ndio utakuwa mwisho wao
Hawa jamaa wanatapatapa ili CCM isiwaengue kutoka kwenye kugombea ili hata ikifanya hivyo wakihamia upinzania wapiga kura wawaonee huruma na kuwapigia kura. Tunahitaji whistle blowers and wabunge wenye upinzani wa tija kwenye bunge letu. Tunahitaji Spika asiyekuwa mbabe wala biased. Tunahitaji watu shupavu wanaopiga kelele sio pale tu inapoonekana kuwa ufisadi uliotendeka unagusa maslahi yao binafsi ama wao wameachwa solemba au nje ya ring bali ni kwa ajili ya Watanzania wote. Tunahitaji watu wenye uchungu na maendeleo yetu sisi Watanzania wote na sio maendeleo ya kikanda. Tunahitaji viongozi wanaojua thamani ya Mtanzania mmoja, siyo wa kuruhusu kemikali za sumu kutiririka kwenye mito huko North Mara na kuundia tume badala ya kuchukua hatua immediately. Tunahitaji viongozi wa kuongoza wananchi jinsi ya kupata haki zao. Tunahitaji viongozi wanaojua kuwa kuwatumia polisi kuwatisha wananchi pemba sio suluhisho...Tunahitaji viongozi watakaoona kuwa millioni282 za kuwalipa wahindi wa TRL kw siku ni fedha nyingi sana, eti kukodisha vifaa ambavyo zinazidi kuidhoofisha huduma ya reli nchini, n.k.
 
Naungana na wana JF kwamba tatizo la wanasiasa wengi ni woga wa kudondosha kitumbua chao. Kwa hiyo wanajikuta wanalinda maslahi yao kuliko maslahi ya nchi pale inapofikia kutoa maamuzi yenye risk.

CCM ishajidhihirisha kwamba ni chama cha mafisadi kutokana na mwenendo wa viongozi wao - NEC. Hivyo ni vigumu wala sio sahihi kupambana nao ukiwa ccm. Ni sawa na kukata tawi la mti ukiwa umelikalia.

Mimi naamini kwamba hawa wapiganaji wana nia njema ila tu woga wao unawaponza kiasi kwamba umeyeyusha mbinu na mikakati yao.

Kila kitu kina garama yake. Wajitoe mhanga watoke kwenye kifungo cha CCM. Suala ya kwamba siku moja wapiganaji wataiteka CCM ni ndoto, kwani wanaochagua viongozi ndio hao hao NEC ya CCM sasa wapiganaji watapita wapi kushika usukani. Wajifunze kwa wapiganaji wengine kama G55 walivyosambaratishwa. Nao taratibu watashughulikiwa kimya kimya - tunaona Makamba ameshawafuata huko huko na kuwapunguzia munkari kama Mwanakijiji alivyohojil.

Vita ni vita
 
naungana na wana jf kwamba tatizo la wanasiasa wengi ni woga wa kudondosha kitumbua chao. Kwa hiyo wanajikuta wanalinda maslahi yao kuliko maslahi ya nchi pale inapofikia kutoa maamuzi yenye risk.

Ccm ishajidhihirisha kwamba ni chama cha mafisadi kutokana na mwenendo wa viongozi wao - nec. Hivyo ni vigumu wala sio sahihi kupambana nao ukiwa ccm. Ni sawa na kukata tawi la mti ukiwa umelikalia.

Mimi naamini kwamba hawa wapiganaji wana nia njema ila tu woga wao unawaponza kiasi kwamba umeyeyusha mbinu na mikakati yao.

Kila kitu kina garama yake. Wajitoe mhanga watoke kwenye kifungo cha ccm. Suala ya kwamba siku moja wapiganaji wataiteka ccm ni ndoto, kwani wanaochagua viongozi ndio hao hao nec ya ccm sasa wapiganaji watapita wapi kushika usukani. Wajifunze kwa wapiganaji wengine kama g55 walivyosambaratishwa. Nao taratibu watashughulikiwa kimya kimya - tunaona makamba ameshawafuata huko huko na kuwapunguzia munkari kama mwanakijiji alivyohojil.

Vita ni vita

ina maana hawa ccm wanatufanyia sisi viini macho ????
 
ina maana hawa ccm wanatufanyia sisi viini macho ????
Hii vita hawakuianzisha wao pamoja na kwamba walijua kilichokuwa kinafanyika. Walipoona akina Dr Slaa wanapata umaarufu na uungwaji mkono na Watanzania wakainunua vita hii ili kuwanyamazisha wapinzani. Hawataibua jingine hadi upinzani waseme.
Tutafanya makosa makubwa kudhani kwamba hawa kweli ni wapambanaji. Ilikofika CCM na viongozi wake sio rahisi mapambano haya yakaanzia ndani.
 
Wapambe njaa au wa kutumwa utawaona tu. Hii thread ni kuhusu wapiganaji na wala sio Mwakalinga. Kuna thread ya Mwakalinga kule na unaweza kwenda kutukana utakavyo.

?

Ningeomba wanakyela na vita yao ya Mwakyembe vs Mwakalinga wahamishie thread nyingine kwa sababu wanapotosha maana ya makala ya Mwanakijiji.
 
Nasikia gazeti mojawapo (Tazama Tanzania) limeitumia makala hii na kuandika kuwa nimesema mmoja wa wapiganaji wa CCM (Dr. Mwakyembe) asichaguliwe mwakani? Labda nimeandika vibaya, lakini wale walioisoma sijui na wao wamepata impression ya mimi kusema wapiganaji wasichaguliwe mwakani?
 
Mzee mwanakijiji,
Kwa taarifa yako maelezo yako mengi ni kuonyesha kuwa hawa Wapiganaji ni wasanii watupu.. Na Katika siasa siku zote kuna pande mbili kama sarufi. Unapompiga vita mpiganaji na juhudi zake, moja kwa moja unaonyesha kukubaliana zaidi na upande wa pili hata kama hukuzungumzia kitu.
Mara nyingi wanasiasa wetu hukosea sana wanapoleta zile habaari za siasa za Kutofungamana na upande wowote...hali tunaegemea upande mmoja zaidi... watu hawasubiri kukupa mji!
Ndio maana sisi Tanzania tuliitwa nchi ya Kikomunist kwa sababu tuliegemea zaidi China na Urusi ktk kila baya walozungumzia Ukoloni mamboleo ambao unatafsirika na nguzo za Kibepari..
Kama hupendi Ubepari basi bila shaka wewe ni Mkomunist..
 
Mzee mwanakijiji,
Kwa taarifa yako maelezo yako mengi ni kuonyesha kuwa hawa Wapiganaji ni wasanii watupu.. Na Katika siasa siku zote kuna pande mbili kama sarufi. Unapompiga vita mpiganaji na juhudi zake ni moja kwa moja unaonyesha kukubaliana na upande wa pili hata kama hukuzungumzia.

Hiyo ni tafsiri ya mtu anavyopenda kutafsiri kwani kama ningetaka kusema hicho cha upande wa pili ningeweza kusema. Tatizo linakuja mtu anapozungumza kana kwamba ndivyo nilivyosema. Lengo langu halikuwa kuonesha kuwa wapiganaji ni wasanii watupu, bali mikakati wanayotumia haifai. Kama kweli wanataka kupambana na ufisadi na mafisadi ni lazima waoneshe au kuchagua mikakati bora kuliko hiyo iliyo sasa.

Hivyo, lengo ni kuwakosoa ili wasibweteke katika comfort zones zao.

Mara nyingi wanasiasa wetu hukosea sana kuleta zile habvari za kutofungamana na upande wowote...hali unaegemea upande mmoja zaidi. Ndio maana sisi Tanzania tuliitwa nchi ya Kikomunist kwa sababu tuliegemea zaidi China na Urusi ktk kila baya walozungumzia Ukoloni mamboleo ambao unatafsirika na nguzo za Kibepari..

Ni kweli hilo.
 
Nasikia gazeti mojawapo (Tazama Tanzania) limeitumia makala hii na kuandika kuwa nimesema mmoja wa wapiganaji wa CCM (Dr. Mwakyembe) asichaguliwe mwakani? Labda nimeandika vibaya, lakini wale walioisoma sijui na wao wamepata impression ya mimi kusema wapiganaji wasichaguliwe mwakani?

Mzee Mwanakijiji,

Nimeliona gazeti la TAZAMA na Kichwa cha habari yako kilikuwa 'Chukueni pesa za akina Mwakyembe lakini msiwakubali ukifika uchaguzi!

Mambo mengine kwenye hiyo habari ni copyright na ulivyoituma hapa JF.
 
sasa jamani hata kupotosha kwingine hakuwi na haki; well ni sehemu ya mapambano I guess.
 
sasa jamani hata kupotosha kwingine hakuwi na haki; well ni sehemu ya mapambano I guess.

Hata mimi nilipoona hicho kichwa nikacheka tu na kusema "no comments".

Mimi magazeti ya Tanzania sina hamu nayo na kwa asilimia zaidi ya 90 nimeacha kuamini wanachoandika.

Kwa aina ya uandishi nilioushuhudia na majungu wanayoyaandika, nitakuwa wa mwisho kutumia gazeti lolote la Tanzania kwenye shughuli yangu yoyote.
 
Mkuu Mwanakijiji nimesoma makala yako na kuielewa.

Mi niseme tu kuwa inawakatisha tamaa kabisa wapambanaji wetu wa ufisadi. Pamoja na kwamba hujatangaza kama wewe unawapigia chepuo mafisadi. Lakini uchambuzi wako wa kebehi kwa wapambanaji ni dhahiri umetaka kuonesha kuwa hawa wapambanaji si lolote si chochote mbele ya jamii. Binafsi imenisikitisha hasa kwa kujua kwamba vita hii ni ngumu, ngumu, ngumu sana. Na kibaya zaidi watanzania wengi hatuna uthubutu wa kunyooshea kidole viongozi wezi kwa kuwatuhumu hadharani, wengi ni wajanja wa kwenye keyboards, na kulalamika tu around "watu wetu".

Hivi kweli kabisa kwa upeo wako mkubwa unaamini, hawana wanalolifanya. Bunge letu lina wabunge zaidi ya 300, hao wanaosimama kidete ni kama 12 tu, lakini bado wanawanyima usingizi mafisadi. Sasa nashindwa kuwaelewa misimamo yenu watu wengine, au mnaandika tu kucreate confusion kwenye jamii, maana mara mnapinga ufisadi kwa nguvu zote mara mnakebehi wanaopigana na ufisadi... Wananchi hawajui in the end wamchague nani!

Hakuna mpambanaji aliye mkamilifu. Hata wewe Mwanakijiji pamoja na umahiri mkubwa ulionao, bado kuna watu wanaweza kusema mbinu unayotumia ya fimbo ya mbali kwa kurusha madongo ukitokea majuu ni dhaifu na haitatokomeza ufisadi Tanzania. Kila mwenye kuchangia vita hii apewe moyo badala ya kubezwa...Hakuna njia moja, hakuna njia rahisi, lakini tumeona kelele zao za mlango, zinawanyima wenye nyumba usingizi pamoja na mapungufu yao yooote uliyoyaonesha.

Safari ya maili 100 inaanaza kwa hatua moja. Kwa aina ya watu tulionao sasa hivi Tanzania, na woga uliokithiri wa watanzania wengi, unafiki na ubinafsi ulioshindikana. Hawa jamaa wamejitoa muhanga kwelikweli mi nasema, hata kama in the process nao wanalinda mkate wao.

Hivi jamani mmewahi kujiuliza dili za kifisadi zilizokuwa kwenye pipeline moments kabla ya EL kutemwa?...Ufisadi ulikua kwenye full throttle Dec 2007, baada ya EL kutemwa dili nyingi zimekua shelved lakini hazijawa cancelled, wanasubiri moment yao tena wamalizie kuingiza nchi mikataba ya ajabu. Bila ya hawa watu tunaowabeza sasa hivi, nchi hii by now ingebaki watu wake tu kuuzwa(exag!). Watu walishagawana sekta nzima nzima za kujimiliksha kwa vizazi na vizazi lakini sasa wanahaha.
 
Nasikia gazeti mojawapo (Tazama Tanzania) limeitumia makala hii na kuandika kuwa nimesema mmoja wa wapiganaji wa CCM (Dr. Mwakyembe) asichaguliwe mwakani? Labda nimeandika vibaya, lakini wale walioisoma sijui na wao wamepata impression ya mimi kusema wapiganaji wasichaguliwe mwakani?
Mwenye post hii ifuatayo atakuwa anajua mengi kuhusu habari kutokea katika hilo gazeti https://www.jamiiforums.com/589431-post28.html
 
Mkuu Mwanakijiji nimesoma makala yako na kuielewa.

Mi niseme tu kuwa inawakatisha tamaa kabisa wapambanaji wetu wa ufisadi. Pamoja na kwamba hujatangaza kama wewe unawapigia chepuo mafisadi. Lakini uchambuzi wako wa kebehi kwa wapambanaji ni dhahiri umetaka kuonesha kuwa hawa wapambanaji si lolote si chochote mbele ya jamii. Binafsi imenisikitisha hasa kwa kujua kwamba vita hii ni ngumu, ngumu, ngumu sana. Na kibaya zaidi watanzania wengi hatuna uthubutu wa kunyooshea kidole viongozi wezi kwa kuwatuhumu hadharani, wengi ni wajanja wa kwenye keyboards, na kulalamika tu around "watu wetu".

Hivi kweli kabisa kwa upeo wako mkubwa unaamini, hawana wanalolifanya. Bunge letu lina wabunge zaidi ya 300, hao wanaosimama kidete ni kama 12 tu, lakini bado wanawanyima usingizi mafisadi. .

Kwa staili ya hizi makala za kejeli wabunge wengi wataendelea kula jiwe bungeni, kusinzia au kula bata tu dom, maana wakisema sana watajikuta kwenye fungu la kuandikiwa nyaraka/makala za kejeli na watu kama akina Mwanakijiji, japo mwishoni wa makala anaonekana kuwashauri lakini ukweli ni kuwa makala hii imekuwa mtaji wa mafisadi haijakaa KUSHAURI bali KUKEJELI. Watz hii vita ni ngumu sana na nadhani mnakumbuka hapo nyuma kidogo kuna wanasiasa au waliokwenda kinyume na maslahi ya mafisadi wa nyakati zile walipoishia, kuna hata waliopoteza maisha. Wengi wetu humu JF hatutaki hata kufahamika majina, sura, hata tunapoishi wakati tunaposhiriki mijadala ya humu JF. Lakini ni namba wani kuchallenge, lakini kuna watu (wabunge) wamejitolea kuyasema maovu hadharani na mchana kweupe. Hawa tuwaunge mkono, kuwashauri na kuwatia moyo.

Hata hizo scandals zinazodaiwa kuibuliwa kwanza hapa JF haziwezi kuwa na maana yeyote kama hatapatikana mtu wa kuthubutu kuzitoa humu na kuzimwaga duniani.
 
Mwanakijiji inaonekana anauma na kupuliza huku na kule. Kuna mmoja wa wachangiaji alisema watu wajiandae kusoma makala za Mwanakijiji kule Rai na Tazama Tanzania. Namnukuu: "Wanakyela jiandaeni kusoma hoja za Mwanakijiji kupitia RAI na TAZAMA TANZANIA".
 
Kwa staili ya hizi makala za kejeli wabunge wengi wataendelea kula jiwe bungeni, kusinzia au kula bata tu dom, maana wakisema sana watajikuta kwenye fungu la kuandikiwa nyaraka/makala za kejeli na watu kama akina Mwanakijiji, japo mwishoni wa makala anaonekana kuwashauri lakini ukweli ni kuwa makala hii imekuwa mtaji wa mafisadi haijakaa KUSHAURI bali KUKEJELI. Watz hii vita ni ngumu sana na nadhani mnakumbuka hapo nyuma kidogo kuna wanasiasa au waliokwenda kinyume na maslahi ya mafisadi wa nyakati zile walipoishia, kuna hata waliopoteza maisha. Wengi wetu humu JF hatutaki hata kufahamika majina, sura, hata tunapoishi wakati tunaposhiriki mijadala ya humu JF. Lakini ni namba wani kuchallenge, lakini kuna watu (wabunge) wamejitolea kuyasema maovu hadharani na mchana kweupe. Hawa tuwaunge mkono, kuwashauri na kuwatia moyo.

Hata hizo scandals zinazodaiwa kuibuliwa kwanza hapa JF haziwezi kuwa na maana yeyote kama hatapatikana mtu wa kuthubutu kuzitoa humu na kuzimwaga duniani.

Kusema ukweli makala hiyo ukiisoma peke yake unaweza ukafikiria ni kejeli au kebehi; tatizo linakuja pale mtu anapoanzia katikati bila kuangalia makala mbili zilizotangulia hiyo. Makala hiyo ilikuwa na lengo la kuonesha udhaifu wa mikakati ya wapambanaji CCM na udhaifu ambao tayari umeonesha kuwa na ukweli.

Kejeli na kebehi (sarcasm na satire) ni sehemu ya uandishi; vina lengo la kuonesha ukweli fulani katika lugha ambayo ni kama kinyume hivi. Na ukiangalia utaona kuwa kama wataendelea na mikakati hiyo hiyo niliyoianisha kama tulivyoona ndugu ya Mwakyembe akirudia tena kulalamika basi wajiandae kuanguka na kama nilivyosema nitakuwa ni mtu wa mwisho kushangazwa.

Lengo langu ni kuonesha ni jinsi gani mikakati yao siyo ya ushindi. Hili hata hivyo siyo sawa na kusema mtu asichaguliwe isipokuwa katika maono na mtazamo wa mnufaika wa ufisadi.
 
Mkuu Mwanakijiji nimesoma makala yako na kuielewa.

Mi niseme tu kuwa inawakatisha tamaa kabisa wapambanaji wetu wa ufisadi. Pamoja na kwamba hujatangaza kama wewe unawapigia chepuo mafisadi. Lakini uchambuzi wako wa kebehi kwa wapambanaji ni dhahiri umetaka kuonesha kuwa hawa wapambanaji si lolote si chochote mbele ya jamii.
Ukisoma vizuri utaona kuwa sijamchambua mpambani mmoja mmoja, nilichochambua ni mikakati wanayotumia na kuionesha ni jinsi gani ni dhaifu. Hapa utaona kuwa kama mimi naweza kuiona hivyo je mafisadi na makuwadi wao wanaionaje?

Binafsi imenisikitisha hasa kwa kujua kwamba vita hii ni ngumu, ngumu, ngumu sana.
Hii vita ni lazima iwe ngumu vinginevyo isingekuwa vita. Ndio maana kabla ya kusoma hiyo makala mtu alitakiwa kusoma makala zilizotangulia ile ya "Ukosoaji wa Wa wazi wa Wapambanaji" na "Tukiwachagua tena (makuwadi wa ufisadi) 2010 tumekwisha".
Na kibaya zaidi watanzania wengi hatuna uthubutu wa kunyooshea kidole viongozi wezi kwa kuwatuhumu hadharani, wengi ni wajanja wa kwenye keyboards, na kulalamika tu around "watu wetu".
Wengine labda hawana uthubutu huo, mimi embe naita embe na kama ni bolibo naita bolibo na siyo sikio au ngong'wa!

Hivi kweli kabisa kwa upeo wako mkubwa unaamini, hawana wanalolifanya.
Sijui umepata wapi wazo kuwa naamini hawana wanalolifanya.

Bunge letu lina wabunge zaidi ya 300, hao wanaosimama kidete ni kama 12 tu, lakini bado wanawanyima usingizi mafisadi.
Ni kitu gani kinakufanya uamini kuwa mafisadi wanakosa usingizi!? Umemsikia mbunge yoyote anayehusiana na ufisadi akilalamika kuwa anataka kuondolewa au anachezewa rafu jimboni kwake? Umesikia kiongozi yoyote anayehusishwa na ufisadi akifanya mikutano mikubwa ya hadhara kujaribu kuelezea kinachoendelea? Hivi kule Dodoma waliokosa Usingizi ni wale waliotaka kumuondoa Sitta au ni wale watu wa upande wa Sitta waliojikuta wanakaribiwa kuzidiwa nguvu? Ukitenda kazi kwa kudhania kuwa mafisadi wanakosa usingizi utafanya makosa makubwa sana.

Sasa nashindwa kuwaelewa misimamo yenu watu wengine, au mnaandika tu kucreate confusion kwenye jamii, maana mara mnapinga ufisadi kwa nguvu zote mara mnakebehi wanaopigana na ufisadi... Wananchi hawajui in the end wamchague nani!
Wananchi wanatakiwa wapewe pande zote za hoja na mjadala wote ili watakapochagua wajue wanachagua nani. Wale wanaopigana na ufisadi ni lazima wajioneshe kuwa wanapigana kweli na ufisadi!

Hakuna mpambanaji aliye mkamilifu. Hata wewe Mwanakijiji pamoja na umahiri mkubwa ulionao, bado kuna watu wanaweza kusema mbinu unayotumia ya fimbo ya mbali kwa kurusha madongo ukitokea majuu ni dhaifu na haitatokomeza ufisadi Tanzania.
Si kweli, mbinu zangu mimi ni advanced kuliko unavyofikiria na matokeo yake yanagusa ardhini moja kwa moja; angalia rekodi yangu. Wanaofanya shughuli zao wakidhani yangu ni "fimbo ya mbali" wanafanya hivyo kwa maangamizi yao wenyewe. Niko karibu na Tanzania kuliko wale walioko ardhini! think about it.

Kila mwenye kuchangia vita hii apewe moyo badala ya kubezwa...
Huwezi kumpa mtu moyo kama anapigana vibaya ni kutaka kumuumiza. Unapoingia vitani huku una mshale na upinde wakati mwenzio anakuja na AK-47 na M16 na Uzzi na mabomu ya kurushwa kwa mikono tutakuwa tuna wazimu tukisimama pembeni na kukushangilia na kukutia moyo! Kama tunataka kukusudia hatuna budi kuonesha ni jinsi gani upinde na mshale havitafua dafu mbele ya silaha za moto licha ya nia yako nzuri.

Hakuna njia moja, hakuna njia rahisi, lakini tumeona kelele zao za mlango, zinawanyima wenye nyumba usingizi pamoja na mapungufu yao yooote uliyoyaonesha.
Kuna njia bora na njia mbovu; mikakati 14 niliyoinesha nimeionesha kuwa ni mibaya na itawaangusha. Kama nimefanya makosa nioneshe uzuri wa mikakati hiyo unaweza kunibadilisha mawazo. Mikakati bora ipo na hawako tayari kuichukua.

Safari ya maili 100 inaanaza kwa hatua moja. Kwa aina ya watu tulionao sasa hivi Tanzania, na woga uliokithiri wa watanzania wengi, unafiki na ubinafsi ulioshindikana. Hawa jamaa wamejitoa muhanga kwelikweli mi nasema, hata kama in the process nao wanalinda mkate wao.
Kujitoa mhanga sidhani; kujitolea inawezekana. Kama wanataka kwenda kupigana kweli basi waende kamili kamili siyo mambo yale ya kupigana kama mtu hataki.

Hivi jamani mmewahi kujiuliza dili za kifisadi zilizokuwa kwenye pipeline moments kabla ya EL kutemwa?...Ufisadi ulikua kwenye full throttle Dec 2007, baada ya EL kutemwa dili nyingi zimekua shelved lakini hazijawa cancelled, wanasubiri moment yao tena wamalizie kuingiza nchi mikataba ya ajabu.
Hivi EL ana wasiwasi wowote wa kutorudi Bungeni mwakani au kuwa na nguvu ndani ya chama?

Bila ya hawa watu tunaowabeza sasa hivi, nchi hii by now ingebaki watu wake tu kuuzwa(exag!). Watu walishagawana sekta nzima nzima za kujimiliksha kwa vizazi na vizazi lakini sasa wanahaha.
laiti hilo lingekuwa kweli! Nchi bado iko mikononi mwa mafisadi na hatujapigana kuwanyang'anya tunapigana kutoka droo! Tusipobadilisha mikakati tumekwisha!
 
sasa jamani hata kupotosha kwingine hakuwi na haki; well ni sehemu ya mapambano I guess.
Mzee MWanakijiji, Katika makala zako zote hii hapa ndio inabeba vita dhidi ya ufisadi na ndio maana vita hii imegeuzwa kuanzia na mkakati huu, Hivyo hata kauli za wakina Mwinyi, Makamba, Sitta, Mwakyembe zote zinaweza kuingia hapa na kuona jinsi gani wanavyocheza makida makida(mzaha) kwa ajili yao CCM waje na List yao
 
Back
Top Bottom