Pale upinzani unapoacha kujadili mambo msingi na kuweka nguvu zao kumjadili Makonda! Tuna wapinzani wa hovyo sana!

Naanza kuelewa Sasa, huwenda ni kweli kwamba Watanzania ni watu wa hovyo na ambao hawawezi Kila kitu na hawawezi Kuibadirisha nchi Yao kutoka Hali mbaya ya umasikini na kuwa nchi yenye neema na uchumi mkubwa

Tumeshindwa kuendesha bandari zetu wenyewe, mbuga zetu tunawapa wageni, Bado tutawapa pia SGR, Tanesco na Hata Ikulu ikiwezekana ili wageni wakae hapo, hii ni kwa sababu moja tu ambayo ni, Majungu na wivu wa kijinga!

Wenzetu wa nchi zinazoendelea, Kila kukicha wanazalisha mawazo mapya ya kipi wafanye ili kitokee kikubwa zaidi,

Hii ni tofauti kabisa na nchi yetu, watu wamejaa wivu na ujinga mwingi, wapo tayari kushinda mitandaoni kumjadili mtu na kumnanga na Bado kusiwe na matokeo yoyote

Ni ajabu kama nchi isimame kisa Paul Makonda ameaminiwa na Rais kupewa ukuu wa mkoa

Umasikini wa Watanzania unatokana na ujinga wa wanaoitwa watetezi wa wananchi kwa maana kwamba wao ni mbadara wa wanaotupeleka chaka na kutufanya tuwe na MAISHA magumu!

Ikiwa mambo haya ni kweli ni yamekuwa agenda kwa wapinzani, basi tunaupinzani wa hovyo na usio na malengo yoyote na nchi yetu

Okay! Tufanye Makonda ameondolewa kwenye nafasi hiyo, wewe unapata faida Gani kama mpinzani, Makonda amekuwa nje ya mfumo wa serikali Karibu miaka miwili unusu hivi, wapinzani, kwa kipindi hiko mmebadirisha nini na kipi kimeshindikana kufanywa na nyinyi baada ya Makonda kupewa nafasi aliyopo?

Tukumbushane tu kwamba, Jambo linaloamriwa na MUNGU mwenyewe kama ambavyo mmeamini Mbowe kuwepo hapo kama M/kiti wa chama chetu CHADEMA kwamba ni Mungu alimpa, ndivyo anaweza kufanya kwa Makonda na kwa mwingine

Suala la dhambi mnayoiona kwa macho yenu kwa Makonda, mkumbuke pia Iko dhambi pia ambayo hamjawahi kuiona kwa mliowaamini kuwa wao ni malaika, lakini jicho la Mungu linajua na kwa wote hawasitahili kuwepo kama mnavyomwombea Makonda

Fanyeni kazi acheni Majungu na wivu wa kijinga!

Makonda chapa kazi usisikilize kelele za chura

Niwakumbushe hivi!

Iwapo Mungu amekuwa upande wa Makonda, mtaomba mno Dua zenu na hazitafanya lolote dhidi yake
Wapinzani wako ndani ya CCM,wakipanga mikakati na kufanyiana timing na figisu wao kwa wao.
 
Back
Top Bottom