Padre na Trafiki!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Padre mmoja akiwa kwenye gari alisimamishwa na Trafic Police,police akiwa anahitaji rushwa alianza kuuliza maswali mengi, mara mbona gari lako linatoa moshi mwingi? mbona gari lako matairi yameisha, hatimaye polisi akamuamuru padre waende nae kituoni.
Njiani polisi alimuuliza padre, umesema wewe ni padre, je unabiblia ndani ya gari, padre akajibu ndio ninayo, polisi akamuambia padre, pack gari pembeni na unipe biblia. Padre akapaki gari na kumpa biblia yule polisi,
Polisi akasita kupokea, akamwsambia Padre 'fungua na usome Matayo 5:25-26 "Mtu wa Mungu akasoma ": malizaneni na aliyekukamata kukupeleka mahakamani.. ..malizaneni upesi.. yamalize mambo haya mngali bado njiani kabla hajakukabidhi kwa hakimu... ambaye aweza kukuhukumu na kukukabidhi kwa bwana jela ili akutie gerezani. Amin nakwambia hautaachiwa hadi umetoa senti ya mwisho...

Mtu wa Mungu akampa yaliyo yake kaizari. Polisi akatabasamu na kusema 'msifanye migumu mioyo yenu.. nenda na amani
 
biblia hipi?

Biblia hii hiii "Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako
ana ugomvi nawe,
24
iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu
yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
25
"Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani,
kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi
kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
26
Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza
kulipa senti ya mwisho."
 
Hii mitabu mingne bwana...!bure kabisa...!!bora FRANK WOOD kuliko hiko kitabu chenu.
 
Nakumbuka hii kitu nimewahi kuisikiliza kenye Nigerian Commedy...... Jamaa amekopi na kupest ila tu kabadili lugha. Tunamshukuru kwa kutusambazia wadau....
 
Tehe tehe tehe !
Ngoja niinakiri hii mistali kwenye note book yangu. Jumatatu nahakikisha naenda kazini na biblia. Atakaeleta ukauzu namsomesha.
 
Back
Top Bottom