Otango Osale ni nani huyu mtu?

Hivi mnaposema waliwasumbua wazungu ni serious kweli? hilo tu kutaka kungonoka na maadui ni udhaifu kwenye harakati.
C.C Elli

serious mkuu.....mpaka ikabidi aletwe mtalaamu kutoka nje.......baba usifanye mchezo kuoana papuchi live bila chenga....ukumbuke wao walikuwa hawaonekani na wazungu.....
 
Hivi mnaposema waliwasumbua wazungu ni serious kweli? hilo tu kutaka kungonoka na maadui ni udhaifu kwenye harakati.
C.C Elli
hahahhaha Mpwa wangu kila mtu ana udhaifu na uzuri wake, hawajamaaa ni kweli waliwapa hard times wazungu
 
Such interesting story..nadhani wajuvi Wa hili watatupakulia hasa kilichojiri enzi hizo
 
Heshima mbele waikuu hapa JF. Tangu nikiwa mdogo na mpaka sasa nimemaliza miaka 3 sasa nasikia baadhi ya watu wakisimulia habari kuhusu mtu mmoja aitwaye Otango Osale, tafadhali wakuu mwenye historia yake atupie hapa tupate kumfahamu vizuri.
Nawasilisha

John Tongo,

Jina ni Osale Otango.
Alikuwa na mwenzake anaitwa Paul Hamisi.

Osale Otango alikuwa Mjaluo na Paul Hamisi Msambaa.
Hawa waliwapa shida sana Wazungu kwa vitendo vyao.

Mengi yameandikwa kuhusu watu hawa ambao wakijificha katika mapango
ya Amboni.

Binafsi nimesoma hayo hayo ya katika magazeti miaka mingi nikiwa mtoto.
Bado sijaona kazi ya kisomi juu ya watu hawa.

Kuna baadhi wanawaita hawa wapigania haki ya Muafrika na kuna wengine
wanawaona walikuwa majambazi wa kawaida.

Nami ningependa kupata habari kamili za watu hawa.
 
habari zao zimekuwa kama kadithi fulani tu....nakumbuka nilienda amboni wa wenzangu tulihadithiwa juu juu tu na kwabahati nzuri tulionyeshwa kijitabu kidogo cha historia ya hawa watu na picha zao........
 
osale otango nilivyohadithiwa ni mpiganaji wa mkoa huo kuukomboa tanga kutoka kwenye makucha ya masetla.wamiliki wa mashamba makubwa.walijaribu kuipigania tanga kilichowaponza ni watanga wenyewe kutoa siri walipo .waliuawa ila imekuwa laana Kwa vizazi vya tanga .watu wa tanga ni vigeugeu hawaaminiki .hadi osale arudi .
 
Tafadhali mwenye historia angalau robo tatu ya kamili ya hawa watanzania atuwekee hapa! Sio wote wenye uwezo wa kufika Amboni mapangoni ili kupata historia halisi wengine tupo huku Misungwi Jiwe kuu karibu na Kolomije.
 
john tongo, OSALE OTANGO alikuwa mpigania uhuru (freedom fighter) kutoka mkoani Tanga kwenye miaka ya 1950. Baadaye alihama kutoka maeneo ya LUSHOTO akahamia Amboni TANGA na kwenye yale mapango ndipo walipokuwa wanajificha. ENDELEA KUTAFITI MKUU.
Mkuu OSALE OTANGO alikuwa ni mpiganaji wa KIKENYA,,aliyekuja kujificha kwenye MAPANGO YA AMBONI TANGA,,,inasemekana alikuwa mmoja wa wapiganaji wa VITA VYA MAUMAU nchini KENYA....kwa majibu wa hadithi za wazee..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom