Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

Mkuu mie nimeshaacha kuangalia vipindi vya kundi hili
hakuna maadili ya sanaa pale. Hata punch haziwi hivyo. wasidhani katuni tunazochora kwenye magazeti wanaweza kuziigiza kwenye runinga.
kazi kweli kweli
 
Yego Geoff,

Kundi hilo limesimama kivyake vyake na ni jinsi gani wewe mwenyewe utakavyo lielewa na maana kuwa kama orijino comedi unaielewa na waelewa wanachokifanya basi wewe wastahili kuangalia hicho kipindi na kama huelwe kabisa wanachokifanya basi wewe hustahili kuangalia icho kipindi waacha wale waelewao waendelea kukitizama kipindi hicho,

Tafuadhali pima upepo wa mtazamo wako ktk vipindi vingi au mwaswala yeyote uyaonapo na uyapambanue ujue lipi nalipi si sawa na nisawa
 
najuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuta kuwafahamu
churrrrrrrraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Wandugu kwa mtazamo wangu naona hawa vijana tangu waondoke pale EATV kama wamepote kabisa katika anga la vichekesho je ikoje hiyo wa JF
 
Wandugu kwa mtazamo wangu naona hawa vijana tangu waondoke pale EATV kama wamepote kabisa katika anga la vichekesho je ikoje hiyo wa JF
Hata mimi naona maana hata hamu ya kuangalia show hiyo kwangu binafsi imepungua ukilinganisha na walipokuwa EATV. Sikui kama hawa TBC1 wanawabania baadhi ya vitu.
Nafuu hawa FUTUHI nao wanakuja juu!
 
Wandugu kwa mtazamo wangu naona hawa vijana tangu waondoke pale EATV kama wamepote kabisa katika anga la vichekesho je ikoje hiyo wa JF
KUNA mambo mawili huenda yakawa yametokea kwa hawa vijana.
1...........watazamaji tumewazoea na hawana jipya lakutuchekesha kama mwanzo , enzi hizo masanja alikua kinara ktk vitimbi vyao..nyota iliwaka.

2...........Kupata kwao udhamini/ufadhili wa kina Yusuph Manji, uliwaongezea kipato, hivyo upo uwezekano kua wamelewa mafanikio, hivyo kiburi kimeongezeka. na sasa wanakula fungate la juhudi zao.

baada ya sababu hizo za kiufundi lipo moja la laana ya Mzee Mengi, maana vijana walimtusi sana baada ya kusign mkataba na TBC , wakasahau fadhila zake zote.
ila nakubaliana nawe kua mvuto umepotea.

 
Mnakumbuka wosia wa Shigongo kwa vijana hawa?
nikweli ERICK SHIGONGO ALIANDIKA MAKALA NZIMA, kuwaasa na kuwashauri njia nzuri ya kupita, unajua wao walijibu kwa kejeli na majivuno.....katika maisha kuna kupanda na kushuka, ila hawa vijana anguko lao limekuja mapema mno, bado hawakupaswa kuwa katika daraja hili, wanatokomea, hata thamani yao ya mialiko imeshuka, sasa unaweza kuwakodisha kwa milioni tatu wakaja kumburudisha mwanao kwa masaa zaidi ya matatu sebuleni kako.
 
laana ya Mzee Mengi, maana vijana walimtusi sana baada ya kusign mkataba na TBC , wakasahau fadhila zake zote.

hilo linawezekana hawa vijana walimtusi sana mzee Mengi, licha ya kutambua mchango wake kwao
 
hilo linawezekana hawa vijana walimtusi sana mzee Mengi, licha ya kutambua mchango wake kwao
kupitia kwao lipo jambo la kujifunza nalo nikua, unapopanda usiwatusi wale waliokupa mbeleko, maana utakapo kuwa unashuka utawakuta wao wanapanda juu, Mengi bado yuko juu baada ya dharau na kejeli zao, bila shaka Seki ipo siku atamuomba radhi hadharani huyu mzee. maana ni heri masanja hana mambo mengi katika historia yake lakini kijana Sekioni, hadi aibu, na niyeye ndie aliekua mtu wa kati katika kelele nyingi zilizopazwa na kundi hilo......
 
Dah kweli sasa hawa vijana wanakoelekea ni kufulia kwa wasanii kwakutokuwa na malengo ya muda mrefu balaa litawafika wasipokuwa makini nowadays wamepoteza ule umaarufu
 
Waraka wa Shigongo kwa Ze Original Komedi


Wekezeni, acheni kiburi cha umaarufu na fedha

Kwenu wadogo zangu.

Masanja, Joti, Mpoki, Wakuvwanga, McRegan, Seki na Vengu.

Nianze kwa kuwakumbusha msemo wa Kiingereza usemao “You can not be a champ for life, one day you will go off and some else will come” sikumbuki vizuri msemo huu kwa mara ya kwanza ulisemwa na nani lakini ni wa zamani hapa duniani na maana yake haichuji kila siku ni mpya, kwamba huwezi kuwa bingwa milele lazima uondoke bingwa mwingine aje!

Najua mlitarajia kwa jambo mlilonifanyia ningeibuka na kisasi, mimi si mtu wa aina hiyo, mwenzenu Dudubaya aliwahi kupewa saa nzima kwenye kipindi cha Nani ni Nani Channel Ten, akanitukana matusi yote aliyoyafahamu lakini sikulipa kisasi, baadaye alipowekwa ndani akikaribia kufungwa ni mimi niliyemtoa mahabusu! Sikufanya hivyo kwa kutafuta sifa bali kutimiza kile kisemacho Wasamehe waliokukosea, leo hii Godfrey Tumaini ni rafiki yangu mkubwa...

Uamuzi niliouchukua si kupigana nanyi, maana ugomvi wa sisi kwa sisi hautasaidia chochote, bali nimeamua kuwapeni ushauri ili mfahamu kwamba kila enzi ina mabingwa wake, leo hii ninyi ni mabingwa lakini mfahamu kwamba wengine watakuja ninyi mtaondoka hivyo badala ya kuwacheka na kuwatukana watu, ni vizuri mkawekeza.

Enzi zile za Hitler aliyeua Wayahudi milioni sita duniani kote hakuna binadamu aliyewahi kuwaza eti siku moja angekuja kutokea mtu aitwaye Osama Bin Laden autingishe ulimwengu kwa mauaji na kusakwa bila mafanikio! Enzi zile za tajiri John D. Rockerfeller hakuna mwanadamu aliyewahi kufikiri atakuja mtu aitwaye Bill Gates au Warren Buffet na kuwa tajiri namba moja.

Enzi zile za Pele hakuna binadamu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Christiano Ronaldo au Messi, enzi zile za Mohamed Ali akiwa bingwa wa Ndondi wa dunia hakuna mtu aliyewahi kufikiri atakuja kutokea mtu aitwaye Mike Tyson na katika enzi za King Majuto, Mzee Small au Jangala aliyetuweka kila siku usiku tumezunguka redio kusikiliza michezo ya kuigiza, hakuna Mtanzania aliyewahi kufikiri kwamba ipo siku mngekuja kutokea ninyi. Kweli kila enzi na watu wake.

Mmekuja na mtapita kama walivyopita wengine wengi waliotangulia kabla yenu, ambao leo hii ukiwatafuta utashangazwa na maisha wanayoishi ingawa waliwahi kutingisha Taifa letu na wengine Dunia, baadhi wanateseka wakisubiri kusaidiwa! Kwenu hivi sasa jua linawaka lakini giza linakuja.

Mifano niliyoitoa ya watu niliowaongelea hapo juu inaonesha kwamba hakuna binadamu anayeweza kubaki bingwa siku zote, lazima aondoke ili kutoa nafasi kwa mabingwa wengine, tutake tusitake ni lazima tuondoke hivyo ni lazima kufanya mambo sahihi wakati huu tukiwa katika ubingwa wetu. Huu ndiyo ujumbe wangu kwenu leo.

Swali linalowasumbua watu wengi duniani na ambalo kila mtu mwenye akili timamu ni lazima ajiulize ni hivi siku nitakayotupwa nje nitafanya nini? Itakuwaje siku nitakayokuwa siwezi kucheza soka? Nitafanya kitu gani siku nitakayokuwa siwezi kuchekesha luningani na watu kunishangilia kila ninakopita? Kama binadamu mwenye akili timamu ambaye umaarufu haukupagawishi ni vizuri kujiuliza maswali haya kwani kila mmoja wetu siku moja atajikuta yupo nje ya mchezo.

Wadogo zangu,
Ilikuwa niwaandikie Waraka huu tangu wiki mbili zilizopita baada ya kunitoa kwenye kipindi chenu cha Orijino Comedi na rafiki yangu mpendwa aliyewahi kuwa mshindani wangu wa Biashara huko nyuma Mashaka Matongo au Abiola! Ingawa hamkututaja majina yetu lakini kila mtu aliyekiona kipindi hicho alielewa mliwalenga nani na nani na nina uhakika aliyetoa wazo hilo ni Sekioni David kwa sababu yeye ndiye aliwahi kuwa rafiki wa karibu sana na Mashaka Matongo enzi hizo wakiigiza pamoja katika kikundi cha MAMBO HAYO, pia akiwa mfadhili wake mkubwa.

Kwa wale ambao hawakubahatika kukiona kipindi hicho nitawasimulia kidogo; kilichotangazwa na vijana hao maarufu hivi sasa nchini Tanzania wakitembelea magari ya kifahari na kufanya kila aina ya starehe wanayoona inafaa ni kumwonyesha Bw. Mashaka Matongo ambaye huko nyuma aliwahi kumiliki magazeti kadhaa Pendwa akiwa amefilisika vibaya! Kazi yake hivi sasa eti ni kunyoa nywele huko Sinza na kuomba misaada kwa watu! Wakanionesha mimi kama mtu aliyefanikiwa ‘sana’ kuliko Mashaka Matongo katika kazi hiyo na kumcheka wakimfanya mjinga.

Inawezekana kwa kunionesha mimi niko juu na mwenzangu akiwa amefilisika mlifikiri ningefurahishwa na kitendo hicho, naomba niwaeleze wazi kwamba mimi si mtu wa aina hiyo, wanaonifahamu wanaelewa na kitendo hicho hakikunifurahisha hata kidogo, sipendi umaarufu wa bei nafuu (Cheap popularity) napenda ninapopewa sifa iwe ni halali na ya kutolea jasho. Mpaka leo ninapowaandikia makala hii binafsi sielewi mwenzangu alijisikiaje baada ya dhihaka hiyo kurushwa na TBC 1 ambayo Mkurugenzi wake ni mtu ninayemheshimu sana katika fani hii, Tido Mhando.

Kilichonituma niandike makala hii ni kuwakumbusha wadogo zangu wa Orijino Komedi kwamba, maisha ni safari ndefu. Kwa kuonekana kwenye luninga kila Alhamisi na Jumapili, kupita huku na kule wakishangiliwa, wasijione wamefika kwenye kilele cha mafanikio na kuanza kucheka wenzao, ninachofahamu mimi na uelewa wangu mdogo juu ya mafanikio ni kwamba safari kwao ndiyo kwanza imeanza.

Safari ya maisha ni ndefu wadogo zangu, hakuna sababu ya mtu kumcheka mwenzake. Mzee mmoja aliwahi kuniambia ni kama safari ya kwenda umbali wa kilometa elfu moja kwa miguu, kila mtu ataondoka kwa staili yake. Mwingine atakimbia mwingine atatembea au kutambaa zote hizo ni safari lakini hakuna mwenye uhakika kwamba atafika mwisho wa safari yake salama kiasi cha kuwacheka wenzake, hiki ndicho ninachotaka kuwaeleza wadogo zangu wa Orijino Komedi.

Ninachojua mimi hakuna anayeweza kukimbia umbali wa kilometa elfu moja bila kupumzika, lazima mahali fulani mbele ya safari atachoka na kuketi chini ya mti ili kuwapisha wengine wapite na pengine huo ndiyo ukawa mwisho wa safari yake huku uliowaacha nyuma wakitembea taratibu wakipita na kukuambia “Mzee tunatangulia” huu ni ukweli.

Inavyoonekana kwa hivi sasa wadogo zangu wa Orijino Komedi mmeanza safari yenu kwa kukimbia kiasi cha kujiona ni wajanja kuliko wanaotembea hata kufikia hatua ya kuwacheka kama mlivyofanya kwa Mashaka Matongo ambaye huko nyuma alimlisha na kumtunza Sekioni! Mmesahau kwamba mbele ya safari ni lazima mahali fulani mtapumzika na waliokuwa wakitambaa na kutembea wakaja na kuwapita mkiwa chini ya mti, nimekwishawaeleza hapo juu kwamba binadamu huwezi kuwa bingwa milele lazima siku moja utoke na wengine waingie, kumbukeni walikuwepo mzee Majuto na Small kabla ninyi hamjaja.

Kibaya zaidi na kinachositikisha ni kwamba mmeanza hata kuwatukana watu waliowasaidia kufika mlipo leo! Hiki ni kitendo cha ukosefu wa shukrani cha kiwango cha juu kabisa ambacho nimewahi kukiona chini ya jua. Kila Mtanzania anafahamu mlipotokea, namna ambavyo mtu kama Reginald Mengi na vyombo vyake vya habari amesaidia kuwafikisha ninyi kwenye mwanga, ambaye hakika hamuwezi kusimama mahali popote duniani kutoa historia yenu mkaacha kutaja jina lake, lakini huyu ndiye amekuwa mtu wa kutukanwa kila siku katika vipindi mnavyofanya! Hili ni jambo la kusikitisha sana.

Najua mnatiwa kiburi na utajiri wa fedha na umaarufu ambao hivi sasa mnao! Mmethibitisha ile kauli kwamba hakuna kitu kigumu duniani kwa mwanadamu kuwa na fedha au mafanikio halafu akabaki yule yule! Fedha na umaarufu ni shetani, huwabadilisha watu na kuwapa tabia ambazo huko nyuma hazikuwahi kuonekana, sitaki kuwahukumu wadogo zangu lakini jambo hili limethibitika kwa matendo mnayoyafanya hivi sasa.

Najua mnatumiwa na watu kutimiza malengo yao, mambo mnayoyafanya si yenu yote, baadhi ni ya kuwafurahisha watu wanaowaweka mjini! Lakini kumbukeni mfano wa Mzee Kijiti aliyesafiri kwenda miji ya mbali akimwacha mke wake nyumbani, akiwa huko ashki ya tendo la ndoa ilimshika na kujikuta akitafuta mwanamke wa kuondoa haja yake.

Akifahamu kuna gonjwa la Ukimwi mzee huyo alilazimika kutafuta mpira wa kujikinga na gonjwa hilo. Kwa mahali alipokuwa ilikuwa kazi kidogo kupata mpira huo, akazunguka huku na kule kwenye vibanda bila mafanikio, mwili wake ukiwaka tamaa ya ngono. Mwisho mhudumu wa nyumba ya wageni aliyofikia alimpa mpira mmoja, akafurahi na kuingia chumbani ambako alifanya shughuli yake mpaka kufikia tamati akauvua mpira na kuutupa sakafuni tena akasikia kinyaa na kujilaumu kwa kitendo alichokifanya kusaliti ndoa yake.
“Ichukue” Akamwambia mwanamke aliyekuwa naye.

“Ichukue wewe” Mwanamke akakataa.
Baadaye wote wawili waliondoka na kuuacha mpira huo sakafuni, sasa wakiwa na akili timamu kondomu haikuwa na umuhimu tena, ilishawasaidia kuwaepusha na Ukimwi basi ilikuwa inatosha, kazi yake ilishakwisha.
Wadogo zangu,

Kwa mfano huu wa Mzee Kijiti naamini mtakuwa mmenielewa vizuri, jiepusheni sana na kutumiwa na watu wenye malengo yao ambao mwisho wa siku yakitimia watawatupa kule kama Kondomu na hawatawajali tena. Mkilijua hili mtafanya mambo mawili, la kwanza ni kuwekeza na la pili ni kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia kufika mlipo kwani kesho ni lazima mtarudi kwao kuwashika mikono, hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kazi.

Jiepusheni na starehe na kulewa umaarufu, jua haliwaki siku zote, kuna mchana na usiku. Muda huu mkiwa juu, ni vizuri kujiuliza giza litakapoingia na mwanga kupotea, au siku tutakapotupwa tutaishi vipi? Anasa hazina mwisho, zipo tu, mlizikuta, mtaziacha na wengine watazikuta na kuziacha hivyo ni vizuri kuwa makini katika kipindi hicho ambacho neema bado ipo, maana mchekaji huwa mchekwaji kesho na mchekeshaji huwa mchekeshwaji kesho kutwa.

Mmekwishanitukana mimi mara nyingi lakini mimi sijali, nimekwishazoea, katika miaka kumi na moja niliyofanya kazi hii ngumu ninao maadui wanaoweza kufanya chochote ili wanichafue, kinachoniuma sana ni kitendo mnachokifanya kwa mzee Mengi ambaye bila yeye TBC1 wasingewaona, kwa umri wake mzee huyu ni sawa na mzazi wenu na mnachokifanya ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sababu tu mmelipwa!

Inawezekana mkawa hamfahamu kwamba umaarufu wenu unapotezwa na kitendo hiki, Watanzania hawapendi watu wenye maringo na kujisifu tabia ambayo hivi sasa imewagubika ninyi mkiwa mwanzo tu mwa safari ya maisha! Mnakumbuka kilichowapata uwanja wa Taifa siku ile mlipopigwa kwa chupa na makopo ya soda? Hilo linapaswa liwe fundisho ili mjiangalie upya, mimi naamini mnaweza kurejesha hali mliyokuwa nayo zamani kwa kujiepusha na matusi kwa watu waliowasaidia.

Mkiendelea na tabia hii si tu mtachukiwa bali mtailetea TBC1 matatizo makubwa sana ya kulipa watu mabilioni ya fedha jambo ambalo najua kabisa TBC1 hawatakuwa tayari kulifanya, hivyo kuamua kujiepusha nanyi! Hata kama TBC1 ni chombo cha serikali, inaelewa kabisa kuna mahakama na hakuna aliye juu ya sheria, kitendo cha wao kuwaruhusu ninyi kuendelea kutukana watu kwa maneno ya uongo, kitakuja kuwaingiza kwenye matatizo makubwa ambayo hatimaye yatavunja ndoa yenu.

Najua maneno yangu yatawaumiza lakini naomba msikasirike kwani tiba ya ugonjwa siku zote inauma lakini mwisho wa siku inaponyesha! Naomba mnivumilie na myafanyie kazi yale mtakayoona yanafaa, binadamu hatujatimia, tunayo mapungufu mengi na kila siku tunafanya kazi kurekebisha sehemu mbalimbali maishani mwetu, nanyi nawasihi mchukue hatua hiyo. Mtu hahitaji kuwa na elimu kubwa sana kuelewa kitakachowapata kama mkiendelea na mtiririko huu mnaokwenda nao.

Sisi sote ni Watanzania tuacheni kuchekana bali tuwatie moyo waliovunjika na tuwasaidie kusimama walioanguka! Matendo hayo ndiyo yatakuwa akiba yetu mara giza litakapoingia hawa mnaowacheka na kuwatukana leo si ajabu ndiyo watakaowasaidia ikitokea siku moja kigogo anayewafadhili sasa akawa hafanyi kazi na ninyi tena jambo ambalo si ajabu kutokea.

Naomba niseme neno moja natumaini sitamuudhi mtu. Watanzania tuna tatizo ambalo ni lazima tulishughulikie kama kweli tunataka kupata mafanikio ya kweli maishani mwetu, tuna tabia ya kuridhika mapema hata kwa mafanikio kidogo. Hapo mlipo wadogo zangu wa Orijino Komedi tayari mmesharidhika, lakini kumbukeni kufika Uingereza au kuendesha ‘Haria’ peke yake haitoshi, kuna mambo mengi sana ya kufanya, kama kufika nje na kuendesha gari ingekuwa kila kitu basi watu wangekwisha acha kufanya kazi.

Hili ni kosa kubwa sana ambalo sisi Watanzania tunalifanya, mafanikio kidogo tu yanatulewesha na kuanza kutukana watu bila kujua kwamba kuna kesho, hata Orijino Komedi mtakubaliana nami katika hili! Wadogo zangu mmelewa sifa mapema, kila mahali mnapoingia mnataka huduma ya VIP? Kumbukeni wanaojikweza hushuswa bali wanaojishusha hukwezwa! Chapeni kazi wadogo zangu, bado hamjafika popote, mafanikio ni safari ndefu mnahitaji sana watu kuliko mnavyohitaji fedha.

Nimeongea mengi sana wadogo zangu, lakini huu ndiyo Waraka wangu kwenu sisi ni ndugu lazima tuelekezane kwa maneno ya ukweli na si visasi, ni vizuri mkakumbuka mlikotoka badala ya kujisikia mmefika mwisho na kuanza kuwatukana watu waliowasaidia kufika juu! Ni vizuri kuelewa hamtakuwa mabingwa siku zote, pengine mtakapokuwa mnaporomoka hawa mnaowatukana leo watakuwa bado wako juu na mtahitaji msaada wao.

Naomba niishie hapo.

Jipu limepasuka siwezi kuwa adui kwa kusema kile ninachoamini ni ukweli. POLE SANA MASHAKA MATONGO, MANENO YA ORIJINO KOMEDI YASIKUVUNJE MOYO, PAMBANA TU HATIMAYE UTAFIKA JUU, YOTE YAWEZEKANA, IF THEY CAN, YOU CAN!

 
Mnakumbuka wosia wa Shigongo kwa vijana hawa?

Shigongo atawapa wosia gani wakati yeye mwenyewe mambo yamampanda.
Mnafiki mkubwa anayejifanya mlokole huku analisha familia yake unafiki na majungu

Ajipe mwenyewe wosia Mkuu Acha hizo
 
Ina mana nyi hamjamshtukia huyu Shigongo?
Siku Orijino Komedi wakisema wanaacha tu kuigiza aseme, "niliwapa wosia hawa vijana lakini hawakunisikiliza"!
Hakuna cha laana ya Mengi wala nini...!bado wapo on line bwana..!Si mnamuona Asha Ngedere siku hizi anavyowa-arest watu...?!
Orijino Komedi bado ipo juu...!
Ni mtazamo wangu tu!
 
Kwa kweli siku hadi siku wanapoteza mwelekeo... Na hiyo ahadi ya kuleta gari mkoani kwako nayo imekaa kisanii... Nadhani wanaelekea kwenye anguko kuu... Ama kweli wahenga walisema NGOMA IKIVUMA SANA MWISHOWE HUPASUKA!!!
 
Shigongo atawapa wosia gani wakati yeye mwenyewe mambo yamampanda.
Mnafiki mkubwa anayejifanya mlokole huku analisha familia yake unafiki na majungu

Ajipe mwenyewe wosia Mkuu Acha hizo
Hii nini ? wivu au ? sijaona nini cha kustahili kuitwa unafika kwenye waraka wenye hoja murua kama wa Shigongo kwa watu wote kwa ujumla na orijino komedi kipekee,ni vema kama una hoja na Shingongo itoe tuione kuliko kupinga nata kizuri ilimradi kimetolewa na Shigongo.
Ni vema kuwasaidia hawa vijana mapema kuliko kusubiri uje uwacheke tuwe na upendo na tutumie busara zetu kuwasaidia wengine,kuwasifu kwa upotofu wao ni ujinga sana na hatutawasaidia...bahati mbaya sana hawa vijana wanaishi kwa msaada wa "goodwill"ya komed ya EATV lakini kisannii wamefulia kama wenyewe wanavyoona wengine wamefulia kimaisha.
 
unasema tu mzee. unafikiri kazi ya kuwachekesha watu ndi ndogo kiivyo? si sawa na kukaa dukani kusubiri wateja, kaka. wape tano zao na uwaombee makubwa tu
 
Wandugu kwa mtazamo wangu naona hawa vijana tangu waondoke pale EATV kama wamepote kabisa katika anga la vichekesho je ikoje hiyo wa JF

sasa JP hapa unataka tuwacheke au tuwape support?

mimi naona wapo juu sana na wanafanya vitu vyao kwa makini zaidi hata kuringanisha na FUTUHI (ambao kuna wakati wanaudhi kwa kurefusha jambo bila sababu hivyo kupoteza muda)

lakini kila msanii bongo anahitaji support zaidi na sio kuchekwa kama tunavyofanya sasa hivi haya ni mambo ya vijijini na yanarudisha sana maendeleo. LET'S SUPPORT ONE ANOTHER AND MOVE FORWARD
 
Back
Top Bottom