Opposition MPs to lead key Bunge committees: Lowassa in; is this a positive move?

Mh. Lowassa, Mh. Lowassa, mzee wa watu, mzazi wa watu, baba wa watu... nakusihi nakusihi nakusihi - ng'atuka katika siasa. Vilio vya Watanzania na majonzi yao ni mengi baba. Wasikilize na kufanya jambo la busara kwa kuondoka katika siasa. Kumbuka Mwenyezi Mungu husikia vilio vya wengi na nina imani wewe ni mcha Mungu. Hivyo utafanya jambo la maana sana kama hutojiingiza katika siasa tena. Ahsante.
 
Kwanza naomba kujua, nguvu ya Mwenyekiti wa hizo Kamati ni kubwa kiasi gani na wigo wa kutumia hiyo nguvu yake ni mpana kiasi gani? Baada ya kujua hayo ndipo tunaweza kujadili kwa mapana na marefu.

Lakini hata hivyo, kwa Bunge ambalo liko dominated na chama kimoja hata Mwenyekiti awe na nguvu kiasi gani bado kunaweza kuwa na matatizo kwenye kupitisha hoja nzito na hasa kama wabunge wa chama tawala hawataki hoja hiyo ipite. Mwenyekiti anaweza kujikuta yeye na wajumbe 10 tu wanataka hoja ipite wakati wajumbe wengine 70 wanasema NO. Kwenye mazingira kama hayo bado kuna ugumu wa kutosha.

Kanuni kama hiyo ni nzuri na inasaidia sana kama Bunge liko balanced kwenye idadi ya wabunge na kwenye kamati. Bunge lililopita la Kenya, kuna baadhi ya mambo serikali ilikuwa inagoma yasifanyike lakini Kamati zilikuwa zinalazimisha kwa kuwa wapinzani walikuwa na numbers kwenye hizo kamati. Sasa kamati za Bunge la Tanzania wapinzani ni wachache sana na hivyo wanakosa sauti/nguvu ya kulazimisha jambo lifanyike. Maana demokrasia inasema hoja ikiwa moto kura ipigwe ili uamuzi ufanyike, na kama mchuano ukiwa droo ndipo Mwenyekiti anatumia "busara" ama kura yake ya turufu. Kura ya turufu haina nguvu kwa upande wa upinzani kwenye Bunge la Tanzania kwa kuwa idadi ya wapinzani ni ndogo.

Ukombozi wa kweli kwa watanzania utakuja kwa kuongeza kwanza idadi ya wabunge kutoka upinzani na hilo ndiyo litapandisha joto la kudai katiba mpya na hatimaye tutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, madaraka ya rais yatapungua na mambo mengine mengi mabaya yaliyo kwenye katiba yatafanyiwa marekebisho kwa maslahi ya watanzania na siyo kwa maslahi ya serikali iliyo madarakani.


Faida kwenye hili ni kwamba kama watakataa ina mana Mjumbe ama mtu wa Upinzani kama kawaida maneno Jagwani na mambo hadharani tunaanzia hapo .Wakiwa nje kabisa kunakuwa na siri kubwa .Ila Bunge na wabunge sasa wanajua kwamba Dunia ni ndogo na hakuna siri tena .So wacha waende huko tuone tusilalame kabla hawajaanza kazi .
 
Mh. Lowassa, Mh. Lowassa, mzee wa watu, mzazi wa watu, baba wa watu... nakusihi nakusihi nakusihi - ng'atuka katika siasa. Vilio vya Watanzania na majonzi yao ni mengi baba. Wasikilize na kufanya jambo la busara kwa kuondoka katika siasa. Kumbuka Mwenyezi Mungu husikia vilio vya wengi na nina imani wewe ni mcha Mungu. Hivyo utafanya jambo la maana sana kama hutojiingiza katika siasa tena. Ahsante.

Huyu Lowasa inabidi apewe one on one na yule mtoto wa mwanza aliyempiga bonge la swali na mwamuzi wa hiyo mechi awe ni our own Mwanakijiji akisaidiwa na washika vibendera bibi senti na mchambuzi the great quiter moran ... papa propaganda!
 
Back
Top Bottom