Operation ya MGUU inakataa kufunga tatizo ni nini!!!!

Angeloos

Member
Jul 18, 2011
56
19
Mama yangu alikuwa na maumivu makali kwenye goti, alivyokwenda hospitali MOI aliambiwa kuwa fluid ambayo huwa inakuwepo kwenye goti ili kuzuia msuguano wa mifupa imekwisha, hivyo solution pekee ni kufanyiwa operation ambayo atawekewa vipandikizi ili kuondoa tatizo lake.

Mwaka 2010 alifanyiwa operation ya goti la mguu wa kushoto pale MOI. Kidonda kilipona lakini kukabakia kitundu kidogo kwenye mguu ambacho kilikataa kufunga na kikawa kinaendelea kutoa uchafu. Daktari aliyemfanyia operation akasema anairudia kwa madai kuwa vipandikizi alivyomuwekea kwenye mguu havipatani na mwili wa mama yangu.


Mwaka jana 2011 alifanyiwa operation tena kwa mara ya pili na kubadilishiwa vipandikizi, lakini tatizo limeendelea palepale, kunakuwa na kitundu ambacho kinakataa kufunga mbaya zaidi walimuwekea vyuma ndani sasa vile vyuma vimekuja juu vinaonekana.

Leo ilikuwa ni siku yake ya kwenda kumuona daktari wake, alivyomuonesha vile vyuma akamwambia kuwa anatakiwa afanyiwe tena operation ili kuviondoa kwamba eti vimekataa. Sasa nimepatwa na wasiwasi naona kama vile daktari anabahatisha, sielewi tatizo ni nini. Mama yangu ni mtu mzima sana kufanyiwa operation mara zote hizo naona anateseka.


Sasa nimekuja huku jamvini, naomba kama kuna mtu anamfahamu daktari bingwa wa mifupa au mwenye ushauri wa aina yoyote kuhusu tatizo hili please please please help me. Nahitaji msahada wa haraka tafadhali.
 
Pole sana. Sidhani kama kwa hapa TZ kuna hospitali yenye uwezo wa mifupa kama MOI. Ongea na daktari kwa kirefu aelewe worries na concern zako. Yaani uwe kama mjadala fulani, muulize in a friendly manner kuwa vpandikizi vya kwanza vimekataa, vya pili vimekataa, je hivyo vya tatu vitafanikiwa! omba kama kuna any other alternative nadhani utafanikiwa. Unajua katika operesheni kama hizo huwa si vizuri kubadirishabadirisha madr.
Pia ujue kuwa madr. kuna wakati huwa hawapendi kumweleza mgonjwa ukweli; yawezekana mama ana tatizo kubwa zaidi; ni mpaka umuulize kwelikweli. Take time to discuss.
Mwamini dr wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom