Open Letter to His Exclence JMK-Is it a Carrot and Stick Land Deal?

...Kumbe wao wanajua kutunza rasilimali zao kwa ajili ya Vizazi vyao vijavyo eh? kwa nini na sisi tusiwaambie hizo ekari zetu 500,000 hatuwezi kuwapa kwa sababu ni kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo?????

TOfauti ni kuwa wao hawajaomba kwa Fao wala Food Programme na kuepusha kuzidi kuomba chakula kwa Japan ndio JK alipoona bora ubia katika kuzalisha.
Kama tunaweza kufa kwa njaa kuliko kuitowa sehemu ya ardhi kwa ajili ya kilimo kitachotusaidia nasi basi na tuiweke hiyo ardhi na kungoja hao watoto watakaokufa kwa njaa wafufuke na kuja itumia hiyo ardhi.
 
...Nakubaliana nawewe kwa kiasi kikubwa. Tatizo kama wanavyoongelea wenzangu ni urefu wa mkataba na kiasi bei iliyotolewa. Kama ni miaka 99 kama wengi wanavyosuggest... hii ni noma. Kwao na sisi.

...Ipo siku yaja ndani ya miaka 99 mambo ya ardhi yaliyoikumba Zimbabwe yatatufika nasi. Hasira kutoka kwa wananchi au mmoja wa viongozi. Mambo ya kuuza ardhi yakiwa hivi, itatokea siku 'kichaa' mmoja anauza eneo walilomo na maeneo yanayozunguka eneo hilo kwa miaka mingine 99!!

...Kiongozi wa awamu hii akiuza kata, awamu ijayo atauza tarafa, anayefatia atauza wilaya..... mwingine eneo loooooooote wanaouziwa hawa wakezaji hivi sasa na mkoa wote!!

Ardhi haitouzwa bali kutakuwa na mradi wa Ubia na kinachotakiwa hapo ni kuwa tujaribu kuwa na hisa nyingi iwezekanavyo kama kweli tunaweza na hiyo itatufanya share yetu tuwauzie wao iwapo yao haiwatoshi. Haya ni kupangwa na sio kukataa kabisa huo mradi.
 
Ngekewa,
Well tuna ardhi hatuitumii kutunufaisha kutokana na sababu nyingi ikiwa uvivu ni kubwa yao. Sasa wanakuja watu kuzalisha na kutuachia sehemu yetu ubaya uko wapi? Sisi si wageni na hawa wawekezaji lakini ukweli ni kuwa hatuwezi kuwaepuka kutokana na uvivu wetu. Ni wazuri kukaa mijini kuendeleza Usanii na kuwaacha walio wengi wakiumia kwa kilimo cha jihadi na njaa. Kazi yetu kuuza maneno lakini walio vijijini hufurahia uwekezaji pale unapofanywa kwa uadilifu. Hivyo hivyo mradi huu kama tutakuwa waangalifu utaweza kuleta manufaa makubwa kwetu.
Mimi nadhani kinachotupa shida ni ile miaka 99, wakati kisheria nadhani hati za kumiliki ardhi (lease) kulingana na sheria za sasa hivi huwa zinakupa miaka 99 (Kama sikosei)...na sidhani kama kuna tofauti kati ya mwananchi mzawa na mgeni tena basi naweza sema mgeni ananufaika zaidi kwa taratibu zilizojengwa kumvuta.
Binafsi sitakuwa na tatizo kabisa na Waarabu au Wazungu kuja nchini kuwekesha ikiwa mtazamo wangu kisiasa ni Progressive... Na ndicho wanachokiona Kikwete na CCM kwa sababu ni kundi la watu wanaojiita Progressive ndani ya CCM..
Hivyo mara nyingi mimi napopinga hoja za namna hii hua sitazami mhusika isipokuwa siasa zinazoendana na mpango uliopo. Chini ya mfumo wa hawa jamaa zetu sisi Watanzania wote ni wapangaji tu..hatuna mamlaka ya kumiliki ardhi hivyo kila kinachotokea leo hii ni kutokanma mna mfumo mbaya wa umiliki wa ardhi unaotokana na siasa mbaya za hao wanajiita Progressive.
Mimi as Conservative -Naamnini kabisa kwamba ardhi ni mali ya wananchi na ndio sababu kubwa iliyotusukuma kupigania Uhuru wetu hivyo wageni wanapokuja nchini ni dhahiri hata kama ku lease ardhi ni lazima iwe kwa faida ya wananchi wenyewe na sio kufikiria NJAA iwe sababu ya kutoa ardhi.
Huwezi kumwoza mwanao kwa sababu una njaa, au mume ni tajiri, vibaka wa mtaani wameshindwa kupanda dau, haya ndio yaliyompata baba wa yule mtoto wa kike ktk sinema ya 'Slumdog Millionea'.
Tuache fikra za NJAA..Wazee wetu wa Kariakoo wangefikira njaa wakati ule wa miaka ya 80 wasingeweza leo kuuza nyumba zao kwa dollar 800,000 isipokuwa thamanai ya nyumba hizo ilizidi kupanda ikiwa mikononi mwao..Just 1995 ilikuwa 20,000 na nyuma ya hapo with 10,000 uliweza kununua nyumba Msimbazi na Sikukuu..

Kesho ardhi hii ya kilimo tunayotaka kumpa mwarabu au hata wazungu waliokwsiha chukua watavuna mara kumi na wakisha watauza kwa faida mara 10 wakati mwananchi bado maskini..Njaa ya leo isiwe sababu kabisa ya kuuza nchi kwani binadamu hula mara tatu kwa siku, kushiba kwa mara moja haina maana njaa hiyo haitarudi na kesho ukishikwa njaa tena mwarabu atadai ardhi zaidi ili upate kipande cha mkate.
Ndivyo Wayahudi walivyoweza kuichukua sehemu kubwa ya miji ya Palestine..
 
Tatizo letu hapa ni kuamini kitu at face value. Maadam mtu ataamuwakuleta pumba yoyote ile maadam inakandia Serikali au JK basi tutayasema yote.
Hivyo katika akili zetu unatupitikia kuwa watu wa pande zote mbili watakuwa wapumbavu wa kuingia mikataba kichwa kichwa? Kwa upande wetu tutajaribu kulinda ardhi yetu na kwa upande wa wenzetu watajaribu kulinda fedha zao. Hili suala la kusainiwa mikataba bila ya kufanya utafiti kwa kila upande linawangia akilini? Ndio tunaingia mikataba mibovu lakini tunafanya hivyo baada ya kupitia taratibu zilizowekwa ingawa tunazipindisha hapa na pale mara nyingi.
Sasa hili la kikwete kutia saini mkataba linatoka wapi? Jee mkataba huo aliusaini nani kwa niaba yake au alisaini mwenyewe. Kikawaida wakuu wa nchi hufunguwa milango ya majadiliano juu ya masuala mbalimbali na siamini kuwa JK alipokwenda huko alikuwa anajuwa kuwa Vilemba wanataka ardhi,kwani angejua angemchukuwa waziri wa Kilimo.

Kilichojiri huko bila shaka itakuwa ni scratch my back and I will scratch yours.Tunaweza vkushangaa kuwa pengine JK aliomba mengi kwa niaba ya Watanzania kwani kwa Vilemba kama kiongozi unataka kwa binafsi yako cha kufanya ni kumsifu Mfalme tu na utapewa zako. Ukiona suala la miradi linazungumzwa na Waarabu basi aliyezungumza alizungumza kwa niaba ya nchi.
Hatuwa inayofuata sasa ni kwa Waarau kuleta Wataalamu kustudy huo mradi wa ubia na kwa upande wa Tanzania tutawajibika kufuata taratibu zetu zinazohusiana na masuala kama haya.

Ngekewa with due respect,

Matendo yanaonyesha hivyo. Mtu aliyeumwa na nyoka hata unyasi ukimbia. Tizama kuanzia madudu ya ununuzi wa Rada, Richmond, IPTL et al. Kwa hiyo suala la kusema tunatimu imara hilo futa hata ( majority of them dont have morals to be our representative kwa sababu ya siasa za kujaza matumbo)hata huyo JMK alishanyanyua mikono.

Past experience zinatupa sababu ya kutokuwa na imani na utendaji wa serikali hasa linapokuja suala linalogusa jamii kama hili la ardhi. Muda wa kukaa na kuimba nyimbo za kuipongeza serikali zimepitwa na wakati. We have employed them for 5 years and they have a duty to deliver na kama wanakuja na mambo yenye utata lazima tukemee.

We have casted doubts on the all 'deal', the duty now is on the government to persued us that it is a just and reasonable deal. Kumbuka tumeijiri hii serikali na si serikali imetuajiri. They are responsible kwa wananchi!

Mwisho tunahitaji sera za ardhi zinazomlinda na kumwezesha mzawa. Nafikiri Mkandara ametoa wazo zuri sana kuhusiana na uwekezaji wa kwenye Ardhi.

Mheshimiwa Ngekewa, kumbuka kukubali kukubaliana katika kutokukubaliana kwa hiyo njoo na sababu za kuikumbatia serikali hili tuzichambue na si kukimbilia kutoa hitimisho la ajabu ajabu.

For God and My Country,

Shadow.
 
Last edited:
It is tru, bongo is pure kiinimacho. Mi niliambiwa na mzazi wangu, nisiamini chochote ninachoambiwa na amini nusu ninachoshuhudia kwa macho yangu, kwa kumaanisha dont take kila kitu at face value. Bwana, idea ya kuuza mbogamboga na mazao mengineyo nje ya nchi ni "kitu visionary sana", na manufaa kwa taifa letu ni limitless.lakini mi nahofu utekelezaji wa huu mpango na matokeo yake. Haya maeneo hawa waarabu watakodisha yatageuka kuwa kambi za jeshi, na ole wake mswahili akamatwe anachuma mapera bila ruksa. Hivi kuna mtu kashawahi kujiuliza kwanini mwekezaji lazima aje toka nje? ebwanaee, sikiliza, ulaya ni watu wachache mno wanamiliki mali zao, kwa mfano watu wengi wananunua nyumba kwa kupata mkopo wa miaka 25-30 toka benki, soo ni pale zungu linapoachishwa kazi, halafu linashindwa malipo ya kila mwezi ya; nyumba about $1000, shangingi $450, luninga 60 inch $150, nk. Kwani bongo hakuna watu wenye hela? tatizo lipo pale wapi pakuwekeza mali. Mi kila siku nawaambia watu wasiofahamu the real situation kwamba nembo kwenye bidhaa inasema made in china lakini inatakiwa kusema produced in Afrika. Mimi binafsi naamini kwamba Watanzania ni "too passive", ukiangalia mfano wa Msumbiji, wareno walishindwa. Hata Kenya, wenzetu walikuwa mapanga shwaa, waingereza wakakipa kitu. Ndugu JK'ers, naomba mnielewe kwamba i dont advocate violence, lakini sipendi upuuzi. Kwa kweli Watanzania tukijituma, na viongozi wetu wakiwajibika, TZ inaweza kuwa kama South Afrika, if not better.
 
NImetembelea thread hii kujaribu kusoma comments mbalimbali lakini naona kuwa kuna ishu moja muhimu inayorudiwa:
- kutokuwa na imani na serikali ya CCM na uongozi wa JK kutekeleza vyema mradi huu.
Nadhani arguments zote against mradi huu unaweza kushindwa na hoja za kisheria, logical or practical calculations of cost-benefit etc. Hivyo mara nyingi oppoistion to this project appears to be based solely on emotions like patriotism, nationalism etc.
Lakini nadhani Shadow ndo ame-summarize vizuri kwamba all arguments are theoretical tukiangalia in the past for precedent tunaona madudu tu, showing that the CCM governemnt is not able to handle any project transparently and for the benefit of the nation.
So like many others, I support this project in theory but I oppose it practically kwa sababu ya kukosa imani na serikali ya CCM ambayo imefanya kazi mbovu katika sekta hii na zingine zihusuzo matumizi ya ardhi ya watanzania.
 
Ndugu yangu hii nadhani ni oversimplification! Tuliangalie jambo hili kwa mapana zaidi huku tukizingatia kuwa huko tuendako dunia itakuwa na upungufu mkubwa wa vitu viwili muhimu chakula na maji,looks like wenzetu wanaona mbali maana si wasaudi tu hata wakorea wanatafuta ardhi afrika kwa ari mpya na kasi mpya.Hili ni suala nyeti na pana na la kufuatilia kwa makini.
Lakini tusije kuwapa ardhi kubwa yoote hiyo. Maana kama Kikwete kagawa ardhi kubwa namna hiyo je sisi wengine ndio tutalima wapi? yaani ikifika wakati wetu na watoto wetu je? Na Miaka 99, ni mingi sana kwa kweli, kama viongozi wetu wanaona kwamba wenyewe hawawezi kuendeleza ardhi mpaka waikodishe kwa watu sio lazima wafikiri na sisi hatutaweza kuishughulikia kama wao! Na watoto wetu wanaweza kuiendeleza piaa, kwa hiyo sio watoe ardi kubwa namna na kwa miaka mingi.
 
Mkuu Bishanga,

Kwa nini tusilime wenyewe na kuwauzia chakula? Je, Inaingia akilini kweli kwamba wanataka kulima kwa ajili ya kulisha wananchi wao? Sound to be a shady deal, mzee. Kumbuka kwamba sasa hivi teknolojia pia inabadilika mafuta ya ethanol nayo yanaanza kuchukua mkondo. Hawa jamaa wanaangalia mbali zaidi . Miaka 99 hata 33 si mchezo kwa mwekezaji. Tunaongelea mpaka vizaizi 3.

I will sticky to my position. This deal sound to be shady period.

Asante kwa ukweli. Na la kuongeza ni kwamba je kama na sisi tunataka kupata visima vya mafuta huko kwao uarabuni ili tuchimbe mafuta kwa ajili ya matumizi yetu hapa Tanzania watatukubalia hawa waarabu?. Sisi hatujashindwa kuwekeza katika kilimo bali tuna uhaba wa vifaa. Kwanini tusinunue vifaa vya kisasa vya kilimo na kufanya kilimo cha kisasa?. Kilimo ni utii wa mgongo kwa Tanzania, sasa kama tutauza ama kukodisha uti wetu wa mgongo ama muhimili wetu tutabaki na nini cha kutegemea?. Tumeuza mashirika ya umma na makampuni, waliokuwa wafanyakazi wengi wameachishwa kazi tokana na zoezi hilo la kuuza mashirika na makampuni na sasa wamekimbilia kulima na kufuga ili wapate riziki, sasa kama na huko pia wataingiliwa tunataka hawa watu wakimbilia wapi?, je tunataka kuwafanya watanzania wawe watumwa katika nchi yao kwa mtindo wa utumwa mambo leo?.

Tunahitaji uchambuzi wa kina katika hili na kuwa makini huku tukizingatia kwamba kuna vizazi vijavyo katika Tanzania. Wajukuu zetu wasije kufukua makaburi yetu na kutaka kuyafanyia uchunguzi mafuvu yetu kutaka kujua kwanini tulikuwa wapumbavu na wavivu wa kufikiri.
 
Asante kwa bandiko hili. Waswahili tunafahamu kirahisi sana kupitia mifano. I like the challenge na tutafakari vizuri. Kwanza jee waarabu watakubali kutukodisha visima ili tuchimbue mafuta - tufue umeme na kutumia kule Pemba kwa haja zetu na kunufaisha watoto wetu?
 
the maths behind the deal.....

kenya 40,000 hectares = wamepewa port yengye thamani tsh 3 trillion = $2 billion

je TZ itakuwaje
500, 000 / 40,000 = 12 and 20,000 hectares free

$2 billion x 12 = $24 billion or tsh 3 trillion x 12= 36 trillion
the govt will be selling us short if the get anything less than $24 billion or tsh 36 trillion

current budget tsh 7 trillion
4 yrs budget= 4 x 7 trillion = 28 trillion
36 trillion - 28 trillion = 8 trillion
kutokana na uchumi kukua 8 trillion itakuwa itajazilia mapungufu ya budget

TZ hectares 500, 000 = $24 billion = tsh 36 trillion

maswali ambayo yanahitaji majibu??
1.would TZ govt get $24 billion from saudis?
2.do you trust this govt to sign such a deal?
3.Je hela zitakazopatikana zitaisaidi hii nchi au zitaishia mifukoni mwa viongozi?
4. kwa nini hawa jamaa walienda serikalini moja kwa moja kwa mkulu bila kupitia TIC, hata mkurugenzi wa TIC hakuwepo na walikuwepo watu kama waziri wa mambo ya ndani(masha)?
5. long term deal in bussiness is 20 -25 yrs, sheria za ardhi bongo za miaka 33, 66, au 99. je miaka 33 haitoshi kurudisha hela yao?
6. je miaka 66 haitoshi kurudisha hela yao?
7. je miaka 99 ni kidogo au mingi?
8. kuna mtu yeyote anaejua nchi ime sign deal ya ardhi kwa ukubwa wa kuanzia hecta 100, 000 kwa zaidi ya miaka 33 au dili ambayo inakaribiana na hii tunaomba utufahamishe...
9.je tz ina hecta ngapi zenye rutuba ambazo sio jangwa?
10. je tukiwapa hecta 500, 000 zenye rutuba watanzania watabakiwa na hecta ngapi zenye rutuba?
11. je baada ya miaka 33 TZ kutakuwa na watu wangapi? je baada ya miaka 66 tutakuwa wangapi? sidhani kama tunaweza kutabiri tutakuwa wangapi baada ya miaka 99 kwa hiyo siulizi hili...

hill deal sio lenyewe kabisa, hapa watanzania tunaingizwa chaka kama kawaida yetu. Haya ndio yatakuwa kama yale ya LOLIONDO...
 
Hili dili sio lenyewe kabisa, hapa watanzania tunaingizwa chaka kama kawaida yetu. Haya ndio mambo kama ya LOLIONDO...
 
TOfauti ni kuwa wao hawajaomba kwa Fao wala Food Programme na kuepusha kuzidi kuomba chakula kwa Japan ndio JK alipoona bora ubia katika kuzalisha.
Kama tunaweza kufa kwa njaa kuliko kuitowa sehemu ya ardhi kwa ajili ya kilimo kitachotusaidia nasi basi na tuiweke hiyo ardhi na kungoja hao watoto watakaokufa kwa njaa wafufuke na kuja itumia hiyo ardhi.

...Unajuaje kama kitatusaidia? Si hata madini tuliambiwa tuwaite wawekezaji waje wachimbe halafu tugawane? matokeo yake? Na kwa nini tufe kwa njaa kumbe kuna ardhi ambayo waheshimiwa wetu wanataka kuikodisha kwa watu? Si ndio haya ya kutafuta majibu mepesi kwa maswali magumu ya maisha? Ameuliza Mchangiaji mmoja; Kwa nini basi tusilime wenyewe halafu tukawauzia hicho chakula?? kinachotushinda ni nini? Kwa nini tuone kukodisha ardhi yetu kwa miaka 99 ndio suluhisho pekee??
 
Asante kwa ukweli. Na la kuongeza ni kwamba je kama na sisi tunataka kupata visima vya mafuta huko kwao uarabuni ili tuchimbe mafuta kwa ajili ya matumizi yetu hapa Tanzania watatukubalia hawa waarabu?. Sisi hatujashindwa kuwekeza katika kilimo bali tuna uhaba wa vifaa. Kwanini tusinunue vifaa vya kisasa vya kilimo na kufanya kilimo cha kisasa?. Kilimo ni utii wa mgongo kwa Tanzania, sasa kama tutauza ama kukodisha uti wetu wa mgongo ama muhimili wetu tutabaki na nini cha kutegemea?. Tumeuza mashirika ya umma na makampuni, waliokuwa wafanyakazi wengi wameachishwa kazi tokana na zoezi hilo la kuuza mashirika na makampuni na sasa wamekimbilia kulima na kufuga ili wapate riziki, sasa kama na huko pia wataingiliwa tunataka hawa watu wakimbilia wapi?, je tunataka kuwafanya watanzania wawe watumwa katika nchi yao kwa mtindo wa utumwa mambo leo?.

Tunahitaji uchambuzi wa kina katika hili na kuwa makini huku tukizingatia kwamba kuna vizazi vijavyo katika Tanzania. Wajukuu zetu wasije kufukua makaburi yetu na kutaka kuyafanyia uchunguzi mafuvu yetu kutaka kujua kwanini tulikuwa wapumbavu na wavivu wa kufikiri.

...Nimependa mno bandiko lako Mkuu! Mimi nadhani kesi inapaswa kuwa ni kwa nini sisi wenyewe hatuwezi kuzilima hizo eka 500,000 na kuwauzia hawa waheshimiwa chakula na sio wapewe ama wasipewe!!!
 
...Nimependa mno bandiko lako Mkuu! Mimi nadhani kesi inapaswa kuwa ni kwa nini sisi wenyewe hatuwezi kuzilima hizo eka 500,000 na kuwauzia hawa waheshimiwa chakula na sio wapewe ama wasipewe!!!

Hapo ndipo ninaposema kwamba sisi ni wavivu wa kufikiria. Hatuna sababu ya kuuza ama kukodisha ardhi kwa wageni. Tulime chakula na tuwauzie kama wao wanavyochimba mafuta na kutuuzia. Na tungefanya hivyo hata kwa madini tuliyokuwa nayo. Inasikitisha sana kila kitu kinauzwa.
 
sijasoma maoni ya wengi humu, lakini ningependa ku-suggest kwamba kwanini sisi wenyewe tusilime na kuwauzia hizo products iwe vegitables, etc badala ya kuwapa hiyo ardhi ili wao walime? hata kama tutamwajiri Msaudi moja kama Project Manager, atueleze hizo product zao wanataka ziweje? Packaging etc etc, hata hao ndugu zetu wa kenya, Rwanda Burundi, wakitaka kuwekeza Tz, msimamo uwe wa ardhi ni Yetu, labda tushirikiane kwenye Management, Project Manager Wao, Finance Officer Wetu, tusije kuibiwa bila kujua
 
Kweli maswala yote ya uwekezaji nchi hii yanahitaji yaangaliwe kwa makini sana. Maana tumeshaumizwa sana sisi Watanzania.
Tatizo ni kuwa TIC ni Bomu haswa kutokana na uongozi usioeleweka. Sielewi kwa nini hili haliangaliwi kwanza kabla ya yote.Pili Investment policy ya nchi yoyote kama policy nyingine zozote ni lazima ziwe dictated from within the respective country siyo kila mwekezaji aje na sera yake hapa!
Kwa hiyo sisi ndio tungepaswa kuainisha spatial development/investment strategy ya nchi yetu yaani wapi tunataka kuwekeza nini; hasa Kilimo cha umwagiliaji, na mipango mingine ndio tuamue tunawakaribisha wawekezaji kwa masharti gani kwa muda gani na kwa maslahi yapi ama incenctive zipi kwa yale maeneo yenye changamoto.

Hawa wakubwa wetu wanaotembea nchi za wenzao kila siku haswa huko Uarabuni wameona wenyewe waarabu wanavyosimamia uwekezaji na maendeleo ya nchi zao. Ulizeni Malaysia investment policy yake ikoje. Wao ndio wanaopanga investor gani aende wapi na kwa masharti yepi na incentives zipi. Ulaji umezidi. hebu tuamke tuanze kuipenda nchi yetu hata kidogo jamani.
 
Back
Top Bottom