Only in Tanzana, kama huna pesa tupishe!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Kisa cha kwanza…

Nafika bucha na kuagiza kilo mbili za nyama kawaida. Kwa kuwa najua bei, natoa chenji kamili na kumkabidhi muuza bucha.

Anahesabu na kuniuliza mbona hela haitoshi? Napigwaa butwaa na kumuuliza kwani kulikoni? Ananijibu bei imepanda.

Naanza kulalama na ghafla nyuma yangu nasikia sauti, “Ee bwana kama huna hela tupishe, unatuchelewesha!

Sijakaa sawa sauti ya kike nayo ikadakia, “Wengine bwana, wapuuzi kweli kweli! Mtu huna hela kwani lazima ule nyama?

Taratibu nageuka na kukuta mstari nyuma yangu. Wote wamefura wakinitazama kama vile natoka sayari ya mbali.

Hakuna sura hata moja iliyoonekana kuniunga mkono au hata kushangaa kwa nini bei imepanda karibu mara mbili!

Kisa cha pili...


Nikapokea simu ya mkono kutoka ng’ambo, simu ambayo kwa makusudi kabisa ya kibiashara inaitwa simu janja (TZ!)

Baada ya kuipokea mara moja nikaanza utafiti wa kampuni gani ya simu itanifaa kwa matumizi yangu na kwa gharama nafuu zaidi.

Laiti ningejua kuwa ipo mamlaka inayohakikisha inaua ushindani katika biashara ya simu nchini ili wao wanufaike, wala nisingehangaika.

Nikapiga hodi kampuni moja ya simu inayosajili na kuunganisha simu. Huko nikakuta ziko bando za siku moja, za wiki na za mwezi!

Basi ngoja kizaa zaa kianze. Nikauliza vipi nikinunua kifurushi cha wiki halafu nisikitumie au nikatumia bila kukimaliza katika wiki hiyo?

Haraka haraka akanijibu mhudumu, “ndio imepotea hiyo na itabidi ununue kingine.” Sikuamini masikio yangu nikabaki tu nimeduwaa!

Mwenzake mhudumu (wanakaa wawili wawili) akaingilia kati kunielewesha, “unaweza kununua cha siku moja kama matumizi yako ni kidogo.”

Kwa mshangao nikauliza je vipi kama nimetumia tu nusu, hiyo nusu nyingine mnaipeleka wapi. Ghafla sura zote mle ndani zikabadilika.

Bia kujali nikaongezea nikauliza tena kwa mshangao, kama hamrudishi hela hiyo bando yangu iliyosalia kwa nini isiwe carried forward?

Nyuma yangu sauti ikasikika, “Huyu mzee kachanganyikiwa nini! Hebu tupishe kama huna hela…wazee wengine bwana."

"Simu yenyewe labda katumiwa na kijana wake, huyo kijana wake atakuwa naye wa hovyo tu, hatumi hata hela ya kutosha ya bando!"

Taratibu nikajiondokea kuelekea kampuni nyingine iliyokuwa mtaa wa pili bila kujua huko mtaa wa pili nitakutana na nini...

KIsa cha pili kinaendelea...

Baada ya kukata kona mpaka mtaa wa pili nikakuta mambo ni yale yale hivyo nikawa sina tena namna .

Mwaka jana mwezi wa sita bei ya kifurushi cha pure data kwa kampuni zote zinazotoa huduma za internet kilikuwa kama ifuatavyo;
  1. GB 10...Tsh. 10,000/= (sawa na shilingi 1,000 kwa kila GB moja)
  2. GB 19...Tsh. 20,000/= (sawa na shilingi 1,050 kwa kila GB moja)
Nikanunua cha Tsh. 20,000/=, Katikati ya mwezi wa nane Gb zangu zikaisha na ikabidi nisasishe upya kupitia mtandaoni...

Cha ajabu nikakuta bando za pure data kwa kampuni zile zile zikitoa huduma zile zile bei zake zimepanda kama ifuatavyo;
  1. Tsh. 10,000/= inanipa GB 4.5 tu! (sawa na shilingi 2,200 kwa kila GB moja)
  2. Tsh. 20,000/= inanipa GB 9.5 tu! (sawa na shilingi 2,105 kwa kila GB moja)
Ilikuwa kama vile nimepigwa radi nilipokuta bei zimeongezeka zaidi ya mara mbili!

Kesho yake asubuhi nikafunga safari hadi ofisini na kuwakuta wahudumu wamekaa wawili wawili kama ilivyo kawaida yao.

Nikaunga foleni ndogo nilioikuta nikisubiri zamu yangu ifike niulize tu katika miezi miwili kumetokea nini hadi bei iongezeke kihivyo.

Zamu yangu ikafika...ninachokumbuka kusikia ni zile sauti za kikejeli...za kunitaka nifanye haraka, za kama pesa yangu haitoshi, za tupishe.

Kwa safari ya tatu sikupata support...si kutoka kwa wahudumu wala wateja!
 
Mzee Mag3 hii ni story tu. Tokea lini bucha kukawa na foleni kama vile nyama ni kitu adimu wakati zinaozea buchani?

Wateja hawawezi kukushambulia kwa maneno sababu wanasubiri wahudumiwe. Never. Labda ulikuwa mbishi wakakuona unazingua.

Lakini siyo sababu hujui bei ya nyama na huna buku 2 kufidia bei mpya. Huu ni uwongo mkuu.
 
Chief huku ulipoleta hii habari ni hovyo kuliko huko ulikokuwa. Kama huamini soma mawazo ya wachangiaji.

Hili ni taifa la wajinga. Watu ambao wanaweza hata kunyanyaswa tu na kondakta wa daladala.

Hapa kwetu unaweza kupandisha bei ya bidhaaa yoyote utakavyo na bado hao masikini wakakushangilia.

Wala usipoteze muda wako kuwatetea masikini, jitetee wewe na familia yako.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Kisa cha kwanza…

Nafika bucha na kuagiza kilo mbili za nyama kawaida. Kwa kuwa najua bei, natoa chenji kamili na kumkabidhi muuza bucha.

Anahesabu na kuniuliza mbona hela haitoshi? Napigwaa butwaa na kumuuliza kwani kulikoni? Ananijibu bei imepanda.

Naanza kulalama na ghafla nyuma yangu nasikia sauti, “Ee bwana kama huna hela tupishe, unatuchelewesha!

Sijakaa sawa sauti ya kike nayo ikadakia, “Wengine bwana, wapuuzi kweli kweli! Mtu huna hela kwani lazima ule nyama?

Taratibu nageuka na kukuta mstari nyuma yangu. Wote wamefura wakinitazama kama vile natoka sayari ya mbali.

Hakuna sura hata moja iliyoonekana kuniunga mkono au hata kushangaa kwa nini bei imepanda karibu mara mbili!
Tafuta hela
 
Back
Top Bottom