Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
- Thread starter
- #21
Mwafrika wa Kike:
Kikwete anachemsha BIG TIME. Pamoja na hayo itakuwa vizuri kama tutaanza kuonyesha resources gani JK atumie kupambana na matatizo unayoyaona.
Bin Maryam,
Kuna msemo unasema kuwa desperate solutions for desperate issues na kuna mwingine una mengi lakini naweka machache tu hapa ...... then stop the bleeding first......
Katika hili Kikwete na watanzania wako kwenye desperate position na hii bei ya umeme na nishati inaathiri kila kitu kuanzia bei ya usafiri hadi uwezo wa watu kununua (au kutunza pesa) na kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye.
Inapofikia wananchi wanajiuliza kama wanunue chakula au walipie umeme basi ujue kuwa hali imekuwa ngumu. Multiplying effect ya bei ya nishati sasa inaathiri kila kitu na kunakoelekea itakuwa ni the worst scenario ya depression.
Kinachoombwa hapa ni emergency measures ili kurudisha confidence ya wananchi economically na hakika kuwa energy prices zikizuiwa kupanda kwa sasa basi vitu vingine vitasimama kupanda bei na kwa taratibu lakini kwa hakika bei zote zitastabilize.
Ukiuliza kuwa serikali itumie resources gani kusaidia katika hili nadhani jibu unalo kuwa waaache matumizi ya ajabu ikiwemo ya kuendesha baraza la mawaziri kwa zaidi ya bilioni moja kwa mwezi na mengineyo mengi ili kunusuru taifa.
Kuna uwezekano mkubwa kuwa tunachofanya ni kuomba serikali kufanya vitu ambavyo imejaribu kuvifanya kwa zaidi ya miaka 40 bila mafanikio au mafanikio madogo sana.
Au kuna uwezekano mkubwa tu kuwa serikali ilichukua majukumu ambayo haikutakiwa kuyachukua.
Tunachoomba hapa ni serikali kuacha kufanya kile ambacho imekuwa inafanya for 40 years - business as usual - na kutojali wananchi wengi. Serikali kuna wakati inabidi iache ubadhirifu na matumizi mabaya ya pesa za kodi ili kusaidia kustabilize uchumi wa nchi kwenye nyakati kama hizi.
Kuna mtu anatoa mfano wa Joji Bush kutoa rebate hili kuchochea shughuli za uchumi. Mpaka sasa bajeti ya serikali ya Marekani ina madeni makubwa. Je rebate checks zinatoka kwenye mfuko gani? Ukweli ni kuwa rebate checks zitaongeza deni la serikali. Na baadaye kulipa deni ili itabidi serikali ikate mifuko ya kuwasaidia wananchi au iongeze kodi.
Hili la marekani na rebate checks lina ubishi mkubwa katika circle za economists ila in the end wote wamekubaliana kuwa kwa sasa kurudisha confidence kwenye economy ni muhimu kuliko deni la taifa - desperate solutions for desperate issues.....