MwK, is it the right time?? Well, we need something done fast but ina maana Muungwana ameweka kadi zote mezani na hana la zaidi???????
I believe he is more brilliant than already observed......
Au mimi ndio nina daydream wakuu?
Mheshimiwa sana Dk Shein,
Naomba nichukue nafasi hii kwanza kwa kukupongeza kwa kazi nzuri sana unayofanya ya kufungua majengo, vituo, maduka ya nyama na biashara mpya katika nchi. Samahani kidogo kwa kuiita hii kazi yako kwa jina la kazi ya mikasi. Pamoja na haya, natoa wito maalumu kwako na kwa ofisi yako kulinusuru taifa letu tukufu la Tanzania.
Ninakumbusha jambo unalolielewa vyema kabisa kuwa kikatiba wewe una ruhusa ya kufanya kazi ya uraisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pale mambo fulani fulani yanapojitokeza. Moja ya mambo hayo ni pale rais wa nchi anapokosa uwezo wa kutenda kazi zake kikamilifu (incapacitated). Najua wataalamu wa sheria na lugha watatumia tafsiri mbalimbali kuelezea hili neno incapacitated lakini kwa mtizamo wangu na watanzania wengi, Rais Kikwete kwa sasa anafit kabisa definition hii ya kukosa uwezo wa kutenda kazi zake kwa ukamilifu.
Ninakuandikia hili huku nikikumbuka maneno ya mtanzania mmoja aliyewashauri watanzania kwenda kunywa chai na Kikwete kama walipenda sura yake au tabasamu lake. Kazi ya uraisi ni kubwa kuliko Kikwete alivyofikiria na inawezekana ameshindwa tu kusema hili wazi. Kwa vile mkuu wako wa kazi sasa ameshindwa kazi yake na anapeleka taifa la Tanzania kubaya, ni jukumu lako kutimiza kiapo ulichoapa kuwa utachukua kazi ya urais na kufanya kazi yako kwa maadili pindi itakapothibitika kuwa raisi hana uwezo tena wa kufanya hivyo.
Chonde chonde Mheshiwa Shein, nchi yote inakuangalia wewe kufanya the right thing kipindi hiki cha mpito ambacho wanaccm wakifikiria nani wampitishe katika uchaguzi mkuu 2010. Tafadhali sana ikomboe nchi hii kwa kuchukua madaraka ya nchi toka kwa Kikwete na kuzuia zahama inayolikabili taifa la watanzania. Kumbuka kuwa watanzania wengi wamechoshwa na wizi huu unaondelea usiku na mchana wakati nchi ikiuzwa kwa wageni kama njugu.
Ahsante sana na ubarikiwe kwa uamuzi huu unaotakiwa kuufanya haraka sana.
Asante
Mwafrika wa Kike,
Hivi rais mzima unazunguka na mwizi Chenge, kweli hapo kuna neema?
Kitila:
Perhaps, the rhetorical question to ask is: What is it that the opposition parties are going to do about it, if they are that capable as you assert?
Yaani pamoja na misukosuko yote hii nchini na ndani ya CCM, hata msisimko katika upinzani hakuna? Na hii ni mwaka mmoja tu na nusu kufikia kwenye uchaguzi mwingine, 2010!

MWK, hilo neno incapacitated hapo nadhani litaleta mgogoro hapa...kuwa na maana inayokubalika, na ambayo kwayo JK anaweza kufit ili kuhalalisha makamu wa rais 'kuchukua nchi'.
Nadhani wataalam wa sheria wangetupa hasa ni mazingira gani tunaweza kusema kuwa rais amekuwa incapacitated?
yaani mnavyo- discuss kuhusu huyu vasco da gama mimi nataka hata kulia,yaani jamaa kakalia kutembea tembea tu huku nyumba yake inawaka moto,watanzania walikosea sana kumchagua huyu jamaa kuwa raisi, na uhakika kabisa haya mambo yangetokea na raisi ni salim ahmed salim hawa viongozi fisadi wangeishia jela, lakini huyu check-bob wetu anaangalia tu jinsi mawaziri na viongozi wengine wanavyshindana kuiba, JK BURE KABISA.