Ombi langu Maalum kwa Mhe Rais:Naomba uwaachie Rais wa DARUSO na Katibu wa TGNP

Mkuu Gembe, umeeleza vizuri. hawa vijana na hata mabango yao wala si ya uchochezi bali ni kufikisha tu ujumbe walionao kwa jamii ni kama tu magazeti. watanzania tuna uhuru wa ku eleza matatizo yetu pasipo kubughudhiwa na mtu yoyote. hapa ni hasira tu za uongozi wa chuo ndiyo zinasababisha wanafunzi wateseke, hii ni mbaya sana.
hata hiyo kesi itafutika tu mbona zile za mwaka jana zilifutika baada ya kuona makosa ya wanafunzi yanatakiwa yasikilizwe na uongozi wa chuo na wapewe adhabu na chuo?
 
Unaweza kutusaidia kifungu cha Katiba (ya Marekani) alichotumia Rais Obama? ... siamini kama alikurupuka tu ... na hiyo Guantanamo Bay iliundwaje na kwa mamlaka ya nani?

Mkuu Ilongo,

Obama ameingilia suala la Guantanamo Bay,nakuamuru kesi hizo za Kijeshi zisimamishwe kwa kuwa Obama kama Rais wa Marekani kikatiba ndiye amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya Marekani.Kiprotokali Obama ameamuru kesi za kijeshi za Guantanamo Bay zisimamishwe ili mchakato wa kesi hizo upitiwe upya.So anayo mamlaka kwa sababu suala lenyewe ni la kijeshi,but in our case ,Udsm Student's Saga is totally different.Norma legal procedure should be adhered.Hapo ndipo kuliko na tofauti kati ya hizi ishu mbili

Ndiyo maana naona kama Jk tunampa fursa ya kuingilia mahakama zetu,au kuendesha mahakama za kiraia as if ni za kijeshi.Ndiyo maana kule Mara nilipinga Suala la Lowasa pia kuamuru polisi kuachia raia waliokua wamekamatwa wakiwa na mabango.Nilipinga nikasema huo uwezo Lowasa aliutoa wapi kisheria.Hata kama alikua waziri mkuu.Yes alifanya jambo jema kuwanusuru wale waliokua wananyanyaswa,lakini je kama tulimsifia alipoamuru mtu kuachiwa huru,je asingeutumia huo uwezo wakati mwingine kuamuru mtu kukamatwa?

Au kwa hii kesi kama anaweza kuamuru wanafunzi wa UDSM waachiwe,je huoni anaweza kutumia uwezohuo kuamuru watu wakamatwe,au nwaliowekwa detention kama ni mafisadi au maswahiba wake waachiwe?
 
Mheshimiwa Rais ,

Naomba nikupe pole na jinsi khali ya uchumi inavyoendelea hapa nchini,Naona jitihada zako mpya za kuweza kufufua uchumi wa nchi hii zikianza kwa nguvu mpya na kasi mpya tena.Mikutano yako na viongozi wa BOT,Wizara ya Fedha itasaidia sana japo kuwapa watanzania maisha bora waliyoyasubiri toka 2005.

Mhe. Rais,
Najua tumekuwa tukikushauri kwa muda mrefu sana kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na tumekusaidia sana katika kuongoza nchini yetu ya Tanzania,tumeweza kuvumbua uozo wa ACTL,Ufisadi katika sehemu mbali mbali,tumekusaidia mambo magumu ambayo kwa khali ya kibinadamu na kirafiki haikuwa rais kufanyika(rejea kashfa ya RDC).

Mhe Rais najua kuna mambo mengine tumekukera sana kwa kuwa haukutaka tuyazungumze hapa .Yawezekana ulifikia hatua ya kuchukia wachangiaji hapa kama alivyofanya mwandishi aliyemmjibu Mzee Mwanakijiji katika akala ya ndege inayopaa ya mwaka 2007.Rais wetu mpendwa tulifanya hivyo ajili ya maslahi ya nchi yetu na kama kuna sehemu tulikosea tunaomba utusamehe

Mhe Rais,Leo nina ombi moja tu naombakwako,Ombi lililo maalum.Naomba uagize Jeshi la Polisi liwaachie hawa vijana wawili,Rais wa DARUSO Mhe. MAchibya na steven Owawa ambaye ni katibu wa TGNP,inawezekana wana kosa ila hawana Hatia,Nakuomba sana utoe maelekezo sasa.Nimesoma habari ya kukamtwa kwao kwa masikitiko makubwa sana sababu hii inajenga picha kwamba watanzania walio wadogo hawawezi kuzungumza lile wanaloliamini ni sahihi.

Mhe Rais,
umekekuwa ukizungumzia demokrasia kwa muda mrefu sasa,Tena inayotoa uhuru kwa watu kuchagu aviongozi waaadilifu .Hawa vijana ni waadilifu sababu wanatetea jamii nzima ya wanafunzi wa vyuo vikuu.

Mhe Mwenyekiti wangu,
Nakuomba sana huku nikikusihi sana uwaachie sababu hawa vijana wanapigania yale yaliyo kweli kwa sasa na wanafanya hivyo kwa ajili ya watanzania masikini(walio wengi).ambao wanategemea msaada wa serikali yao katika maendeleo.

Kwa wanafunzi wa vyuo,Naomba muwe watulivu wakati serikali ikiangalia njia ya kuweza kutatua jambo hili,na nina uhakika Mhe. Rais ataingilia kati jambo hili kwa kuwa linagusa maisha ya watanzania walio wengi.

Mhe. Naomba unisaide japoo hili tu.

Mungu akubariki sana na wasaidie Vijana hawa


Mkuu Gembe,

I beg to differ with you, Je, unataka kuniambia kuwa katiba ya nchi hii inampa mamlaka Rais kuwasamehe watu ambao wanatuhumiwa kufanya makosa? Kama hana uwezo wa kufanya hivyo kikatiba kwanini unamwomba? Let hao vijana wa-face hizo charges na kama inatakiwa msaada basi ni pale Kisutu. Tuweke standards za kurejesha nidhamu na utawala bora. Kufikishwa Kisutu ndiyo mahala muafaka zaidi badala ya kuomba kuvunja sheria.
 
Last edited:
Back
Top Bottom