"Ole wako uzitumie vibaya" haikuwa kauli sahihi kutoka kwa rais kumueleza Meck Sadick hadharani!

Mwasilisha mada uelewe hakuongea vile Kwa sababu ya kuangalia umri alikuwa anatoa order kama kiongozi ...suala la kusema sijui haikuwa vizuri mi sioni tija yake after all hii nchi imefika hatua viongozi lazima wawe makauzu ili mafisadi wasiendelee kutafuna mali za walio wengi
 
hahaha bavicha bana, yaani hamna hoja tena, bora hata ile list of shame mngekua nayo ingewapiga kick, but ndo hivyo tena, ila nawakumbusha 'kama huna hoja, shut up' by lowasa
 
Hapa kazi tuu..muda wa kucheka cheka na kutaniana ndio uliotufikisha hapa tulipo!! Ngosha piga kazi kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala..lazima namba wazisome tuu tumechokaa.
 
ImageUploadedByJamiiForums1455453446.191349.jpg
 
Kwa hilo, naona magu amejitahidi sana mana kwa msukuma matumizi ya lugha tatzo. Ila kiukwel staha ya kuongea bwana pombe kanyimwa sana
 
Ni KAZI TU,
Inabidi mjitune jamani,hanaga lugha laini,sasa kama umezoea lugha ya kubembelezwa ilishatoka hiyo
 
Magu ameomba waandishi wa habari wamsaidie kutambua majipu,UKAWA hawana maana,wamebaki kujadili umbeya. Dr Slaa ndiye kiongozi wa kweli wa upinzani,anakosoa,alionyesha mahali kuna jipu,alitaja hata majina ya mafisadi. Collabo ya Dr Slaa(PhD) upande moja,na Dr Magufuli(PhD) upande wa serikali ingekuwa msaada kwetu. Hii CDM ya team EL nao ni majipu.
 
Keshasema nchi iko hovyo hovyo kwa hiyo sitegemee lugha za pembelezo, heshima na staha wakati Kama huu ropoka tu JPM ndio lugha wanayo stahili majizi na mazembe yote... Tabasamu walifuate msoga
 
Jana kwenye hotuba ya John Magufuli (rais wa Tanzania) alitumia kauli isiyo na weledi kutoka kwenye cheo alicho nacho kumueleza mtendaji wake ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadick! "Nitakupatia hizo fedha na OLE WAKO UZITUMIE VIBAYA" kauli ya "Ole wako uzitumie vibaya" ingawa hamtasema wala kuongea ila kiukweli ilimfedhehesha sana Meck Sadick!

Kwanza Meck Sadick kiumri ni mtu mzima sana kwa Magufuli! Lakini pia ni aina ya watu ambao wamestaharabika! Ile kauli rais aliitoa kama anamueleza kijana mdogo na au mwanaye!

Pili haipendezi kuanza kujenga malengo hasi na inaonyesha kuwa kuna mashaka fulani!

Rai yangu kwa rais; emb ajifikirie kuwa yeye angekuwa ndiye Meck Sadick kwa kauli ile angeipokeaje? Ndiyo maana vyuo vinafundisha communication skills! Ile CL111 pale thietre za UDSM hiyo ndiyo kazi yake! Uongee lipi ukiwa wapi na kwa nani!

Hizi kauli za kutishana kabla hata kazi haijaanza kwa kweli hazijengi! Zinazaa uoga na kutokujiamini! Magufuli atazame mfano wa mawaziri wake walivyokwama! Hii ni kutokana na uoga aliowajengea!
Ulitaka aseme NAKUOMBA NIKO CHINI YA MIGUU YAKO tumia pesa vizuri?
Hapa Kazi Tu!!
 
Msitake kutuletea Mazoea hapa,nakuleta busara za ajabu ajabu,huyu ni rais wa hapa kazi,wala si kama mliowazoea,kubembelezana si awamu hii,na hizo humanistic approach za kujihami hatuzitaki.
 
Sioni shida hapo na aendelee kutumia hizo lugha tu, yanini kuzunguka mbuyu!? Huo utamaduni umetudhorotesha sana watanzania kwa fikra na vitendo na hauna budi kubadilika.
 
Back
Top Bottom