Ole wako Tanzania, viongozi vijana ni wanafiki haswa Zitto: Posho alisema hivi...

Birigita, kwa taarifa yako nimelitumikia hili taifa kwa muda mrefu sana ,nimesema nasikitikia taifa langu kwani wale vijana niliowadhania kumbe sio , Kama unaheshimu waliokuzidi kidogo kwa lolote acha matusi jibu hoja ama kosoa kwa staha kidogo.
 
hakuna mahali nimeona zito amekubali posho, isipokuwa nimeona amezungumzia stahili, sasa posho sio stahili coz hazipo kisheria, wabunge walipaswa kudai nyongeza ya stahili kama mafuta n.k, kweli inakuhitaji kuwa great thinker kumuelewa kamanda zitto kabwe
 
Sidhani kama huyo zito sasa awe ndo sportlight ya watz hasa vijana kwa kila atakalolisimamia,naamini kabisa watz wa leo ni wafuatiliaji wazuri tu wa mambo mnayoyafanya na ww ukiwa mmoja wao kama kweli na ww ni mbunge,unachotaka kutuaminisha ni kipi?labda ni kumchongea huyo zito,ingekuwa bora ukatupa msimamo wako,au na ww ndo walewale mnaoongozwa na maslahi ya chama zaidi au kisa habari zako hazikuandikwa na mwananchi..ningependa kama utatueleza msimamo wako khs posho

msimamo wangu upo hapo juu kwani nimesema wengine kutokana na sababu mbalimbali hatuwezi kusema hadharani , ila tunawaunga mkono wenye uwezo wa kusema .

Mimi hata kama hakutakuwa na posho nina uwezo wa kuendelea kuishi kutokana na pension yangu ni nzuri tuu kwa wastani wa maisha ya kitanzania .
 
wewee ni mbunge? huoni kama hata wewe una jukumu la kupinga kwa nafasi yako kwani zitto alizaliwa kukuonesha kila mwelekeo na kama uligundua hoja ya zitto awali ilikuwa sahihi mbona hukutoka hadharani kumuunga ili asikate tamaaa weka pia sababu kwa nini huwezi wewe kupinga hadharani? lakini pia kumbuka "zitto si msaafu wa vijana nchi hii wala siye QURAN AU BIBLIA kuna vijana wengi bado tunawangazia macho

uMEJIKANYAGA @ ustadh, mada ni zitto kuwa ndumi la kuwili. Mawazo kama "kwani zitto alizaliwa kukuonesha kila mwelekeo" ni upuuz na SIO POINT. Na kwa kauli hii ""zitto si msaafu wa vijana nchi hii wala siye QURAN AU BIBLIA kuna vijana wengi bado tunawangazia macho" inaonesha kuwa uwezo wako wa kufikiri ni mdogo na unakubali kuwa zitto ni mnafik na sio mtu wa kutegemewa kwa kauli za mdomo wake. Siku nyingine jifunze kuyakubali makosa. Au kama hujajipanga ni bora kuacha kuandika upupu kwenye jukwaa la wasomi.
 
Kwa sababu Zitto keshakuwa "mnafiki" basi tusaidie wewe, tuambie uko upande gani, wanaoshabikia au wanaopinga posho ili tukutume.
Usilaumu wakati huna msimamo!!!!
 
Birigita, kwa taarifa yako nimelitumikia hili taifa kwa muda mrefu sana ,nimesema nasikitikia taifa langu kwani wale vijana niliowadhania kumbe sio , Kama unaheshimu waliokuzidi kidogo kwa lolote acha matusi jibu hoja ama kosoa kwa staha kidogo.
What have you done? what is your stand? usilete habari za Zitto hivi na zitto vile.
Come clean, utuambie umepigana kiasi gani na umefanikiwa nini na ume-fail nini na kwa nini?

To me, this seems like another failed attempt to disrupt the issue in question, why do you guys need 200k for sitting in a meeting?!!

Wewe unaleta hii issue hapa kama vile wananchi wameshawishiwa na Zitto kuhusu upuuzi wa kulipana 200k per day. Kama umelitumikia taifa hili, unaona hii ni sawa?
 
hakuna mahali nimeona zito amekubali posho, isipokuwa nimeona amezungumzia stahili, sasa posho sio stahili coz hazipo kisheria, wabunge walipaswa kudai nyongeza ya stahili kama mafuta n.k, kweli inakuhitaji kuwa great thinker kumuelewa kamanda zitto kabwe

Hivi unajua kuwa Mbunge analipwa shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya mafuta kwa mwezi na maana yake ni kuwa kila siku anapewa shilingi 83,333 sawa na lita 37.87 kwa bei ya shilingi 2,200 kwa lita , hata siku ambazo tunakaa Dodoma?

Kuna haja gani ya Mbunge wa Viti maalum kupewa hizo fedha wakati hana hata jimbo la kutembelea? Kuna haja gani wabunge wa majimbo ya mjini kupewa hizo fedha kila mwezi? kwanini pasiwe na ratiba kuwa kwa wakati wote wa vikao vya kamati na vile vya bunge hawatalipwa mafuta? Kwanini Zitto anataka kusema kuwa waseme wanahitaji fedha kwa ajili ya mafuta?

Naomba kuishia hapo , ntarejea baadae kidogo.
 
Tatizo kuna watu mnashambulia bila kujua mantiki ya hoja yangu, soma gazeti la Mwananchi la leo utaona kifungu walichomnukuu Zitto akisema kuwa tatizo wabunge they think small...... hapo hapo anasema kuwa walipaswa kujenga hoja kuwa nishati ya mafuta imepanda bei na hivyo ndio iwe sababu ya kueleza umma kuhusiana na nyongeza ya posho .......hapo unaweza kuona namaanisha kitu gani.
#

we ni kilaza, kwanza ushasema huwezi kuongea kwa sababu fulani so wewe ni muoga na hatuna imani na wewe vile*2 wewe si mtetezi wa umma, pili alichosema zitto ni kutaka kujenga hoja kwamba unaposema unapandisha posho uwe na sababu muhimu na mahususi ambazo hazitawachanganya wananchi, tunajua umeme umepanda, mafuta yamepanda, nyumba zimepanda, so ukijenga hoja kwa kufuata hiyo misingi unaweza ukaeleweka huo ni mfano lakini alafu baadae posho uanyoongeza iwe reasonable,

laikin mwisho utaulizwa je bei zilizopanda zinawahusu wabubge tu, kama ndiyo sawa hakuna swali lakini kama hapana mbona wafanyakazi wengine hawakumbukwi kuongezewa sawasawa na rate ya ongezeko la bidhaa na huduma katika eneo husika?

nadhani ni uelewa tu kuwa hoja tunazidakia katikakati bila ya kwenda ndani zaidi!
nawasilisha!
 
Wewe ndiye mnafiki namba moja uliyefungua account mpya jana tena bila hata kudhubutu kutumia jina lako la ukweli ili tukutambue. Nina mashaka hata kama ni mbunge kweli, na kama ni mbunge basi wewe ni mchumia tumbo mwenye wivu kuliko wa kike.

Baada ya wabunge wa pande zote kushindwa kusimamia imara hoja ya posho na kumuacha Zitto pekee kusimama hoja hii sasa Zitto anapata maadui wengi sana, maana wanajua wananchi wote hatutawaelewa na wanaona kama Zitto anajipatia umaarufu. Wanasahau kuwa masuala ya msingi si ya kufanyia mzaha au kutafutia sifa.

Mleta mada pamoja na wenzako mnaamua kupotosha ukweli na kusema kwamba Zitto alitaka nyongeza ifike milioni 12 kwa mwezi ila isiitwe posho... swala la kuboresha maslahi ya wabunge Zitto alishaliongelea na hata aliandika makala kwenye gazeti kushauri suala hili, mnaweza kusoma kwa kufuata hii link Creating the right incentives for MPs Creating the right incentives for MPs

Kama uliyeleta hii mada hapa kweli ni mbunge basi wewe ni kilaza hata huelewi watu wanapotoa point, incentive anazozungumzia zitto si hela za wabunge kutia mfukoni.

Halafu unataka Zitto asiombe msamaha kama maneno yake ya hasira yaliwakera baadhi ya watu ili mseme ana tabia mbaya.

Onyo kwa wale wote mnaochumia tumbo na kufanya siasa za kipuuzi kumchafua Zitto kwenye suala la posho, msimamo wake uko wazi na utabaki kuwa wazi kwamba haungi mkono posho za vikao kwasababu ni kazi ya wabunge na wanalipwa kwa kazi hiyo. Wananchi tuko nyuma yake. SAY NO TO SITTING ALLOWANCES

Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema "Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho" ………….

Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema "Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana"

Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.
 
Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema “Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho” ………….

Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema “Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana”

Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.

Reveal you identity kwanza, mbona Zitto anaingia hapa kama Zitto
 
Tatizo kuna watu mnashambulia bila kujua mantiki ya hoja yangu, soma gazeti la Mwananchi la leo utaona kifungu walichomnukuu Zitto akisema kuwa tatizo wabunge they think small...... hapo hapo anasema kuwa walipaswa kujenga hoja kuwa nishati ya mafuta imepanda bei na hivyo ndio iwe sababu ya kueleza umma kuhusiana na nyongeza ya posho .......hapo unaweza kuona namaanisha kitu gani.

Lakini mkuu ww ulikuwa wapi usimpenge kwa kauli yake hiyo kule bungeni kama kweli ulimwona ni mnafiki? Acha kutupiga changa la macho na kauli zako hizo za kupakana matope.
 
Wewe ndiye mnafiki namba moja uliyefungua account mpya jana tena bila hata kudhubutu kutumia jina lako la ukweli ili tukutambue. Nina mashaka hata kama ni mbunge kweli, na kama ni mbunge basi wewe ni mchumia tumbo mwenye wivu kuliko wa kike.

Baada ya wabunge wa pande zote kushindwa kusimamia imara hoja ya posho na kumuacha Zitto pekee kusimama hoja hii sasa Zitto anapata maadui wengi sana, maana wanajua wananchi wote hatutawaelewa na wanaona kama Zitto anajipatia umaarufu. Wanasahau kuwa masuala ya msingi si ya kufanyia mzaha au kutafutia sifa.

Mleta mada pamoja na wenzako mnaamua kupotosha ukweli na kusema kwamba Zitto alitaka nyongeza ifike milioni 12 kwa mwezi ila isiitwe posho... swala la kuboresha maslahi ya wabunge Zitto alishaliongelea na hata aliandika makala kwenye gazeti kushauri suala hili, mnaweza kusoma kwa kufuata hii link Creating the right incentives for MPs Creating the right incentives for MPs

Kama uliyeleta hii mada hapa kweli ni mbunge basi wewe ni kilaza hata huelewi watu wanapotoa point, incentive anazozungumzia zitto si hela za wabunge kutia mfukoni.

Halafu unataka Zitto asiombe msamaha kama maneno yake ya hasira yaliwakera baadhi ya watu ili mseme ana tabia mbaya.

Onyo kwa wale wote mnaochumia tumbo na kufanya siasa za kipuuzi kumchafua Zitto kwenye suala la posho, msimamo wake uko wazi na utabaki kuwa wazi kwamba haungi mkono posho za vikao kwasababu ni kazi ya wabunge na wanalipwa kwa kazi hiyo. Wananchi tuko nyuma yake. SAY NO TO SITTING ALLOWANCES
Achana ne huyu jamaa, nimemwambia ni boga kabisa, nia yake ni sisi watu wazima na nanihii zetu tumjadili Zitto badala ya kujadili Uhalali wa SITTING allowance, na uhalali wa Ongezeko la SITTING ALLOWANCES kwa wabunge.
 
hapa hoja si mleta mada kupinga posho, hoja ni unafiki wa zitto.
Kwann kwenye media na kwenye majukwaa aipinge halafu akiwa na wenzake aikubari?
Anakuwa kama simba kwenye ngozi ya kondoo
 
Zitto amewadanganya vijana kuhusu ahadi ya kupeleka hoja binafsi ya tatizo la ajira kwa vijana..kwa hili nitaendelea kumweka kwenye list ya wanasiasa wanaotumia matatizo ya vijana kama ngazi ya kuelekea anapotaka.

wewe Matumbo hii hoja kaijadili kwenye respective thread tushakujibu kule usipoteze mada inayojadiliwa hapa. Aliyewatuma ni mmija nini? mbona kama vile mpo kazini wenzetu?
 
Kwa maneno yake hayo kwa kweli ni mnafiki,tena anacheza na akili za watz,lakini mi naamini ipo siku mapinduzi yatatokea katika nchi hii,

Hata kama itapinduliwa, viongozi watakaoongoza baada ya hayo mapinduzi yako watakuwa na matendo kama ya hawa wanaotuongoza sasa. Kwa sasa wasafi ni wachache na hawana madaraka makubwa, hebu angalia tangu ngazi ya balozi wa nyumba kumi ufisadi wanaofanya. Tehe
 
hapa hoja si mleta mada kupinga posho, hoja ni unafiki wa zitto.
Kwann kwenye media na kwenye majukwaa aipinge halafu akiwa na wenzake aikubari?
Anakuwa kama simba kwenye ngozi ya kondoo
Hebu tuonyeshe wapi amekubali SITTING ALLOWANCES?
 
kwa akili za huyu mbunge, atakuwa ni yule mwenye gari lilozaa kule wanapotuletea umeme kwa bwawa lenye matope kuliko maji.
 
Hata kama itapinduliwa, viongozi watakaoongoza baada ya hayo mapinduzi yako watakuwa na matendo kama ya hawa wanaotuongoza sasa. Kwa sasa wasafi ni wachache na hawana madaraka makubwa, hebu angalia tangu ngazi ya balozi wa nyumba kumi ufisadi wanaofanya. Tehe
When you decide to be a looser, don't involve others.
kama wewe umejikatia tamaa, tulia tu,
kama umeajiriwa, basi fanya kazi, ngoja upate mshahara mwisho wa mwezi na ukalipe bills,
kama hautatosha, kakope kwa duka la Mangi.
 
Zitto ni mnafiki hakuna anachotetea , ila anatafuta hoja za kuugilibu umma wa watanzania ,huku akiwa kwenye vikao ni unafiki mtupu anaendekeza , nimeamua kuweka wazi hapa na kama anabisha aeleze kwenye press yake anayotegemea kuifanya leo nini alisema kwenye kikao.

Naona umedhamiria kweli kweli kumpaka matope Zitto. Najua huna nia ya kweli ya kuwatetea WAVUJA JASHO ndio maana unapata nafasi ya kueneza siasa zako hizi za kupakana matope. Mwana wa magamba, mbunge FEKI.
 
Tatizo kuna watu mnashambulia bila kujua mantiki ya hoja yangu, soma gazeti la Mwananchi la leo utaona kifungu walichomnukuu Zitto akisema kuwa tatizo wabunge they think small...... hapo hapo anasema kuwa walipaswa kujenga hoja kuwa nishati ya mafuta imepanda bei na hivyo ndio iwe sababu ya kueleza umma kuhusiana na nyongeza ya posho .......hapo unaweza kuona namaanisha kitu gani.
MKUU UPO SAHIHI, WANAOKUPINGA 'they think small....'
 
Back
Top Bottom