Oktoba 14: Tumuenzi Mwl Nyerere. Lete mistari ya nyimbo za kizalendo za zamani!

"Nyerere Baba wa Taifa ee, Nyerere Jemedari wetu ee!
Tunakusifu kiongozi wetu, kwa kazi kubwa unayoifanya ya Ukombozi......"

Wimbo ulipigwa na kuimbwa na Mlimani Park, Sikinde Ngoma ya Ukae mwaka 1979! Yaani ni kama walijua ataitwa BABA WA TAIFA!!
 
ni kweli sikinde waliona mbali leo hii tuna vijana wa bongo wa fleva matusi mtindo mmoja.
 
Bomu limeshapasuka, mabepari wanahangaika, walanguzi wanatapatapa aaaaaahh~~~
wahujumu nao wako ndanieeeeeeeeeeeeeeeeee!!
Nikilala nikiamkaaa sabuni haionekani,
nikilala nikiamkaaaaaaah sukari haionekaniii
Kumbe sababu ya walanguzieeeeeeeeeeeeeeeeeeee>>>>>>>>>>>>
Amandlaaaaaaa
 
Sisi ndio vijana wako Mwalimu Nyerere, tutakaokilinda Chama cha Mapinduzi,
Hongeera mwenyekiti mwalimu Nyerere, hongeera na makamu Ali Hasaniii x 2

:):):):):)

enzi hizoooo, mstarini tunafundishwa ukakamavu, gwaride na salute na askari wa mgambo wa kijiji. Saafi saaanaaa
 
kuna wimbo mmoja umepigwa na bendi fulani wimbo unaitwa 'tanzania yetu'




Nyerere.jpg
TANZANIA YETU NDIO NCHI YA KUSIFIKA
KOTE ULIMWENGUNI WATU WOTE WATAMBUA
TANZANIA YETU NDIO NCHI YA FURAHA!
NAYE BABA NYERERE NDIYE WETU MUHISANI
NAYE NDIYE ALIYELETA UHURU .....
 
Back
Top Bottom