Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, yateketea kwa Moto!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,641
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, imeteketea kabisa kwa moto, jana usiku wa manane, na asubuhi hii, pamebakia kuta tupu na bango linaloonyesha hapa ndipo zilipokuwepo ofisi hizo!.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Taarifa ya Habari ya TBC asubuhi ya leo, ambapo mwandishi wa TBC, alionyesha moto huo, hatua kwa hatua na jinsi mji wa Dodoma wenye hadhi ya mji mkuu kivuli wa Tanzania, isivyo kuwa na huduma za uhakiza za zima moto.

Huku akishuhudia kwa macho yake mwenyewe, Mkuu wa Dodoma, Dr. James Nsekela, na Kamanda Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Zelote Stephen, walikosa cha kusema, bali kushudia tuu jinsi moto huo ulivyokuwa ukiiteketeza ofisi hizo, huku magari ya zimamoto yamepaki pembeni kutokana na kuzidiwa uwezo na moto huo.

Dr. Nsekela, amesema ni mapema mno kuja chanzo cha moto huo, wakati Zelote Stephen alisema, sina la kusema zaidi ya unachokishuhudia hapa!.

Hata hivyo, wakazi wa Dodoma, walijitolea kuokoa baadhi ya magari, kwa kuyaburuta kwa nguvu, toka eneo la hatari, huku magari hayo yakiwa yamefungwa, mengine waliyabeba na kuyasogeza.

Tukio hili ni la kusikitisha sana, lakini pia huu, ndio uwezo wa serikali yetu, kupitia jeshi lake la zimamoto, katika kukabiliana na majanga ya moto.

Jengo la Nasaco jijini Dar es Salaam lilipoteketea kwa moto, ule mwaka 1996, nilishuhudia kwa macho yangu tukio hilo lililotokea mchana kweupe, na liliteketea likaishia licha ya zima moto za jiji, Mamlaka ya Bandari na Uwanja wa Ndege kujitahidi kuudhibiti, zilishindikana kufuatia kutokuwepo nchini, zimamoto zenye uwezo wa kuzima moto ghorofa ndefu. Huu wa Dodoma, umetokea usiku, na ofisi hizo, sio za ghorofa.

Leo wananchi wa Dodoma, hawataamini macho yao watakaposhuhudhia uwanja wa wazi wa ghafa wenye majivu meusi na kuta nyeusi zisizo na paa, uliochukua nafasi ya zilipokuwepo ofisi hizo, na butwaa kubwa zaidi, itawakumba watumishi wa ofisi hizo, watakaoripoti ofisini asubuhi hii, kukuta hakuna ofisi.

Pia pole ziwaendee wafanyakazi wenzangu na mimi, ambao tunajiaminisha ofisini ndipo mahala salama zaidi pa kuweka nyaraka nyeti za binafsi, hata yale mafungu makubwa ya migao, ambayo huwezi kuiweka benki kwa kuogopa maswali, sambamba huwezi kuziweka nyumbani kwa kuhofia kudhibitiwa matumizi yake, huziweka kwenye droo za ofisi, achilia zile safe za petty cash!.

Poleni wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake.
 
Uzembe wa mwenye ofisi,tutaambiwa hitilafu ya umeme. Lini watanzania tutajifunza utamaduni wa preventive.maintaince:confused2:
 
Ikulu ya DSM iliungua kwa moto wakati Mzee Mkapa, zimamoto walishindwa kuzuia uharibifu japo waliuzima moto kwa taabu. Watanzania hatukuambiwa sababu na mpaka leo hakuna ajuaye nini chanzo cha moto ule. Orodha ya ofisi za serikali zilikwishaugnua kwa moto ni ndefu -Mambo ya ndani, ardhi, Nasaco, hotel ya Sea Cliff, paradise, nk.

Nini kimebakia kuungua?
 
Kama huo wameuangalia unavyoishia mpaka majengo yanakuwa majivu, inamaanisha kama ndo ingekuwa ni jengo la bunge ndo linaungua maana yake ni kwamba muda huu tungekuwa twaongelea multibillions loss, huh!!
 
dah

hata pakiungua ni sawa, nyaya zilikuwa zimechoka. ile mitungu ya gesi imewekwa kama mapambo, nda hakuna gesi
hitilafu ndogondogo zilikuwa zinatokea mara kwa mara. sasa limeungua lote

wajifunze na pole zao
 
Nimecheka sana, eti ofisi ya zimamoto iko kilometa mbili kutoka ilipo ofisi ya mkuu wa mkoa, lakini magari ya zimamoto yalichukua masaa mawuili kufika eneo la tukio.
Hii inamaana kuwa magari yalitumia saa moja kwa kilometa.
Hii ni kichekesho sana.
 
Ikulu ya DSM iliungua kwa moto wakati Mzee Mkapa, zimamoto walishindwa kuzuia uharibifu japo waliuzima moto kwa taabu. Watanzania hatukuambiwa sababu na mpaka leo hakuna ajuaye nini chanzo cha moto ule. Orodha ya ofisi za serikali zilikwishaugnua kwa moto ni ndefu -Mambo ya ndani, ardhi, Nasaco, hotel ya Sea Cliff, paradise, nk.

Nini kimebakia kuungua?

Mkuu umesahau kuiweka BOT (Benki Kuu ya Tanzania), Jengo la Ushirika pale chini upande zillipokuwa ofisi za Brela
 
Hii inaonyesha wazi kuwa ofisi imechomwa kuficha mazambi yao (kupoteza ushaidi) subirini mtasikia tu.....
 
Jamani mkisema serikali ya CCM inazemeba kwenye issues kama hizi ni uchochezi wa hali ya juu. Mnataka kuvunja amani na utulivu wa nchi yetu?
 
mnategemea nini kuhusu Serikali yenu? Hamuwaoni kwenye kampeni thithiem wanasema "mkiichagua thithiem tutajenga barabara za juu!. Tangu uhuru mbona yaliwashinda? Wanachojua ni ukwapuaji na si maendeleo!
Wadanganyika mlie tu!
 
Afadhali iungue ili wajenge nyingine. Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, ndiyo ofisi yenye mwonekano mbaya kuliko ofisi zote za wakuu wa mikoa hapa nchini ukilinganisha na hadhi ya mji wa dodoma. Majengo yake ni choka mbaya kama vibanda vya kufugia kuku.
 
aisee hii ni balaa, ila tafsiri ya chanzo cha moto huo inaweza kuwa very controversy. subiri muone mi najua kilichotokea pale.
 
Jamani mkisema serikali ya CCM inazemeba kwenye issues kama hizi ni uchochezi wa hali ya juu. Mnataka kuvunja amani na utulivu wa nchi yetu?
Usikimbilie kusema ni UCHOCHEZI ilhali ndiyo ukweli HALISI.

Tuambie ni serikali ya chama gani iliyokuwa madarakani?
Na ni kwanini wanashindwa kununua magari ya zimamaoto lakini wanaweza kununua VX za watumishi wa serikali yake na kuaguza gari zaidi 60 kwa ajili ya kampeni?
Ni kwanini wanafikiri kujenga barabara za juu na kutengeneza mtandao wa mabasi yaendayo kasi wakati huduma ya msingi ya uokozi na zimamoto iko zii?

Katika hili CCM ndiyo wanataka kuvunja amani kwa wamepoteza kumbukumbu nyingi za maana za wanachi wa Tanzania.

 
sijui walikua na bima???
Serikali huwa haikati bima, hata magari ya serikali hayana bima, ukigonhwa imekula kwako.
Hata shirika la reli hali bima, yaani ukisafiri na treni zetu, liwalo na liwe, hakuna bima.
Kisheria ndege na meli, haziruhusiwa kusafirisha abiria bila bima, angalau ATC ina bima kama shurti la ICAO, lakini Reli na meli za TRC hazina bima, hata wale wahanga wa ajali ya MV Bokoba hakuna walichoambulia au ile ajali ya Treni kule Dodoma.

Hii ndio serikali yetu ya chama chetu!.
 
Ikulu ya DSM iliungua kwa moto wakati Mzee Mkapa, zimamoto walishindwa kuzuia uharibifu japo waliuzima moto kwa taabu. Watanzania hatukuambiwa sababu na mpaka leo hakuna ajuaye nini chanzo cha moto ule. Orodha ya ofisi za serikali zilikwishaugnua kwa moto ni ndefu -Mambo ya ndani, ardhi, Nasaco, hotel ya Sea Cliff, paradise, nk.

Nini kimebakia kuungua?

Nadhani yalitolewa maelezo kuwa chanzo ilikuwa pasi ambayo iliachwa bila kuzimwa baada ya kutumika
 
Back
Top Bottom