Ndugu zangu wanaJF,
Tusiichezee nguvu ya wananchi hata siku moja, kwa usalama wa Taifa letu. Toka juzi nimekuwa nikifanya jitihada mbalimbali za kutuliza munkari ya wananchi wa kijiji cha Mwabangu. Watu wakichoka ni hatari sana.
Mimi sijawaangukia Resolute na wala siwezi kuwaangukia hata siku moja. Wananzega wanachotaka ni maendeleo na haki yao ya kulipwa fidia kwa mali yao iliyohodhiwa na ama kuvunjwa miaka 15 iliyopita, wananzega hawataki mbunge mwehu anayeambiwa sasa tutawajengeeni shule kadhaa, maabara kadhaa, tutawawekeeni lami, tutawalipeni fidia zenu n.k na mbunge huyo akakataa akang'ang'ania maandamano tu! Tulichokifanya sisi ni kukubali kwenda mezani na kuanza mazungumzo na mpaka sasa tupo katika hatua mbalimbali, tukishindana tutaingia Barabarani mpaka mgodini. Nyie subirini tu na mtaona
Ndugu zangu wanaJF,
Tusiichezee nguvu ya wananchi hata siku moja, kwa usalama wa Taifa letu. Toka juzi nimekuwa nikifanya jitihada mbalimbali za kutuliza munkari ya wananchi wa kijiji cha Mwabangu. Watu wakichoka ni hatari sana.
Mimi sijawaangukia Resolute na wala siwezi kuwaangukia hata siku moja. Wananzega wanachotaka ni maendeleo na haki yao ya kulipwa fidia kwa mali yao iliyohodhiwa na ama kuvunjwa miaka 15 iliyopita, wananzega hawataki mbunge mwehu anayeambiwa sasa tutawajengeeni shule kadhaa, maabara kadhaa, tutawawekeeni lami, tutawalipeni fidia zenu n.k na mbunge huyo akakataa akang'ang'ania maandamano tu! Tulichokifanya sisi ni kukubali kwenda mezani na kuanza mazungumzo na mpaka sasa tupo katika hatua mbalimbali, tukishindana tutaingia Barabarani mpaka mgodini. Nyie subirini tu na mtaona!
Hakuna chama eti huwa kina nguvu ya umma, hii huja automatically kwa maamuzi ya wananchi panapokuwa na kero sugu na isiyopatiwa ufumbuzi na mfumo uliopo!
Wananchi hawakuandamana bali waliufunga mgodi tu
Baada ya mawe kurushwa na pande mbili upande wa wanaanchi na upande wa Muwekezaji,
wamekusanyika eneo karibu na polisi na ofisi za CCM wilaya ambao waliamua kumfata mbunge na kumtaka atangulie kuongoza maandamano ya kuwatoa wenzao waliokamatwa hapo wakaampiga polisi wakawahi na kumkamata na yeye na vijana zaidi ya ishirini wote sasa wapo polisi baada ya kumpeleka kupata huduma ya kwanza hospitali hivi sasa yupo ndani.
Atakuwa ameshapozwa huyo. Makelele yote yale kumbe alikuwa anatafuta sababu ya kuongeza uzito wa akaunti yake ya benki. Ama kweli kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake. Ndiyo maana hata mimi siachi kula rushwa.
Hao wananchi wamekosea kujichukulia sheria mkononi. Wanataka kumpiga Mbunge wao!.
Taarifa mpya CCM mkoa wanajaribu kumuokoa ili asipelekwe mahakamani kesho, Jeshi la Polisi linataka wampeleke Mahakamani.
Hapa Nzega nilipofikia kuna kijiwe kinaitwa Meza ya Duara wanadai mgogoro huo umekua mkubwa kwakua Serekali ilitaka kuwalipa Fidia watu ambao walikua na Haki watu hao walikua 17,baada ya Mbunge kuingia madarakani aliongeza list ya watu na kudai kuwa wanaotakiwa kulipwa ni watu 450, na hapa inasemekana ameweka majina hewa na hapa uongozi wa wilaya ukaona kuna kitu anataka kupata ukaanza mvutano na katika kuhakiki ikajulikana kuna majina hewa na kuna ndugu zake ambao si wachimbaji na fidia ikitoka kwa list hiyo maana yake na yeye atakua amepata mshiko hili nalo limechangia mgogoro huo unaoendela. Sasa, inasemekana kesho atapandishwa kizimbani na yeye.
Indeed kama amefanya wizi inabidi ajibu mashitaka..!!Taarifa mpya CCM mkoa wanajaribu kumuokoa ili asipelekwe mahakamani kesho, Jeshi la Polisi linataka wampeleke Mahakamani.