Nzega: Risasi zatumika kumuokoa Mbunge Kigwangalla

MVUA GAMBA

Senior Member
Apr 13, 2011
102
63
Wana Jf nipo nzega nikitoka Mwanza katika ziara ya Ndg ridhwani kikwete.

Usiku huu nikiwa napata chakula nikasikia Risasi zinalia Mjini nikaamua kufatilia na kupata taarifa kuwa Kuna Mgodi ambao unaitwa Isunga Ngwanda ambao siku Mbili zilizopita Mbunge na Wananchi waliungana Kuufunga.

Leo Kilicholeta Vurugu ni Pale Mbunge wa Nzega alipoenda kuwafata wananchi alioshirikiana nao kuufunga Mgodi na kuwataka kuufungua mgodi na yeye akijiunga na Polisi kuwataka wananchi wale waondoke wamuachie muwekazaji.

Wananchi walipandwa na Hasira na kumvamia mbunge na Kuanza kumpiga na Kuvunja Gari ya Daktari wa Wilaya ambayo aliazima naambiwa akiwa nzega huazima gari ya Daktari wa wilaya na kuitumia.

Wananchi hao wenye hasira waliamua kumpiga mbunge kwa kitendo chake cha kuwasaliti wananchi hao na leo kuungana na polisi na wawekezaji.Polisi ilibidi kutumia silaha za moto kumuokoa na na kuwakamata baadhi ya watu na kuwepeleka polisi jambo lilifanya wananchi kuandamana kwenda kuvamia kituo cha Polisi na matokeo yake Polisi kutumia Risasi kuwatawanya wananchi wao.

Liliwaudhi wananchi nitukio la Mbunge Kigwangala kuwageuka wananchi na kujiunga na wawekezaji na Polisi hivi sasa kunavurugu nzega mjini na Maeneo ya Isunga ktk Mgodi huo.

==================
UPDATES:

Taarifa mpya CCM mkoa wanajaribu kumuokoa ili asipelekwe mahakamani kesho, Jeshi la Polisi linataka wampeleke Mahakamani.

Hapa Nzega nilipofikia kuna kijiwe kinaitwa Meza ya Duara wanadai mgogoro huo umekua mkubwa kwakua Serekali ilitaka kuwalipa Fidia watu ambao walikua na Haki watu hao walikua 17,baada ya Mbunge kuingia madarakani aliongeza list ya watu na kudai kuwa wanaotakiwa kulipwa ni watu 450, na hapa inasemekana ameweka majina hewa na hapa uongozi wa wilaya ukaona kuna kitu anataka kupata ukaanza mvutano na katika kuhakiki ikajulikana kuna majina hewa na kuna ndugu zake ambao si wachimbaji na fidia ikitoka kwa list hiyo maana yake na yeye atakua amepata mshiko hili nalo limechangia mgogoro huo unaoendela. Sasa, inasemekana kesho atapandishwa kizimbani na yeye.

na Mustapha Kapalata, Nzega

MBUNGE wa Jimbo la Nzenga, Mkoa wa Tabora, Dk. Hamis Kigwangalla (CCM), jana alinusurika kipigo huku gari lake likivunjwa kioo cha mbele kufuatia vurugu kubwa zilizozuka katika mgodi wa wachimbaji wadogo ulioko kijiji cha Mwabangu, Kata ya Nata dhidi ya wawekezaji wanaomiliki eneo hilo.

Akizungumuza baada ya kutoka katika kikao cha ulinzi na usalama, Dk. Kigwangalla alisema kuwa amefanyiwa vurugu na wawekezaji hao ambao hawana dhamana na mgodi huo wakati akiwapigania wachimbaji wadogo wanaotaka kuporwa eneo lao la machimbo na wawekezaji hao.

Mbunge huyo ambaye ameonekana adui mkubwa wa wawekezaji katika Wilaya ya Nzega, aliwasili kijijini hapo baada ya kupata taarifa kuwa wamiliki hao wapya wana mpango wa kuwafanyia vurugu wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakimiliki eneo hilo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla aliwatuliza wananchi pamoja na wachimbaji kwa ujumla ili kupata suluhu ya tatizo hilo, juhudi ambazo hazikuzaa matunda hatua iliyoibua machafuko makali baina ya pande hizo na kuanza kurushiana mawe.

Mbunge huyo alipambana vikali na kukoswa koswa na mawe ya wawekezaji hao na kuungana na wachimbaji wadogo mpaka kufikia hatua ya kutuliza vurugu hizo baada ya Jeshi la Polisi kuwasili katika eneo hilo licha ya gari lake lenye namba za usajiri T 357 BMP aina ya Caldin kuvunjwa kioo cha mbele.

Dk. Kigwangalla ambaye ameapa kupambana hadi mwisho, alisema katika vurugu hizo wachimbaji wadogo walimpiga mmoja wa wamiliki wa eneo hilo jiwe la kichwani na kumsababishia jeraha kubwa.

Alimtaja majeruhi huyo kuwa ni Moses Kichambati ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega na anaendelea na matibabu.

Baadhi ya wachimbaji hao wakizungumuza kwa nyakati tofauti, walisema kuwa chanzo cha mgogoro huo ni wawekezaji kuingilia eneo lao kijijini hapo, huku wakiacha eneo ambalo wamekuwa wakilimiliki kwa muda mrefu.

Walisema kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na serikali ya wilaya imeshindwa kuutatua mpaka zilipotokea vurugu hizo ambazo zimesababisha wachimbaji hao kujeruhiwa na uharibifu mkubwa wa mali kutokea kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Wilaya, Yusuph Sarungi, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo majira ya saa sita mchana na kusababisha majeruhi wawili. Polisi inamshikilia mtuhumiwa mmoja na upelelezi unaendelea kubaini chanzo hicho cha vurugu.

Aliongeza kuwa tatizo hilo linapaswa kutatuliwa na wizara husika ili kurejesha mahusiano mema kwa wananchi hao na wawekezaji ambapo kila upande unadai una haki kwa eneo hilo.
 
mkuu jana ulisema wewe ni mwalimu huko mwanza,umeamua kutembea na huyo rizone?mwenzio mtoto wa mjini huyo
 
mimi sio nabii, but kuna post niliweka hapa kwamba jamaa hakuwa nao............
 
Wana Jf nipo nzega nikitoka Mwanza katika ziara ya Ndg ridhwani kikwete.

Usikuu huu nikiwa napata chakula nikasikia Risasi zinalia Mjini nikaamua kufatilia na kupata taarifa kuwa Kuna Mgodi ambao unaitwa Isunga Ngwanda ambao siku Mbili zilizopita Mbunge na Wananchi waliungana Kuufunga.

Leo Kilicholeta Vurugu ni Pale Mbunge wa Nzega alipoenda kuwafata wananchi alioshirikiana nao kuufunga Mgodi na kuwataka kuufungua mgodi na yeye akijiunga na Polisi kuwataka wananchi wale waondoke wamuachie muwekazaji.

Wananchi walipandwa na Hasira na kumvamia mbunge na Kuanza kumpiga na Kuvunja Gari ya Daktari wa Wilaya ambayo aliazima naambiwa akiwa nzega huazima gari ya Daktari wa wilaya na kuitumia.

Wananchi hao wenye hasira waliamua kumpiga mbunge kwa kitendo chake cha kuwasaliti wananchi hao na leo kuungana na polisi na wawekezaji.Polisi ilibidi kutumia silaha za moto kumuokoa na na kuwakamata baadhi ya watu na kuwepeleka polisi jambo lilifanya wananchi kuandamana kwenda kuvamia kituo cha Polisi na matokeo yake Polisi kutumia Risasi kuwatawanya wananchi wao.

Liliwaudhi wananchi nitukio la Mbunge Kigwangala kuwageuka wananchi na kujiunga na wawekezaji na Polisi hivi sasa kunavurugu nzega mjini na Maeneo ya Isunga ktk Mgodi huo.

keli hata mi niko nzega niliskia risasi wakati napata mlo hapa ndasa. Nilijua wazee wa kazi wemevamia mahali....hapa hapa ndasa wakati ffu wamepaki risasi ilifyatukia hewani kidogo tutoke nduki.....ova
 
Anatumia gari ya daktari wa wilaya ilihali ana vogue! What a disgusting impostor!!!
 
Duh na haya matatizo ni just a tip of the iceberg...

Mbaya zaidi serikali bado inafanya more of the same sehemu nyingine, huku wanaacha matatizo ambayo hata wajukuu wetu watayarithi. In short its scary. Wamemaliza kugawa migodi sasa wanagawa ardhi kwa wakulima wakubwa.., sijui hawaoni kitakachotokea mbeleni au 10% ndio imewafumba macho.
 
Kingwangalla ni kigeugeu mwanzo mwisho. Kwa muda amekuwa anawasema CHADEMA kuwa wanataka nchi isitaliwake, kisa? kwa sababu wanafanya maandamano. Sasa week kala matapishi yake na kuandamana na wananchi kufunga mgodi. True to himself, siku mbili baadae anajitokeza na msimamo tofauti na aliokuwa nao wakati akifunga huo mgodi na wananchi!

Rewinding the tape, ni huyu huyu Kingwangalla aliyejiapiza huko nyuma kuwa angewahamasisha wananchi ili wafunge mgodi wa Resolute, lakini Kingwangalla being Kingwangalla akavamia ka-mgodi kadogo kabisa na sio Resolute. Kama kuna machafuko huko Nzega Kingwangalla atakuwa right in the middle of it kwa sababu ya kung'ata na kupiliza. Leo anasema hiki kesha anafanya the opposite. Kiongozi gani asiyesimamia anachosema?

Huyu bwana angeendeleza ujuzi wake wa kujitingaza jinsi alivyo 'msomi', lakini kwa muda huu mfupi amabapo amekuwa kwenye public eye anaonekana kuwa very immature in his thinking.
 
mkuu jana ulisema wewe ni mwalimu huko mwanza,umeamua kutembea na huyo rizone?mwenzio mtoto wa mjini huyo

Mkuu, Bora ulipotusadia maana watu wengine ni kama wanawafanyia promotion wenzao kwa kupima maji.
 
Kweli hata mi niko Nzega niliskia risasi wakati napata mlo hapa ndasa. Nilijua wazee wa kazi wemevamia mahali....hapa hapa ndasa wakati ffu wamepaki risasi ilifyatukia hewani kidogo tutoke nduki.....ova
 
nilishasema dogo hana gats ya kuifunga resolute. Huyu kigwangala anatafuta umaarufu tu.hana tofauti na yule ndege aitwae hornbill.
 
waangalieni hao wauaji maana ndiyo kazi wanayoonekana kuvutiwa nayo..arusha, tabora,musoma,ngeita,igunga...sijui na walioko india kama watapona
 
Majuzi Kigwangalla aliyasema haya hapahapa JF!
Ndugu zangu wanaJF,

Tusiichezee nguvu ya wananchi hata siku moja, kwa usalama wa Taifa letu. Toka juzi nimekuwa nikifanya jitihada mbalimbali za kutuliza munkari ya wananchi wa kijiji cha Mwabangu. Watu wakichoka ni hatari sana.

Mimi sijawaangukia Resolute na wala siwezi kuwaangukia hata siku moja. Wananzega wanachotaka ni maendeleo na haki yao ya kulipwa fidia kwa mali yao iliyohodhiwa na ama kuvunjwa miaka 15 iliyopita, wananzega hawataki mbunge mwehu anayeambiwa sasa tutawajengeeni shule kadhaa, maabara kadhaa, tutawawekeeni lami, tutawalipeni fidia zenu n.k na mbunge huyo akakataa akang'ang'ania maandamano tu! Tulichokifanya sisi ni kukubali kwenda mezani na kuanza mazungumzo na mpaka sasa tupo katika hatua mbalimbali, tukishindana tutaingia Barabarani mpaka mgodini. Nyie subirini tu na mtaona!
 
Back
Top Bottom