Nyumba ya mtoto wa Mbowe yakamatwa tayari kupigwa mnada

Nyumba inayodaiwa kuwa ya mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam, imekamatwa kwa ajili ya kupigwa mnada, ili kulipa deni la malimbikizo ya mishahara ya waliokuwa waandishi na wahariri wa gazeti hilo, Sh62.7 milioni.

Nyumba hiyo ya ghorofa moja iliyoko katika kiwanja namba 9, Mtaa wa Feza, barabara ya Chipata, Mikocheni A imekamatwa leo Jumatano, Februari 28, 2024 na dalali wa mahakama, kampuni ya udalali ya MM Auctioneer & Debt Collectors.

Dalali huyo alifika katika nyumba hiyo saa 3:40 na kuegesha gari lake nje ya geti la nyumba hiyo.

Baada ya muda mfupi Dadley, ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitoka nje na kumfuata dalali huyo na baada ya kusalimiana, dalali huyo alijitambulisha na jukumu alilokwenda kulitekeleza.

Pia soma:
- Mahakama yaamuru nyumba ya mtoto wa Mbowe ipigwe mnada
Means Mbowe hana milioni 64?
 
IWEKWE NAMBA HAPA MAKAMANDA TUCHANGE NDANI YA SAA 24 TUNAIKOMBOA NYUMBA YA KAMANDA DUDLEY MBOWE, SHIME IWEKWE NAMBA TUANZE KUCHANGA........
Ujinga tu

Mtu tajiri kama huyo imshinde kulipa wafanyakazi only 62M
mpaka wampeleke mahakamani?

Anapoisema serikali wakati yeye anafanya mabaya tu, shame on him.
 
Nyumba inayodaiwa kuwa ya mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam, imekamatwa kwa ajili ya kupigwa mnada, ili kulipa deni la malimbikizo ya mishahara ya waliokuwa waandishi na wahariri wa gazeti hilo, Sh62.7 milioni.

Nyumba hiyo ya ghorofa moja iliyoko katika kiwanja namba 9, Mtaa wa Feza, barabara ya Chipata, Mikocheni A imekamatwa leo Jumatano, Februari 28, 2024 na dalali wa mahakama, kampuni ya udalali ya MM Auctioneer & Debt Collectors.

Dalali huyo alifika katika nyumba hiyo saa 3:40 na kuegesha gari lake nje ya geti la nyumba hiyo.

Baada ya muda mfupi Dadley, ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitoka nje na kumfuata dalali huyo na baada ya kusalimiana, dalali huyo alijitambulisha na jukumu alilokwenda kulitekeleza.

Pia soma:
- Mahakama yaamuru nyumba ya mtoto wa Mbowe ipigwe mnada
Wapambe wangelisema ni magazo kutoka juu bora imetokea kipindi hiki cha walamba asali
 
Back
Top Bottom