Nyumba (Makazi) ya Mwl. Nyerere....

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Rais wa kwanza wa Tanzania,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,ameacha vitu vingi vya kukumbukwa ikiwa ni pamoja na nyumba yake ndogo(kwa umbo na thamani) iliyopo kijijini kwake Butiama.Hii ni kielelezo tosha.Imebeba maana kuwa Mwalimu hakupenda makuu na alitaka kufanana na wananchi wake.Marais waliomfuata nao waliapa kufuata nyayo za Mwalimu...
 
Mwenzetu hiyo 'title'! Duh! Mbona hukumalizia? Unataka tuchangie nini?
 
Katika uhai wake wengi walimuona Mwalimu kuwa msaliti wa tabaka lake (a traitor of his own class), kutokana na hulka yake ya kutotaka makuu, na vile vile kutokana na uwezo wake wa kusimamia kwa kauli na vitendo, imani yake kwamba hapa nchini kwake, hakuna yeyote atakayeruhusiwa kuishi kwenye utajiri wa kutupwa, kabla ya kukidhi mahitaji muimu ya wananchi wote. Kufuatia kifo chake wametokea manyang'au na kujigawia miongoni mwao rasilimali muimu zote za taifa huku wakiwaacha wananchi wengi wakitaabika,. Kila kuchao tabaka hili la walionacho linazidi kujiimarisha kwa kubuni sheria na mifumo ya kuwagandamiza wanyonge. Ni vigumu kufikiria ya kuwa wanyonge hao wanaweza kujikwamua kwenye minyororo hii bila msaada. Itabidi azaliwe msaliti mwingine wa tabaka lake, kutoka miongoni mwa hao wanaofaidika na mfumo wa sasa, ili kuongoza mapambano ya ukombozi wa pili. Kitendo cha uongozi wa chadema cha kuanza kuhoji uhalali wa tabaka hilo la walionacho, kujilundikia marupurupu ya aina mbali mbali, wakati wale wa kipato cha chini wakipwa mishahara ambayo haikidhi haja , ni ishara nzuri ya kuwa saa ya ukombozi imewadia
 
kha...umenishtuuuuuuuuuuuuuuaaaaaaaaaaaaaaaaaa.....kumbe wapi!!! hata baba yangu ana nyumba ndogo, but it doesnt necessarily mean ndo hukuiba! It could also mean, hukuweza kutumia pesa zako kuzalisha nyingine so as to have a nyumba kubwa uliyotaka..lol!
jus thinking aloud...
 
Ahahahahaaaaaaahhh!!! Hiyo Title....dah!!! Sina cha kuchangia....
 
Hii title imekaa kimtego tego...kwakua alikua na nyumba zaidi ya moja sitapenda kumsoma kitabia kupitia hiyo "nyumbandogo" yake unayoizungumzia
 
Sasa-sasa saa ya kwenda kwetu!
Sasa-sasa saa ya kwenda kwetu!

Mwalimu kwaheri eeh kwaheri!
Tunakwenda zetu nyumbani!
Mungu akipenda tutaonana kwaheriii eeeh!
 
Title jamani.....niliamini ni....hata hivo pouwa tu kama alikuwa nayo. Si binadamu bwana. Ila kweli alikuwa na nyumba Butiama tu! SIDANGANYIKI
 
Back
Top Bottom