BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Je, Nyumba alizonunua fisadi Mkapa nazo zimerudishwa? Wekeni hizo address za hizo nyumba ili tufanye uhakiki kama hii habari ina ukweli maana hii serikali haiaminiki hata kidogo.
Date::8/29/2008
Nyumba 128 zilizouzwa kinyemela zarejeshwa serikalini
Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi
SERIKALI imezirejesha nyumba zake 128 zilizouzwa kwa watu mbalimbali kinyume cha utaratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma zikiwemo zilizopo kwenye maeneo maeneo nyeti nchini kote.
Hatua hiyo ilitangazwa bungeni na Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa jana na kusema kuwa nyumba hizo zinarudishwa serikalini na wahusuika kurudishiwa fedha zao.
Miongoni mwa nyumba zilizorejeshwa serikalini ni ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Raia, Harith Bakari Mwapachu na za viogogo wengine akiwamo Jaji Stephen Ihema na Balozi Adam Marwa ambao waliuziwa nyumba za Halmashauri ya Kinondoni.
Waziri Kawambwa, alisema, wakati wa utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba nyumba zote za serikali zilizouzwa kinyume cha utaratibu zirejeshwe.
Dk Kwambwa alitaja makundi hayo kuwa ni pamoja na nyumba zilizopo katika makambi, nyumba
ziliozouzwa kwa watumishi binafsi ambao si watumishi wa serikali na watumishi wa umma na nyumba zaidi ya moja zilizouzwa kwa familia moja ya watumishi wa umma.
Nyigine ni nyumba za taasisi mbalimbali zilizouzwa kwa watumishi wa serikali kuu na zilizoko katika maeneo nyeti ya serikali na ambazo ziliuzwa kwa watumishi wa umma.
Waziri Kawambwa alisema, nyumba 52 zilizopo katika makambi ziliuzwa kwa makosa, idadi hiyo ikihusisha nyumba nane zilizoko katika maeneo ya makambi ya polisi, nyumba 10 za maeneo ya Magereza na nyumba 34 katika maeneo ya Hospitali.
Alisema wahusika wote wameandikiwa barua ya kusitisha mikataba na kuwataka wasiziendeleze kuzikarabati kwa kuwa serikali inafanya utaratibu wa
kukagua na kutathmini maendelezo yaliyofanywa na wahusika ili kupata thamani halisi kwa ajili ya kuwafidia .
Alisema wakati wa kuuza nyumba za serikali pia ilibainika kuwa nyumba nne ziliuzwa kimakosa kwa watu ambao si watumishi wa serikali jijini Dar es Salaam, baada ya wahusika kutoa taarifa zisizokuwa sahihi.
Katika hatua za kurekebisha kasoro hiyo, serikali imefuta mikataba yote ya mauzo ya nyumba hizo na nyumba tatu kati ya nne tayari zimerejeshwa kwenye miliki ya serikali na nyumba moja iliyobaki, muhusika amefungua kesi Mahakama Rufaa ya ardhi, alisema.
Alisema kasoro nyingine iliyojitokeza wakati wa zoezi hilo ni baadhi ya familia na watumishi wa umma waliuziwa nyumba zaidi ya moja na kwamba uchunguzi uliofanywa na serikali umebaini kuwa kuna familia sita na watumishi wanne waliuziwa nyumba zaidi ya moja.
Alisema kati ya familia sita zilizouziwa nyumba zaidi ya moja, tano zimerudisha nyumba tano na kubakiwa na nyumba tano badala ya 10 kama ilivyokuwa awali na kwa upande wa watumishi wanne serikali imetoa muda hadi Septemba 15 mwaka huu kwa wahusika kurejesha nyumba za ziada na kubakiwa na nyumba moja.
Alisema pia serikali iligundua kuwa nyumba 27 zilizokuwa za serikali kuu ziliuzwa kwa watumishi wa umma, nyumba hizo ni pamoja na na nyumba 21 za serikali za mitaa, nyumba mbili za Shirika la Viwanda vidogo (Sido), nyumba moja ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na nyumba tatu za Shirika la Nyumba la Taifa.
Waziri Kawambwa alisema jumla ya nyumba 35 zilizouzwa zipo katika maeneo nyeti ya serikali na ambazo hazikupaswa kuuzwa kutokana na unyeti wa kazi za watumishi wanaostahili kuzitumia.
Alisema serikali kupitia Wizara yake imeorodhesha nyumba za namna hiyo na waliouziwa wote wameandikiwa barua za kusitisha mikataba yao ili kuzirejesha nyumba hzio kwa matumizi ya serikali kwa mantiki hiyo numba za namna hiyo hazitauzwa tena.
Katika zoezi hilo la uuzwaji wa nyumba jumla ya Sh bilioni 38.69 zilikusanywa katika kipindi cha miaka mitano hadi mwezi Juni mwaka huu kati y ash bilioni 57.05 ikiwa ni sawa na asilimia 67.81 zinazotarajiwa kukusanywa katika kipindi cha miaka kumi kutokana na mauzo ya nyumba 7,159.
Azimio hilo la Bunge linafuatia hoja binafsi ya uuzwaji wa nyumba za serikali iliyowasilishwa bungeni katika mkutano wake 11 uliofanyika Aprili mwaka huu na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro.