Nyumba 128 zilizouzwa kinyemela zarejeshwa serikalini

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,004
Je, Nyumba alizonunua fisadi Mkapa nazo zimerudishwa? Wekeni hizo address za hizo nyumba ili tufanye uhakiki kama hii habari ina ukweli maana hii serikali haiaminiki hata kidogo.

Date::8/29/2008
Nyumba 128 zilizouzwa kinyemela zarejeshwa serikalini
Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi

SERIKALI imezirejesha nyumba zake 128 zilizouzwa kwa watu mbalimbali kinyume cha utaratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma zikiwemo zilizopo kwenye maeneo maeneo nyeti nchini kote.

Hatua hiyo ilitangazwa bungeni na Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa jana na kusema kuwa nyumba hizo zinarudishwa serikalini na wahusuika kurudishiwa fedha zao.

Miongoni mwa nyumba zilizorejeshwa serikalini ni ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Raia, Harith Bakari Mwapachu na za viogogo wengine akiwamo Jaji Stephen Ihema na Balozi Adam Marwa ambao waliuziwa nyumba za Halmashauri ya Kinondoni.

Waziri Kawambwa, alisema, wakati wa utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba nyumba zote za serikali zilizouzwa kinyume cha utaratibu zirejeshwe.

Dk Kwambwa alitaja makundi hayo kuwa ni pamoja na nyumba zilizopo katika makambi, nyumba

ziliozouzwa kwa watumishi binafsi ambao si watumishi wa serikali na watumishi wa umma na nyumba zaidi ya moja zilizouzwa kwa familia moja ya watumishi wa umma.

Nyigine ni nyumba za taasisi mbalimbali zilizouzwa kwa watumishi wa serikali kuu na zilizoko katika maeneo nyeti ya serikali na ambazo ziliuzwa kwa watumishi wa umma.

Waziri Kawambwa alisema, nyumba 52 zilizopo katika makambi ziliuzwa kwa makosa, idadi hiyo ikihusisha nyumba nane zilizoko katika maeneo ya makambi ya polisi, nyumba 10 za maeneo ya Magereza na nyumba 34 katika maeneo ya Hospitali.

Alisema wahusika wote wameandikiwa barua ya kusitisha mikataba na kuwataka wasiziendeleze kuzikarabati kwa kuwa serikali inafanya utaratibu wa
kukagua na kutathmini maendelezo yaliyofanywa na wahusika ili kupata thamani halisi kwa ajili ya kuwafidia .

Alisema wakati wa kuuza nyumba za serikali pia ilibainika kuwa nyumba nne ziliuzwa kimakosa kwa watu ambao si watumishi wa serikali jijini Dar es Salaam, baada ya wahusika kutoa taarifa zisizokuwa sahihi.

“Katika hatua za kurekebisha kasoro hiyo, serikali imefuta mikataba yote ya mauzo ya nyumba hizo na nyumba tatu kati ya nne tayari zimerejeshwa kwenye miliki ya serikali na nyumba moja iliyobaki, muhusika amefungua kesi Mahakama Rufaa ya ardhi,” alisema.

Alisema kasoro nyingine iliyojitokeza wakati wa zoezi hilo ni baadhi ya familia na watumishi wa umma waliuziwa nyumba zaidi ya moja na kwamba uchunguzi uliofanywa na serikali umebaini kuwa kuna familia sita na watumishi wanne waliuziwa nyumba zaidi ya moja.

Alisema kati ya familia sita zilizouziwa nyumba zaidi ya moja, tano zimerudisha nyumba tano na kubakiwa na nyumba tano badala ya 10 kama ilivyokuwa awali na kwa upande wa watumishi wanne serikali imetoa muda hadi Septemba 15 mwaka huu kwa wahusika kurejesha nyumba za ziada na kubakiwa na nyumba moja.

Alisema pia serikali iligundua kuwa nyumba 27 zilizokuwa za serikali kuu ziliuzwa kwa watumishi wa umma, nyumba hizo ni pamoja na na nyumba 21 za serikali za mitaa, nyumba mbili za Shirika la Viwanda vidogo (Sido), nyumba moja ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na nyumba tatu za Shirika la Nyumba la Taifa.

Waziri Kawambwa alisema jumla ya nyumba 35 zilizouzwa zipo katika maeneo nyeti ya serikali na ambazo hazikupaswa kuuzwa kutokana na unyeti wa kazi za watumishi wanaostahili kuzitumia.

Alisema serikali kupitia Wizara yake imeorodhesha nyumba za namna hiyo na waliouziwa wote wameandikiwa barua za kusitisha mikataba yao ili kuzirejesha nyumba hzio kwa matumizi ya serikali kwa mantiki hiyo numba za namna hiyo hazitauzwa tena.

Katika zoezi hilo la uuzwaji wa nyumba jumla ya Sh bilioni 38.69 zilikusanywa katika kipindi cha miaka mitano hadi mwezi Juni mwaka huu kati y ash bilioni 57.05 ikiwa ni sawa na asilimia 67.81 zinazotarajiwa kukusanywa katika kipindi cha miaka kumi kutokana na mauzo ya nyumba 7,159.

Azimio hilo la Bunge linafuatia hoja binafsi ya uuzwaji wa nyumba za serikali iliyowasilishwa bungeni katika mkutano wake 11 uliofanyika Aprili mwaka huu na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro.
 
duuh,

afadhali na wao waende waishi uswahilini walau itasaidia kuboresha maisha na miundombinu uswahilini....!

Haiwezikani kila mtu kukaa masaki na oysterbay...!
 
tuliambiwa nyumba zitarudishwa lakini hatukuamini. Muhimu ni zote za masaki upanga na osterbay zirudishwe. Kwani zile kota za mawaziri pale masaki hazifai kwa waziri kuishi pale labda naibu. Nyumba ziliuzwa milioni 22 kweli si zuluma hizo kwa walala hoi wanaoishi uswahilini.
 
watazimiliki tena mafisadi wengine au wenyewe kwa wenyewe ... naona kama danganya toto tu .. wale ambao wako kwenye system ni just a small matter kufanya ujanja ... maana mpaka upekue mafaili yao ndiyo ujue it will be too late
 
Zimerudishwaje? Waliouziwa wamerudishiwa fedha kiasi gani? Zile walitoa kununua au na riba na fidia ya usumbufu? Isije ikwa tunafanya biashara kichaa, kuuza nyumba kwa bei ya chee halafu kuirejesha kwa zaidi ya fedha tulizouzia.
Naona kuna mmoja kaamua kwenda mahakamani, serikali itaingia gharama kubwa katika maamuzi haya na hata uamuzi wa kurejesha nyumba hizi utakuwa na gharama kubwa sana
 
Hii ndiyo Tanzania bwana:

Rais alisema angerudisha nyumba ambazo zimeuzwa kimakosa yaani kuuza nyumba ya OCD for example iliyoko kwenye karibu na ofisi ya OCD.

Hakusema anarudisha nyumba zote... that's what exactly done. Sasa munaanza kuongea upupu tena.
 
Kinachonipa wasiwasi ni kauli ya waziri kuwa watalipa fidia kwa wale ambao wamefanya renovations ya hizo nyumba. Mfano nimenunua nyumba millioni 20, nikafanya renovation ya millioni 100, je serikali itanilipa milioni 120? Watajuaje renovation yangu ilikuwa ya millioni 100?
 
Kinachonipa wasiwasi ni kauli ya waziri kuwa watalipa fidia kwa wale ambao wamefanya renovations ya hizo nyumba. Mfano nimenunua nyumba millioni 20, nikafanya renovation ya millioni 100, je serikali itanilipa milioni 120? Watajuaje renovation yangu ilikuwa ya millioni 100?

Hapo hapo yaani mimi kichwa kimeanza kuniuma sasa....walipwe fidia ya nini??Hivi police akifanya renovation kwenye kota anayo ishi akiamishwa iwa analipwa???Hapo sasa watu watalipana mihela mimilioni balaa watu watatajilika UFISADI mwingine huu sasa unanukia.....sijui tunataka kufanya nini hapa sasa na wengi wao hawajalipa pesa walizo nunua nyumba hizo lakini vitafanyika viini macho hapo balaaa...watu wataongeza wake kwa ajili ya dili hili sasa.
 
Hivi hao kina Mwapachu na wenzie mnafikiri wamenyang'anywa tu bila ya kupewa nyumba zingine sehemu muafaka? I doubt it...
 
Ziliuzwa kimakosa?

Kuna mazingira ya Rushwa na Ufisadi katika hili.
Mtu asiye mtumishi wa serikali kuuziwa nyumba zilizo walenga watumishi wa serikali ni dalilili moja kubwa ionyeshayo kwamba Rushwa ilipokelewa au Ufisadi ulitumika.

Hayo maeneo nyeti ya serikali yalianza kuwa maeneo nyeti baada ya nyumba kuuzwa?
Hii inaonyesha kwamba hata nyumba ndani ya Ikulu ingeweza kuuzwa kwa mfanyibiashara mwenye michuzi au mtu mwenye nasaba na wauzaji?

Serikali yetu imeonyesha dharau kubwa sana kwa kushindwa kwake kuheshimu vyombo vya dola kama Polisi na Magereza.

Kuna kundi kubwa la watumishi wa serikali wanaostahili kufukuzwa kazi mara moja.

Serikali haiwezi kuendelea kupamba na kujishauashaua mbele ya watumishi wake wanao kiuka taratibu kanuni na sheria kwa namna yeyote, kwani kitendo hicho ni sawa na mkulima kucheka na kima shambani mwake.

Upuuzi huu wa serikali na watumishi wake kulegea kama machoko utaisha lini???!!!
 
Vigogo waanza kunyang'anywa nyumba

na Salehe Mohamed, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SERIKALI imeanza kuzirejesha katika mikono baadhi ya nyumba zake zilizouzwa kwa watumishi wa umma na Serikali ya Awamu ya Tatu.

Hatua hiyo ya serikali imesababisha kuwepo hali ya wasiwasi miongoni mwa maofisa wake wa juu, hasa baada ya baadhi ya waliokuwa mawaziri na viongozi wengine wa juu serikalini kujikuta wakinyang'anywa nyumba zao.

Baadhi ya vigogo walikwishanyang'anywa nyumba hizo ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, Jaji Stephen Ihema na Balozi Adam Marwa, waliouziwa nyumba hizo na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Taarifa ya kuanza kurejeshwa kwa nyumba hizo ilifahamika jana wakati Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, akisoma utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali kinyume cha utaratibu.

Dk. Kawambwa alisema uamuzi huo wa serikali umekuja baada ya kubainika kwamba nyumba zake 128 ziliuzwa kimakosa na kwa watu wasiostahili kuuziwa nyumba hizo zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini, na kwamba uamuzi wa kuzirejeshwa nyumba hizo umefanyika kwa kuzingatia sheria za nchi.

Dk. Kawambwa, alifafanua kwamba baadhi ya nyumba serikali ziliuzwa kimakosa kwa watumishi wasio wa serikali huku ikifahamika kuwa hazikupaswa kuuzwa. Nyumba hizo ni pamoja na zilizo katika maeneo ya utawala wa serikali.

Katika urejeshaji huo unaohusisha makundi matano, nyumba zilizokusudiwa kurejeshwa katika mikono ya serikali ni zile zilizo katika makambi, zilizouzwa kwa wasiokuwa watumishi wa serikali, na watumishi wa familia moja walionunua nyumba zaidi ya moja.

Kundi jingine ni wale walionunua nyumba za taasisi mbalimbali zilizouzwa kwa watumishi wa Serikali Kuu na nyumba zilizo katika maeneo nyeti ya serikali na ambazo ziliuzwa kwa watumishi wa umma.

Alizitaja baadhi ya nyumba zilizouzwa kimakosa kuwa ni pamoja na 52 zilizo kwenye makambi, zikiwemo nane zilizo katika makambi ya polisi, nyumba 10 zilizo maeneo ya magereza na nyumba 34 zilizo katika maeneo ya hospitali.

Dk. Kawambwa alisema serikali imesitisha mikataba ya nyumba hizo na wahusika wameandikiwa barua kuarifiwa jambo hilo pamoja na kuwaarifu wasiziendeleze zaidi nyumba hizo.

"Tumesitisha mikataba yao lakini pia tumewataarifu wasiziendeleze, wakati huo huo sisi tunafanya tathmini ya maendelezo waliyoyafanya ili kuwafidia," alisema Dk. Kawambwa.

Aidha, alieleza kuwa nyumba nne zilibainika kuuzwa kimakosa kwa watu ambao si watumishi wa serikali jijini Dar es Salaam, baada ya wahusika kutoa taarifa zisizokuwa sahihi.

Kati ya nyumba hizo, tatu zimesharejeshwa serikalini na moja iliyobaki aliyeinunua amefungua kesi Mahakama ya Ardhi.

Dk. Kawambwa, pia aliwataja watu wanne ambao wameuziwa nyumba huku wakiwa si watumishi wa serikali kuwa ni Ester Chilambo, mfanyakazi wa Radio Tumaini, Mussa Joseph, mfanyakazi wa ujenzi, Monica Senga, mfanyakazi wa DAHACO na Stanley Manongi, mfanyakazi wa ujenzi.

Aidha serikali iligundua kuwa nyumba 27 zilizokuwa za Serikali Kuu ziliuzwa kwa watumishi wa umma.

Nyumba hizo ni pamoja na nyumba 21 za Serikali za Mitaa, nyumba mbili za Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), nyumba moja ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na nyumba tatu za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Uuzwaji wa nyumba za serikali uliingizia serikali jumla ya sh bilioni 38.69 katika kipindi cha miaka mitano, hadi Juni mwaka huu kati ya sh bilioni 57.05 zilitarajiwa kukusanywa.

Kiasi hicho ni sawa na asilimia 67.81 ya zinazotarajiwa kukusanywa katika kipindi cha miaka kumi kutokana na mauzo ya nyumba 7,159.

Kurejeshwa kwa baadhi ya nyumba kulitokana na azimio hilo la Bunge lililopitishwa baada ya kutolewa kwa hoja binafsi ya uuzwaji wa nyumba za serikali iliyowasilishwa bungeni katika mkutano wa 11 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uliomalizika mjini hapa mwezi Aprili mwaka huu.

Hoja ya kurejeshwa kwa nyumba hizo ilitolewa bungeni na Mbunge wa Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro.
 
Kinachonipa wasiwasi ni kauli ya waziri kuwa watalipa fidia kwa wale ambao wamefanya renovations ya hizo nyumba. Mfano nimenunua nyumba millioni 20, nikafanya renovation ya millioni 100, je serikali itanilipa milioni 120? Watajuaje renovation yangu ilikuwa ya millioni 100?

Ndugu,

Kama umeuzia nyumba kwa mkataba halali ulio-be-registered say mahakamani...

Mtu/Serikali haiwezi kukuondoa hivi hivi... infact sheria ya Ardhi hairuhusu hivyo..

Tuwe pia tunaelewa... nyumba zinazorudishwa ni wale walio uziwa nyumba kwenye maeneo ambao si sawa kwa usalama wa Taifa...

Lakini otherwise... nyumba zingine zote wafanyakazi wa Serikali waliouziwa wanatakiwa waendelee na kujenda mabanda yao ya nguruwe na ng'ombe, na vibanda vya chips kuku... kama walivyopanga.

Serikali haina mpango wa kurudisha nyumba zote zilizouzwa... mambo hayo yameshaisha.
 
jamani hili ni changa la macho jingine, ukifuatilia unaweza kubaini kuwa fidia inayolipwa ni mara tisa na kiwango cha fedha ambacho mtu alitoa kununulia nyumba
 
..uuzaji wenyewe ulikuwa makajanja.

..sasa katika kuzirejesha watalipa market value ya nyumba na kiwanja au???
 
Mwandishi Wetu, Dodoma
Daily News; Saturday,August 30, 2008 @10:38

SERIKALI imeagiza kufutwa kwa mikataba na kurudishwa kwa nyumba kadhaa ilizowauzia maofisa wake waandamizi na watu binafsi, baada ya kubainika kwamba waliuziwa kinyume cha sheria au katika sehemu zisizostahili, ilifahamika bungeni jana.

Imebainika pia kwamba Waziri mmoja mstaafu, Jaji na balozi mmoja waliuziwa nyumba ambazo si za Serikali Kuu na sasa itabidi zijengwe mpya na kufidiwa kwa wamiliki wa awali.

Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, aliliambia hayo Bunge jana kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge la Uuzaji wa Nyumba za Serikali yaliyotokana na hoja binafsi iliyowasilishwa na Aloyce Kimaro (Vunjo-CCM), Aprili mwaka huu.

Katika maazimio hayo, wabunge walitaka serikali itekeleze agizo la Rais la kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha utaratibu; itoe orodha ya nyumba zilizouzwa kwa watu ambao si watumishi wa serikali na ambazo hazikupaswa kuuzwa kutokana na unyeti wa wanaostahili kuzitumia.

Katika kueleza namna serikali ilivyotekeleza maazimio hayo, Waziri Kawambwa aliwaambia wabunge kwamba imebainika kuwa kuna makundi matano ya nyumba za serikali zilizouzwa kinyume cha taratibu ambazo ni zilizoko kwenye makambi; zilizouzwa kwa watu binafsi na nyumba zaidi ya moja zilizouzwa kwa familia moja.

Nyingine ni nyumba za taasisi mbalimbali zilizouzwa kwa watumishi wa Serikali Kuu na ambazo ziko katika maeneo nyeti zilizouzwa kwa watumishi wa umma.

Kwa mujibu wa Kawambwa nyumba 52 ziliuzwa kwa makosa katika makambi, kati yake nane ziko katika makambi wa Polisi, 10 katika makambi ya Magereza na 34 katika maeneo ya hospitali.

Alisema Serikali inakagua na kutathmini maendeleo yaliyofanywa kwa lengo la kupata thamani halisi zitakazokuwa msingi wa kuwafidia wahusika.

Juu ya nyumba za taasisi mbalimbali zilizouzwa, Waziri Kawambwa alisema zilifikia 27, zikiwamo 21 za Serikali za Mitaa, mbili za Shirika la Viwanda Vidogo (Sido), moja ya Mamlaka ya Mapato (TRA) na tatu za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Waziri Kawambwa alisema serikali itajenga nyumba mbadala kufidia nyumba zilizouzwa.

Miongoni wa waliouziwa nyumba hizo kwa mujibu wa kiambatanisho kilichowasilishwa bungeni, ni Waziri mstaafu Bakari Mwapachu, Jaji Stephen Ihema na Balozi Adam Marwa. Hao waliuziwa nyumba za Serikali za Mitaa.

Dk. Kawambwa aliwaambia wabunge kwamba nyumba nne ziliuzwa kwa makosa kwa watu ambao si watumishi wa serikali mjini Dar es Salaam baada ya kutoa taarifa zisizo sahihi. Alisema serikali imefuta mikataba ya mauzo ya nyumba tatu kati ya hizo na moja mhusika amefungua kesi mahakamani.

Kwa mujibu wa viambatanisho vilivyowasilishwa bungeni, miongoni mwa waliouziwa nyumba hizo ni Esther Chilambo katika eneo la Karume; Monica Senga katika eneo la Upanga, Mussa Joseph na Stanley Manongi, wote katika eneo la Ubungo Camp.

Kuhusu familia sita na watumishi wanne waliouziwa nyumba zaidi ya moja, alisema familia tano zimerudisha nyumba tano na kubakiwa na tano wakati watumishi hao wanne wamepewa hadi Septemba 15 kurejesha nyumba ya ziada vinginevyo serikali itafuta mkataba wa nyumba mojawapo.

Kiambatanisho kinaonyesha wahusika walikuwa familia ya Balozi Ben Moses na Dk. Edna Moses (Mambo ya Nje na Afya); Hussein Abdulrahman na Mwanamtama Marandu (Shirika la Reli na Elimu), Emil Kayega na Emerensiana Kayega (Ofisi ya Makamu wa Rais na Ardhi na Makazi), Clement na Esther Mshana (TVT na RTD).

Wengine ni Dk. Mollel Jacob na Theodora Mollel (Mifugo na Ofisi ya Rais Utumishi) na Ngore Kondo na Zainab Kondo (Ofisi ya Rais).

Watumishi waliouziwa nyumba mbili ni Dk. Edna Moses wa Afya, Veronica Mabula wa Bohari Kuu (Mwanza), Sweetbert Bajuza wa DAS (Karagwe) na Agnes Chamshama wa Halmashauri ya Wilaya Lushoto.

Alibainisha zaidi kuwa nyumba 35 zilizouzwa katika maeneo nyeti waliouziwa wameandikiwa barua za kusimamisha mikataba na kuzirejesha serikalini.

Takwimu zilizowasilishwa na Waziri Kawambwa kwa Bunge zinaonyesha kuwa hadi Juni mwaka huu serikali ilikuwa imeuza nyumba 7,159 na ilikuwa imepata Sh bilioni 38.6 kutokana na mauzo hayo kati ya lengo la Sh bilioni 57.

Source: Habari Leo
 
Balozi Ben Moses na Dk. Edna Moses. Hawa ni mtu na mke wake, kama sikosei Ben Moses ni balozi Sweden na inasemekana wameoa nyumba moja na Mkapa.
 
naombeni kujua, yaani kwa kifupi nyumba zote zinarudi? na za mashirika ya umma pia???

Bado kuna utata katika hili swala la nyumba. Wangetwambia ni nyumba ngapi za serikali na mashirika ya umma zilizouzwa ili tujue kama hizo zilirudishwa serikalini ni asilimia ngapi ya nyumba zilizouzwa.

Kuna uwezekano kabisa hizo 128 zilizorudishwa ni aslimia ndogo sana ya nyumba zilizouzwa. Mkapa inasemekana alinunua nyumba tatu je naye karudisha? Magufuli naye aliyevalia njuga swala la kuuza nyumba karudisha ngapi? Majina yaliyowekwa hadharani ni machache mno ukilinganisha na nyumba zilizorudishwa.
 
Bado kuna utata katika hili swala la nyumba. Wangetwambia ni nyumba ngapi za serikali na mashirika ya umma zilizouzwa ili tujue kama hizo zilirudishwa serikalini ni asilimia ngapi ya nyumba zilizouzwa.

Kuna uwezekano kabisa hizo 128 zilizorudishwa ni aslimia ndogo sana ya nyumba zilizouzwa. Mkapa inasemekana alinunua nyumba tatu je naye karudisha? Magufuli naye aliyevalia njuga swala la kuuza nyumba karudisha ngapi? Majina yaliyowekwa hadharani ni machache mno ukilinganisha na nyumba zilizorudishwa.

Asante sana, pls keep on informing us
 
naombeni kujua, yaani kwa kifupi nyumba zote zinarudi? na za mashirika ya umma pia???

Waheshimiwa Mbona hamsomi mkaelewa.

Scope ya hii project ni Nyumba za Serikali Kuu tu... kwa maana nyingine zilizokuwa chini ya wizara ya Miundo Mbinu. in other words zilizokuwa chini ya TBA (Tanzania building Agency)

Mashirilka ya Umma ni independent entity...hazihusiki!!!

Hivi mna matatizo gani hamuelewi vitu virahisi kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom