Nyota wa Hollywood kuja Tanzania

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
thursday, may 28, 2009

Nyota wa Sinema wa Marekani wataka
kutengeneza filamu zao katika Tanzania
. Wawakilisha mapendekezo kwa Rais Kikwete

Na Mwandishi Maalum
KUNDI la wachezaji sinema maarufu wa Marekani limewasilisha mapendekezo yake kwa Serikali ya Tanzania wakitaka kufungua shughuli zao za kutengeneza sinema katika Tanzania.​

Kundi hilo, chini ya kampuni ya The Bridge, liliwasilisha maombi hayo wakati mchezaji na mtengenezaji sinema maarufu, Bill (William) Zane alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Bill Zane ni kiongozi mshirika wa The Bridge.​

Rais Kikwete alikutana na mchezaji sinema huyo mjini Los Angeles wakati kiongozi huyo wa Tanzania alipokuwa kwenye mji huo kupokea tunzo maalum kutoka kwa kundi la US Doctors for Africa wakati wa ziara yake katika Marekani.
Tuzo hilo linatambua mchango wa Rais Kikwete na Serikali yake katika kuendeleza shughuli za afya katika Tanzania na Afrika. Rais alirejea nchini mwanzoni mwa wiki hii baada ya kumaliza ziara hiyo.​

Jiji la Los Angeles ndilo maarufu zaidi kwa uchezaji na utengenezaji wa filamu katika Marekani na duniani pote katika eneo maarufu la jiji hilo la Hollywood.
Akiwasilisha maombi yake kwa Rais, Zane alisema kuwa Tanzania inayo mazingira ya kuvutia ya kuchezea na kutengenezea filamu ikiwa ni pamoja na Visiwa vya Zanzibar na Pemba, fukwe za kuvutia za bahari, misitu mikubwa, theluji juu ya Mlima Kilimanjaro, mbunga za wanyama na maziwa makubwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.​

Miongoni mwa sinema ambazo Zane ameshiriki kama mtengenezaji ama mchezaji ni pamoja na Back to the Future, Critters, Dead Calm, Cleopatra na The Phantom.
Chini ya mapendekezo hayo, nyota hao wa sinema wa Marekani wanakusudia kuanzisha "Tanzania Studios" na wanapenda Serikali ya Rais Kikwete kuwaunga mkono kufanikisha jambo hilo ikiwa ni pamoja na Serikali kutoka eneo kwa ajili ya kuanzisha studio hizo.​

Uchezaji na utengenezaji sinema ni moja ya shughuli kubwa na zenye fedha nyingi katika Marekani. Inakadiriwa kuwa utengenezaji wa sinema moja unagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 200 na kuchukua wastani wa miezi 16 kukamilika.​

Kwa mujibu wa wachezaji sinema hao, kiasi cha watanzania kati ya 300 na 400 watanufaika moja kwa moja kwa kushiriki kwa namna moja ama nyingine katika utengenezaji wa sinema moja.​

Katika Afrika, ni Afrika Kusini pekee yenye studio za kisasa kwa ajili ya uchezaji na utengenezaji wa sinema.​

Mbali na kupokea mapendekezo hayo ya kundi hilo, Rais Kikwete pia aliahidiwa mambo mbali ya kuisaidia Tanzania kijamii na wachezaji sinema nyota wengine ambao wameonyesha nia ya kusaidia maendeleo ya Tanzania.​

Ahadi hizo zilitolewa wakati kundi la wachezaji sinema maarufu na matajiri wengine walipomwandalia chakula cha usiku Rais Kikwete mjini Los Angeles.​

DSC_7746.jpg

Rais Kikwete akitembelea maeneo ya ya studio za Sony Picures wakati wa ziara yake ya Marekani katika jimbo la California
DSC_8033.jpg

Mhe Rais akiwa mchezaji mwingine maarufu wa sinema Steve Seagal wakati wa hafla ya chakula cha jioni ambako taasisi ya US Doctors for Africa ilimwandalia Rais Jakaya Kikwete mjini Los Angeles wakati wa ziara yake katika Marekani

http://mawasilianoikulu.blogspot.com/2009/05/nyota-wa-hollywood-wapania-kuja.html

wapi hii mambo, AU ndo yale yale??
 
Duuu prezooo wetu nomaa..... ana project ya kuleta wahandisi wa kujenga clubs an casino za ukweli hapa bongo, wacha wewe JK ni sooo !! itakua hakuna kulala !!
 
Yaani hichi nacho ni kitu cha Rais kushughilikia?
Si kuna baraza la sanaa? Kwa nini asiwaelekeze hao akina Zane huko?
Yaani every Tom, Dick and Harry can just get the attention of our President as long as they are American?
 
afadhali hata hii ya merikano kuliko ile ya jana akipokea yeboyebo kutoka china na vitu vingine vya thamani ya shilingi millioni hamsini... it was pathetic kabisa
 
Rais ameona kila kitu afanye mwenyewe maana bongo hadi wanaohusika na sanaa wamelala wameconcentrate kwenye bongo movies kusema "pumbavuuuuuuu" na kuvaa makoti mazito dar pamoja na lilee joto, au mtu anavaa shati nyekundua naingia kwny gari akishuka anakua na shati nyingine, na jambazi anayevua viatu anaingia kwenye nyumba ya vigae. hahaha kweli tu ahitaji msaada, Movie kama District 9 ya South Africa ina CGI za hollywod kabisa, very well made, ila bongo nani atainvest $100M kwenye movie, haha! we need help utake usitake, kama kweli unataka kutoka kwenye hii industry afu still inabidi tu kutumia ngeli... usiseme tuige wahindi maana wao soko lao linajitoshelezea, wako bilioni nchini kwao, swahili speakin countries wako wangapi? afu hata theatres za kuhesabu hata mia hazifiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom