Nyoka, alama ya Uungu (Ukombozi) au Ushetani (Upotofu)?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,373
Na DaVinci XV

SEHEMU YA I

4FD1D3C5-E19E-441B-8F6B-9DA3A6819BD9.jpeg

Masal kheyr wakuu,

MWANZO 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.

Binafsi tangu ningali mdogo nilikuwa na tatizo la Ophidio-Phobia (Fear of Snake) kikawaida mwanadamu yoyote anaweza kuwa na Uwoga juu ya nyoka ila ule uoga uliopitiliza juu ya kiumbe hicho ndio huitwa Ophidio-Phobia. Sikumbuki hili tatizo lilianzia wapi na kwenye tukio gani, japo Ubongo wangu ulikuwa unanisukuma kuamini vitu viwili ambavyo nadhani vilikuwa vichochezi vya hii kadhia niliyo nayo.

Mosi, Ni Movies ambazo zilihusisha kiumbe huyu kushambulia wanaadamu movie kama Anaconda na nyinginezo pengine ndizo zilichagiza mimi kwa kiasi kikubwa kuwa na mtazamo wa kuogofya juu ya kiumbe huyu, Lakini Pili ,Bibi yangu kipenzi ambaye pia alikuwa mlezi wangu alipoteza uhai kwa kuumwa na Kiumbe huyu ningali bado mdogo hivyo sikuwa na uhakika wa moja kwa moja juu ya phobia yangu imetokana na nini kati ya hivyo viwili.

018E12D5-3B8F-4FCB-985D-2A66293238CB.jpeg

Kadri nilivyozidi kukua ndivyo phobia yangu iliposhuka kwasababu nlitamani kumjua kiundani kiumbe huyu na kwanini nlikuwa na uoga nae usiomithilika kiu ya Kumsoma ikanijaa kadri nilivyozidi kukata miaka kujongea Utu uzima.

Rasmi nikaingia kwenye dimbwi la kumsoma kiumbe huyu kidini, kimazingira na hata kisayansi halafu mwishowe akabadilika kutoka kwenye kumuogopa hadi kuwa miongoni mwa Viumbe pendwa ninaovutiwa nao, kama ilivyo kwa mtu mwingine yoyote kuvutiwa na Mnyama Simba au Hata Chui, nami ilitokea Sana kumhusudu Nyoka kwa namna alivyo na mwenendo wake kama ningekuwa Msanii mwenye A.K.A za wanyama Basi ningejiita Nyoka 😅😅😅.

Nlitembelea karibuu zoo nyingi zinazotunza wanyama hawa na kujifunza aina tofauti tofauti za viumbe hawa ukiachana na kupitia majarida na facts mbalimbali kuwahusu.

Si mnakumbuka namna Mungu alivyomtumia nyoka katika visa tofauti tofauti ikiwemo pale Misri kwa Musa na Wachawi wa Firauni.

Lakini pia si mnakumbuka Nyoka alivyotumika na Ibilisi kumhadaa Mama yetu Hawa kule bustanini Eden, na Kwenye baadhi ya Mandiko nyoka akabaki kitendawili atasimama Upande upi wema au Ubaya.

Kwani ninyi hamkumbuki vita iliyowekwa kati ya kiumbe huyu na mwanadamu kwenye maandiko popote wakutanapo?

84EF4BE4-5330-4549-B6E4-35E881EDE941.jpeg

Nyoka akanenwa kwa Ubaya sehemu nyingi sana. Na kutokana na maandiko hayo ya mwanzo ambayo Mwanaadamu akikutana na Nyoka basi kinachofata ni vita haijalishi kiumbe huyo alikuwa anataka kudhuru au yupo katika Eneo lake.

B3084C0A-C22D-48B1-934D-B0CD4FA1ADC9.jpeg

Na si mnakumbuka Pale zamani wazee walipotuhadithia mengi sana kuhusu kiumbe huyu wakatutisha kwamba ukiota ndoto za Nyoka basi majini wanakuwa wanashughulika nawe kwa namna moja au nyingine,

Mungu alimuumba nyoka kwa namna ya tofauti sana na kumpa uwezo wa kipekee mno, si unafahamu ya kwamba nyoka kila muda huzaliwa upya pale anapojivua gamba na hii imefanya wengi kuamini kwamba nyoka huwa hawazeeki,na hii ndio kielelezo cha jamii nyingine kumtumia nyoka kama alama ya kuzaliwa upya.

Tukamuona Nyoka katika nembo nyingi sana ikiwemo kwenye Tiba na Afya mahospitalini, waganga wa jadi , Mahekalu na Madhabau, Vikundi vya siri , pete na mikufu ya Watu wakubwa, makanisa, mashirika makubwa makubwa duniani na Logo tofauti tofauti.

Na wengi wakahitimisha kwamba mashirika hayo yapo chini ya Shetani pengine kwasababu tu Alama ya nyoka katika nembo Bila kufahamu haswa chanzo chake ni nini.

312D72B7-D7E9-4DB1-8AF4-CF991F20737B.png

Kuna karibu species zaidi ya 3000 za nyoka na karibu species 600 tu ndio nyoka wenye Sumu duniani. Nyoka huishi sehemu tofauti ikiwemo kwenye mchanga, Majangwa, Mapango na Miamba mikubwa, kwenye Maji, vichaka na nyasi ndefu na kuna wanaoishi kwenye miti mirefu.

Nyoka wengi hula Mijusi, Ndege, vyura na Wadudu wengine wadogowadogo.

MTAZAMO WA NYOKA KULINGANA NA JAMII ZA KALE
Huko misri ya kale ambapo dunia ya sasa kuna wanaomini, ilikuwa ni kitovu cha maendeleo na Utamaduni wa kistaarabu na Elimu iliyo pana sana katika ulimwengu basi kwao Alama hii ya Nyoka ilitumika kama uponyaji na Uhai lakini pia Nyoka alikuwa kama kiumbe anaewakilisha Miungu wengi kama ilivyo utamaduni ule wa kale wa Misri kuwakilishwa na miungu wengi.

87C4B24D-01AB-4715-905F-0A8560E2E404.jpeg

Moja ya uwakilishi wa Alama hii ya nyoka katika jamii hiyo iliyostaarabika ya Wamisri wa kale, kumwakilisha Mungu wao aitwaye Autum mungu huyu wa wamisri, ambaye aliikuwa alama ya Uhai maana wao waliamini yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa Uhai. Wamisri wale wa kale waliwakilisha uhai wa milele na alama ya Nyoka.

Mungu mwingine ni Amuun naye aliwakilishwa na alama ya nyoka huyu mungu wa wamisri wa kale aliwakilishwa na Alama nyoka alikuwa Mume wa Mungu wa kike wa zama hizo ambaye aliitwa Mut , ambaye kwa pamoja walizaa mtoto wao aitwaye khonsu,ambaye alifanya watengeneze Utatu Mtakatifu.

Na utatu huu mtakatifu wa miungu hawa uliwakilishwa na Alama ya Nyoka.
Na ukisoma hadithi zao za Misri ya kale utaona kazi za miungu hawa wanaowakilishwa na nyoka ni zile zile zinazoendana ambazo ni Uponyaji na kutoa Uhai wa Milele.

Hivyo kutupa picha kidogo juu, Ya Alama hii ambayo kwa Asilimia kubwa ni imani uponyaji na Uhai. Kuna miungu wengine kama Geb, Thermuthis, Wadjet na Buto wao pia ni miungu katika jamii za wamisri wa kale ambao ni wema kwao.
696270E4-D67D-4B51-AAA1-42F512E8CEEF.jpeg

Hao ni miongoni mwa Miungu wa misri ya kale ambao kwao na Mujibu wao walikuwa ni miungu wazuri. Ukirudi upande wa pili kuna miungu wabaya ambao miongoni mwao ni Apophis , huyu alikuwa mpinzani mkuu ambaye nae aliwakilishwa na nyoka yeye alikuwa nyoka wa giza kama wao wamisri walivyomwita.

Tunaweza kuthibitisha kwamba, kutokana na uthibitisho wa namna tofauti tofauti kama huo kutokana na hadithi nyingi, nyoka alisimama kwa wema wa hali ya juu na vile vile uovu kati ya Wamisri wa kale, na kwamba taswira ya nyoka ilihusishwa bila ubishi na maisha ya baada ya kifo, ufufuo,uponyaji na umilele.

C1CE8DF0-16CB-4948-8023-AA772D464B97.jpeg

Pia utamaduni wa kale wa Mesopotamia wababiloni na Wasumeria unaonyesha uwili unaohusishwa na Alama ya nyoka sawa na ule unaopatikana katika jamii za WaMisri.

Miungu wao wengi Akiwemo Tamuzi, pia muda mwingine aliwakilishwa na sanamu ya nyoka. Yeye na mama yake waliwakilishwa na Nyoka kwa baadhi ya vielelezi.

Miungu hawa waliwapa uponyaji wale wote waliowatii na kuwaabudu
Katika mitazamo ya ulimwengu ya Wasumeri na Wababiloni, nyoka alikuwa ni mfano wa sifa ya kuzaliwa upya na uponyaji wa Walimwengu.

Kwa hiyo, Wasumeri na Wababiloni waligeuza mambo haya ya asili kuwa miungu maalum ya nyoka kama walivyofanya kwa miungu wengine.

41A4DFE4-731B-4857-A501-58FB9CF9AA12.jpeg

Na si ajabu kukuta milango mingi ya mahekalu ya wakati huo wa tawala za Babyloni kuwa na Alama za nyoka, hasa kipindi cha mfalme nebchadneza katika milki ya Babiloni (605 - 562 K.K)

Kuna hadithi ilikuwepo miongoni mwa wababiloni kwamba, kuna mmea ulikuwepo ambao ulikuwa ukiutumia basi, huwezi kufa lakini alitokea Mungu muovu Ahriman na kutengeneza Nyoka ambaye alifanya uharibifu juu ya Mmea huo.

Lakini pia kuna hadithi ya nyoka wakubwa ambao watafanya mashambulizi dhidi ya Miungu ya kweli ya Babiloni kwa Mujibu wao. Hivyo maandishi ya Wababiloni pia yanaonesha pande mbili za Nyoka kama ilivyo katika Hadithi za Wa Misri.

Vivyo hivyo hata katika jamii za wagiriki Miungu yao Eshimun na Asclepius ambao pia walikuwa miungu ya Dawa, Tiba na uponyaji, kama itatokea mtu amekutana na Maradhi au sumu mwilini mwake basi, hawa walihusika katika Uponyaji na Ujuzi wa Dawa za kutatua matatizo mengi mengi kwa Watu wao.

7B016073-6B24-484D-BCDE-A7162079368D.jpeg

Ingawa mifano inaweza kuongezeka hapa, lakini yatosha kusema kwamba kuna uthibitisho wa kutosha ili kuonyesha wazi kwamba ibada na Alama ya nyoka kwa namna moja au nyingine ilipatikana kotekote katika eneo la kale la Mediterania, hasa miongoni mwa jamii kubwa kubwa za wakati huo ikiwemo maeneo ya karibu zaidi na Israeli.

Hadithi zinazojulikana za Mashariki ya kale hudhihirisha mapambano ya mwanzo kati ya nguvu za mema na mabaya, zote mbili ambazo mara nyingi huwakilishwa na nyoka.
Akiwa mleta wokovu na mtoaji wa uzima wa milele nyoka alifanyika upande wa kimungu. Kama msafirishaji wa kifo nyoka akawa mwili wa pepo wachafu.

Kinyume na hali ya uwili huu tunageukia sasa kwenye maandiko matakatifu, ambapo tunapata habari muhimu ili kutusaidia kuelewa kwa ukamilifu zaidi na kufahamu upana wa maelezo na ulinganifu.

INAENDELEA SEHEMU YA II

SOMA
Nyoka, alama ya Uungu (Ukombozi) au Ushetani (Upotofu)?

NYOKA ALAMA YA UKOMBOZI AU UPOTOFU KWA MUJIBU WA MAANDIKO MATAKATIFU.

Da VINCI XV
 
Nyoka.....

Pamoja na kutajwa kuwa MUOVU/ANATUMIKA NA WAOVU....lakini tunamuona akitumiwa na NABII MUSA(mtu mwema) mbele ya farao kuyameza yale majoka ya "wana mazingaombwe"......

*****************

#Never give wisdom to unworthy because it's unfair to the knowledgeable
 
Na DaVinci XV

SEHEMU YA I

Masal kheyr wakuu,

MWANZO 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.

Binafsi tangu ningali mdogo nilikuwa na tatizo la Ophidio-Phobia (Fear of Snake) kikawaida mwanadamu yoyote anaweza kuwa na Uwoga juu ya nyoka ila ule uoga uliopitiliza juu ya kiumbe hicho ndio huitwa Ophidio-Phobia. Sikumbuki hili tatizo lilianzia wapi na kwenye tukio gani, japo Ubongo wangu ulikuwa unanisukuma kuamini vitu viwili ambavyo nadhani vilikuwa vichochezi vya hii kadhia niliyo nayo.

Mosi, Ni Movies ambazo zilihusisha kiumbe huyu kushambulia wanaadamu movie kama Anaconda na nyinginezo pengine ndizo zilichagiza mimi kwa kiasi kikubwa kuwa na mtazamo wa kuogofya juu ya kiumbe huyu, Lakini Pili ,Bibi yangu kipenzi ambaye pia alikuwa mlezi wangu alipoteza uhai kwa kuumwa na Kiumbe huyu ningali bado mdogo hivyo sikuwa na uhakika wa moja kwa moja juu ya phobia yangu imetokana na nini kati ya hivyo viwili.

Kadri nilivyozidi kukua ndivyo phobia yangu iliposhuka kwasababu nlitamani kumjua kiundani kiumbe huyu na kwanini nlikuwa na uoga nae usiomithilika kiu ya Kumsoma ikanijaa kadri nilivyozidi kukata miaka kujongea Utu uzima.

Rasmi nikaingia kwenye dimbwi la kumsoma kiumbe huyu kidini, kimazingira na hata kisayansi halafu mwishowe akabadilika kutoka kwenye kumuogopa hadi kuwa miongoni mwa Viumbe pendwa ninaovutiwa nao, kama ilivyo kwa mtu mwingine yoyote kuvutiwa na Mnyama Simba au Hata Chui, nami ilitokea Sana kumhusudu Nyoka kwa namna alivyo na mwenendo wake kama ningekuwa Msanii mwenye A.K.A za wanyama Basi ningejiita Nyoka .

Nlitembelea karibuu zoo nyingi zinazotunza wanyama hawa na kujifunza aina tofauti tofauti za viumbe hawa ukiachana na kupitia majarida na facts mbalimbali kuwahusu.

Si mnakumbuka namna Mungu alivyomtumia nyoka katika visa tofauti tofauti ikiwemo pale Misri kwa Musa na Wachawi wa Firauni.

Lakini pia si mnakumbuka Nyoka alivyotumika na Ibilisi kumhadaa Mama yetu Hawa kule bustanini Eden, na Kwenye baadhi ya Mandiko nyoka akabaki kitendawili atasimama Upande upi wema au Ubaya.

Kwani ninyi hamkumbuki vita iliyowekwa kati ya kiumbe huyu na mwanadamu kwenye maandiko popote wakutanapo?

Nyoka akanenwa kwa Ubaya sehemu nyingi sana. Na kutokana na maandiko hayo ya mwanzo ambayo Mwanaadamu akikutana na Nyoka basi kinachofata ni vita haijalishi kiumbe huyo alikuwa anataka kudhuru au yupo katika Eneo lake.

Na si mnakumbuka Pale zamani wazee walipotuhadithia mengi sana kuhusu kiumbe huyu wakatutisha kwamba ukiota ndoto za Nyoka basi majini wanakuwa wanashughulika nawe kwa namna moja au nyingine,

Mungu alimuumba nyoka kwa namna ya tofauti sana na kumpa uwezo wa kipekee mno, si unafahamu ya kwamba nyoka kila muda huzaliwa upya pale anapojivua gamba na hii imefanya wengi kuamini kwamba nyoka huwa hawazeeki,na hii ndio kielelezo cha jamii nyingine kumtumia nyoka kama alama ya kuzaliwa upya.

Tukamuona Nyoka katika nembo nyingi sana ikiwemo kwenye Tiba na Afya mahospitalini, waganga wa jadi , Mahekalu na Madhabau, Vikundi vya siri , pete na mikufu ya Watu wakubwa, makanisa, mashirika makubwa makubwa duniani na Logo tofauti tofauti.

Na wengi wakahitimisha kwamba mashirika hayo yapo chini ya Shetani pengine kwasababu tu Alama ya nyoka katika nembo Bila kufahamu haswa chanzo chake ni nini.

Kuna karibu species zaidi ya 3000 za nyoka na karibu species 600 tu ndio nyoka wenye Sumu duniani. Nyoka huishi sehemu tofauti ikiwemo kwenye mchanga, Majangwa, Mapango na Miamba mikubwa, kwenye Maji, vichaka na nyasi ndefu na kuna wanaoishi kwenye miti mirefu.

Nyoka wengi hula Mijusi, Ndege, vyura na Wadudu wengine wadogowadogo.

MTAZAMO WA NYOKA KULINGANA NA JAMII ZA KALE
Huko misri ya kale ambapo dunia ya sasa kuna wanaomini, ilikuwa ni kitovu cha maendeleo na Utamaduni wa kistaarabu na Elimu iliyo pana sana katika ulimwengu basi kwao Alama hii ya Nyoka ilitumika kama uponyaji na Uhai lakini pia Nyoka alikuwa kama kiumbe anaewakilisha Miungu wengi kama ilivyo utamaduni ule wa kale wa Misri kuwakilishwa na miungu wengi.

Moja ya uwakilishi wa Alama hii ya nyoka katika jamii hiyo iliyostaarabika ya Wamisri wa kale, kumwakilisha Mungu wao aitwaye Autum mungu huyu wa wamisri, ambaye aliikuwa alama ya Uhai maana wao waliamini yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa Uhai. Wamisri wale wa kale waliwakilisha uhai wa milele na alama ya Nyoka.

Mungu mwingine ni Amuun naye aliwakilishwa na alama ya nyoka huyu mungu wa wamisri wa kale aliwakilishwa na Alama nyoka alikuwa Mume wa Mungu wa kike wa zama hizo ambaye aliitwa Mut , ambaye kwa pamoja walizaa mtoto wao aitwaye khonsu,ambaye alifanya watengeneze Utatu Mtakatifu.

Na utatu huu mtakatifu wa miungu hawa uliwakilishwa na Alama ya Nyoka.
Na ukisoma hadithi zao za Misri ya kale utaona kazi za miungu hawa wanaowakilishwa na nyoka ni zile zile zinazoendana ambazo ni Uponyaji na kutoa Uhai wa Milele.

Hivyo kutupa picha kidogo juu, Ya Alama hii ambayo kwa Asilimia kubwa ni imani uponyaji na Uhai. Kuna miungu wengine kama Geb, Thermuthis, Wadjet na Buto wao pia ni miungu katika jamii za wamisri wa kale ambao ni wema kwao.

Hao ni miongoni mwa Miungu wa misri ya kale ambao kwao na Mujibu wao walikuwa ni miungu wazuri. Ukirudi upande wa pili kuna miungu wabaya ambao miongoni mwao ni Apophis , huyu alikuwa mpinzani mkuu ambaye nae aliwakilishwa na nyoka yeye alikuwa nyoka wa giza kama wao wamisri walivyomwita.

Tunaweza kuthibitisha kwamba, kutokana na uthibitisho wa namna tofauti tofauti kama huo kutokana na hadithi nyingi, nyoka alisimama kwa wema wa hali ya juu na vile vile uovu kati ya Wamisri wa kale, na kwamba taswira ya nyoka ilihusishwa bila ubishi na maisha ya baada ya kifo, ufufuo,uponyaji na umilele.

Pia utamaduni wa kale wa Mesopotamia wababiloni na Wasumeria unaonyesha uwili unaohusishwa na Alama ya nyoka sawa na ule unaopatikana katika jamii za WaMisri.

Miungu wao wengi Akiwemo Tamuzi, pia muda mwingine aliwakilishwa na sanamu ya nyoka. Yeye na mama yake waliwakilishwa na Nyoka kwa baadhi ya vielelezi.

Miungu hawa waliwapa uponyaji wale wote waliowatii na kuwaabudu
Katika mitazamo ya ulimwengu ya Wasumeri na Wababiloni, nyoka alikuwa ni mfano wa sifa ya kuzaliwa upya na uponyaji wa Walimwengu.

Kwa hiyo, Wasumeri na Wababiloni waligeuza mambo haya ya asili kuwa miungu maalum ya nyoka kama walivyofanya kwa miungu wengine.

Na si ajabu kukuta milango mingi ya mahekalu ya wakati huo wa tawala za Babyloni kuwa na Alama za nyoka, hasa kipindi cha mfalme nebchadneza katika milki ya Babiloni (605 - 562 K.K)

Kuna hadithi ilikuwepo miongoni mwa wababiloni kwamba, kuna mmea ulikuwepo ambao ulikuwa ukiutumia basi, huwezi kufa lakini alitokea Mungu muovu Ahriman na kutengeneza Nyoka ambaye alifanya uharibifu juu ya Mmea huo.

Lakini pia kuna hadithi ya nyoka wakubwa ambao watafanya mashambulizi dhidi ya Miungu ya kweli ya Babiloni kwa Mujibu wao. Hivyo maandishi ya Wababiloni pia yanaonesha pande mbili za Nyoka kama ilivyo katika Hadithi za Wa Misri.

Vivyo hivyo hata katika jamii za wagiriki Miungu yao Eshimun na Asclepius ambao pia walikuwa miungu ya Dawa, Tiba na uponyaji, kama itatokea mtu amekutana na Maradhi au sumu mwilini mwake basi, hawa walihusika katika Uponyaji na Ujuzi wa Dawa za kutatua matatizo mengi mengi kwa Watu wao.

Ingawa mifano inaweza kuongezeka hapa, lakini yatosha kusema kwamba kuna uthibitisho wa kutosha ili kuonyesha wazi kwamba ibada na Alama ya nyoka kwa namna moja au nyingine ilipatikana kotekote katika eneo la kale la Mediterania, hasa miongoni mwa jamii kubwa kubwa za wakati huo ikiwemo maeneo ya karibu zaidi na Israeli.

Hadithi zinazojulikana za Mashariki ya kale hudhihirisha mapambano ya mwanzo kati ya nguvu za mema na mabaya, zote mbili ambazo mara nyingi huwakilishwa na nyoka.
Akiwa mleta wokovu na mtoaji wa uzima wa milele nyoka alifanyika upande wa kimungu. Kama msafirishaji wa kifo nyoka akawa mwili wa pepo wachafu.

Kinyume na hali ya uwili huu tunageukia sasa kwenye maandiko matakatifu, ambapo tunapata habari muhimu ili kutusaidia kuelewa kwa ukamilifu zaidi na kufahamu upana wa maelezo na ulinganifu.

INAENDELEA SEHEMU YA II

NYOKA ALAMA YA UKOMBOZI AU UPOTOFU KWA MUJIBU WA MAANDIKO MATAKATIFU.

Da VINCI XV
 
Nyoka.....

Pamoja na kutajwa kuwa MUOVU/ANATUMIKA NA WAOVU....lakini tunamuona akitumiwa na NABII MUSA(mtu mwema) mbele ya farao kuyameza yale majoka ya "wana mazingaombwe"......

*****************

#Never give wisdom to unworthy because it's unfair to the knowledgeable
Naam,
Fuatana namimi nadhanu kipande cha pili nmejaribu kuzungumzia kitu cha namna hiyo.
 
KWA MIZIMU NYOKA NI UKUU,NYOKA NI UTAWALA NA ANAPOONEKANA NDOTONI AU KWENYE MAONI HUTAFSRIKA KAMA ULINZI MTUKUFU DHIDI YA HATARI ILIYO DHAHIRI.KWA UTABIBU NYOKA HUASHIRIA NAMNA TUKUFU YA UTABIBU USIMITHILIKA.KIROHO HUTAFSRIKA KAMA TAWALA ISIYOTETEREKA NA YENYE UUNGU MTUKUFU.MWISHO KIUJUMLA HUFASIRIKA KAMA UFALME WA WAFALME.
 
Ndotoni nyoka hutumika ili kumshtua mtu aamke.

Yaani kama umelala vibaya, damu haizunguki vizuri. Basi anakuja nyoka kwenye ndoto ili akutie presha kidogo moyo usukume damu izunguke mwili wote.

Lakini kama umejifunika gubigubi joto limezidi. Basi anakuja nyoka ndotoni akuvuruge ubiringike uliondoe blanketi.

Ikiwezekana basi hiyo adrenalini atakayokupiga itakuamsha ili urekebishe hali mbaya uendelee kuishi.

So wanaohusianisha nyoka na mizimu au majini basi waende mbele na kusema ni mizimu wazuri au majini wazuri wanaokutakia mema. Uishi wala usife.

Desperate needs, calls for desperate actions. Ikibidi kukuamsha na umelala fofofo na unazidi kuishiwa uhai pumzi........ basi inakuwa ndo muda wa kulileta 'bomu la maangamizi' (call in the big guns);

Linaletwa jinamizi ambalo ni mixer ya zimwi, jitu na joka kubwa. Utaaamka tu. Je jinamizi ndio malaika mlinzi!!!????👇
 
KWA MIZIMU NYOKA NI UKUU,NYOKA NI UTAWALA NA ANAPOONEKANA NDOTONI AU KWENYE MAONI HUTAFSRIKA KAMA ULINZI MTUKUFU DHIDI YA HATARI ILIYO DHAHIRI.KWA UTABIBU NYOKA HUASHIRIA NAMNA TUKUFU YA UTABIBU USIMITHILIKA.KIROHO HUTAFSRIKA KAMA TAWALA ISIYOTETEREKA NA YENYE UUNGU MTUKUFU.MWISHO KIUJUMLA HUFASIRIKA KAMA UFALME WA WAFALME.
Sawa
Asante kwa mchango, kuna part nyingi sana nlizifupisha. Ili kuleta uzi usio mrefu.

Mungu akipenda nitaleta Alama ya Nyoka kwa Mtizamo wa Jamii za Kiafrika.
 
Back
Top Bottom