Nyimbo za Tanzania zilipendwa zaidi Kenya 2016

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
26,151
22,726
_91948805_diamondbbcextra.jpg



Video za muziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania ndizo zilizotazamwa zaidi na Wakenya katika mtandao wa YouTube, unaomilikiwa na Google, mwaka huu, takwimu zinaonyesha.

Video hizo zinatawala katika orodha ya video kumi zilizotazamwa zaidi, inayoongoza ikiwa video ya wimbo Salome, uliofanywa upya na Diamond Platnumz na Rayvanny.

Wimbo wa Work, wao Rihanna na Drake ni wa pili lakini kutoka hapo anaingia Diamond Platnumz na Harmonize wakiwa na wimbo wao Bado.

Video ya kwanza ya Wakenya kwenye orodha hiyo ni ya Sauti Sol kwa wimbo wao Unconditionally Bae, lakini bado kwenye wimbo huo walishirikiana na mwanamuziki Mtanzania, Alikiba.

Video nyingine za nyimbo katika orodha hiyo ni Work from Home wa Mmarekani Ty Dolla Sign na kundi la wasichana la Fifth Harmony, This is What You Came For wake raia wa Scotland Calvin Harris, Kwetu wake Rayvanny kutoka Tanzania, Cheap Thrills wao raia wa Australia Sia na Sean Paul wa Jamaica, Pillow Talk wa Mwingereza Zayn na Ain't Your Mama wa Mmarekani Jenniffer Lopez.

Orodha kamili:

  1. Salome - Diamond Platnumz na Rayvanny.
  2. Work - Rihanna na Drake
  3. Bado - Diamond Platnumz na Harmonize
  4. Sauti Sol - Unconditionally Bae, na Alikiba.
  5. Work from Home - Ty Dolla Sign na Fifth Harmony
  6. This is What You Came For - Calvin Harris
  7. Kwetu - Rayvanny
  8. Cheap Thrills - Sia na Sean Paul
  9. Pillow Talk - Zayn
  10. Ain't Your Mama - Jenniffer Lopez.
Source : BBC Nyimbo za Tanzania zilipendwa zaidi Kenya 2016 - BBC Swahili

Hogera za dhati kwa WCB.
 
Habari hii ni chungu mnoo upande wa pili....... Sipati picha kabisa.
 
Mbona huku vijeweni wanasema Alikiba ndo anapendwa zaidi Kenya na Aje ndo nyimbo nyimbo inakimbiza kenya
 
Mbona sielewi mara video ya kwanza kwenye orodha hiyo ni uncondtionaly mara wakati huo kwenye orodha kamili wimbo wa kwanza ni salome
 
Mbona sielewi mara video ya kwanza kwenye orodha hiyo ni uncondtionaly mara wakati huo kwenye orodha kamili wimbo wa kwanza ni salome
Soma vizuri wamesema kwa video za wakenya wenyewe iyo unconditional bae ndo ya kwanza japo kwenye msimamo wa jumla iko katikati
 
kwani mnavyotoa habari inakuwa ni kwa ajili ya kuwaonyesha team kiba au watu wote, huu upumbavu kumbe mashabiki ndo tunaulea

btw, hong3ra kwao wote
 
Back
Top Bottom