Nyimbo za Maombolezo Kifo cha Nyerere

PRINCEd

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
851
594
Wadau alie na nyimbo za maombolezo ya kifo cha Nyerere zilizoimbwa na marehem Komba....

Naomba aziweke hapa.....
 
Wadau alie na nyimbo za maombolezo ya kifo cha Nyerere zilizoimbwa na marehem Komba....

Naomba aziweke hapa.....

Sorry Prince D, naomba kupitia uzi wako niombe zile za DDC Mlimani Park kwenye maombolezo hayohayo
 
Wadau alie na nyimbo za maombolezo ya kifo cha Nyerere zilizoimbwa na marehem Komba....

Naomba aziweke hapa.....
Leo nimesikiliza kipindi cha "Hizi nazo" cha Radio One Stereo, nimefurahi sana japo hazikuwa nyimbo za maombolezo ila nyimbo zilizopigwa ilikuwa ni darasa tosha la kumfahamu mwl Nyerere kuwa alikuwa nani na ni nani.
 
Nyimbo nzuri zilizoteka hisia wakati ule zilimbwa na wanafunzi na baazi ya vikundi mfano wa nyimbo

1.Parapanda italia Parapanda
2.Kilio ham Kilio ham huu wimbo dah watoto walikuwa mpaka na wewe unalikuta unalia
3.hii sasa ndio ilikuwa funga kazi kwa wanakumbuka alikuwepo mzee moja hivi yeye peke yake ebwana anaimba uyo nakumbuka baadhi ya mashairi nyerere baba wa taifa nyerere tuna kulilia

Yani kipindi cha maombolezo mda ule Kuna nyimbo zilipendwa ilikuwa ITV wakipiga tu huo wimbo basi lazima ukimbilie TV
 
kuna mzee mmoja na gitaa lake alikuwa anatokea hawavumj lakini wamo... kibao chake kilikuwa buriani baba nyerere buriani baba wa taifa.... ilikuwa Huzuni sana aisee.... mwenye nazo jamani alete hapa tudownload
 
Nyimbo nzuri zilizoteka hisia wakati ule zilimbwa na wanafunzi na baazi ya vikundi mfano wa nyimbo

1.Parapanda italia Parapanda
2.Kilio ham Kilio ham huu wimbo dah watoto walikuwa mpaka na wewe unalikuta unalia
3.hii sasa ndio ilikuwa funga kazi kwa wanakumbuka alikuwepo mzee moja hivi yeye peke yake ebwana anaimba uyo nakumbuka baadhi ya mashairi nyerere baba wa taifa nyerere tuna kulilia

Yani kipindi cha maombolezo mda ule Kuna nyimbo zilipendwa ilikuwa ITV wakipiga tu huo wimbo basi lazima ukimbilie TV
Mshumaa huwaka polepole
Hata kuwe na upepo mwingi
Mshumaa taratibu humulika mwanga wake
Upepo hauwezi kuuzima
Mshumaa huvumilia shida
Polepole humulika hadi mwisho
Maisha yake mwanadamu
Yanafananishwa na mshumaa
Toka anapozaliwa hadi kifo
Mwalimu jk Nyerere
Ni mfano bora wa mshumaa
Kapigania kaleta uhuru Tanzania
Kadumisha amani na umoja
Tanzania na afrika nzima
Nyerere kazi kubwa umefanya baba buriani
Kibwagizo
Tutaonana tena baba
Tutaonana tena baba
Tutaonana tena baba
Siku ile nzuriiiiiiii
 
Nyingine ni kama ule ulioimbwa na watangazaji wa Clouds akiwamo Fina Mango ukiwa na maneno" Tutakukumbuka baba wa taifa....amani, busara...twaviweka mioyoni" na mwingine wenye maneno "Nyerere baba wa taifa tunakukumbuka, kwa yale yote uliyofanya tunakukumbuka....", "Nyota Umekwendaa.... Twalia....watuacha wenyewe twalia" na "Tangulia Mwalimu" ulioimbwa na Parapanda Arts (Mgunga Mwa Mnyenyelwa na Mrisho Mpoto), Mwingine ni ule ulioimbwa na wanamuziki wa kikongo waishio Tanzania kama Remmy Ongala, TShimanga Asosa na King Kiki ukiwa na maneno " Nyerere baba twakulilia eeh...", na wimbo mmoja hivi ulioimbwa na jamaa mmoja huku kukisikika keyboard ya simanzi sana. Wimbo huo ulikuwa poa sana na ulikuwa na maneno "Mwalimu Nyerere umetuacha na majonzi...(kwa heri Mwalimu)..."

Pia na rap moja hivi sijui ilikuwa ya vijana gani ikiwa na maneno "Nyota imezimika". Daah binafsi hizi nyimbo zilikuwa zinanizidishia simanzi sana.

Ni kipindi hicho ndipo nami nilijikuta nafsi yangu ikinisuta na kukubali kwamba " Hakika Nyerere alikuwa ni mtu wa watu".

Miezi michache baadae Twanga Pepeta wakatoa wimbo wenye maneno "Nyerere Ndiye Mwanasiasa wa Karne".
 
Nadhani nyimbo nyingi za maombolezo zilihifadhiwa na kutoruhusiwa kuwa free. Maana hata zile kanda za tape zenye mkusanyiko wa hizo nilishatafuta sizipati. Si uongo ukiwa disappointed ukazisikiliza nyimbo zile hata nafsi inaweza badili kisasi ulichonacho
 
Mimi ninazo karibia zote kwenye cassette. Nilitumia muda mwingi kuwa nazirekodi kutoka redioni kipindi cha huo msiba.
 
Nyimbo nzuri zilizoteka hisia wakati ule zilimbwa na wanafunzi na baazi ya vikundi mfano wa nyimbo

1.Parapanda italia Parapanda
2.Kilio ham Kilio ham huu wimbo dah watoto walikuwa mpaka na wewe unalikuta unalia
3.hii sasa ndio ilikuwa funga kazi kwa wanakumbuka alikuwepo mzee moja hivi yeye peke yake ebwana anaimba uyo nakumbuka baadhi ya mashairi nyerere baba wa taifa nyerere tuna kulilia

Yani kipindi cha maombolezo mda ule Kuna nyimbo zilipendwa ilikuwa ITV wakipiga tu huo wimbo basi lazima ukimbilie TV
Yule wa buriani baba nyererex2
 
Back
Top Bottom