NYARAKA: Katiba Inayopendekezwa Oktoba, 2014 (Tanzania's Proposed Constitution)

KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI BORA KULIKO YA SASA, HONGERA MH. RAISI, HONGERA WATANZANIA.

Katika historia ya uandishi wa katiba mpya duniani hakuna nchi yeyote ambayo iliwahi kuandika katiba mpya ikakidhi matakwa ya wananchi wote na taifa kwa 100%. Katiba si msaafu wala si biblia kwamba haiwezi kufanyiwa maboresho. Leo hii jambo ambalo tumeliona lina tija na manufaa kwa taifa na tukaliingiza kwenye katiba, kesho tutaliona halina tija na tutakubaliana kuliondoa au kuliboresha. Vilevile jambo ambalo leo tumeliona halina tija na kutoliingiza ndani ya katiba kesho tutaona umuhimu wake na tutakubaliana kuliingiza ndani ya katiba yetu.

Katiba inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wasanii, vijana, wanawake na wengine. Pia katiba inayopendekezwa imetambua haki bunifu, mgombea, binafsi, maboresho katika muungano wetu sambamba na kuweka mfumo bora wa kusimamia rasirimali za taifa na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya rasirimali. Kundi pekee ambalo linadhani halijatendewa haki katika katiba hii ni kundi la wanasiasa wachache ambao kwao tafsiri ya katiba bora ni ile inayokidhi maslahi yao ya kisiasa. Hili ni jambo ambalo watanzania hawana budi kulikataa.

Jambo la msingi ambalo kila mtanzania anapaswa kukubali ni kwamba katiba inayopendekezwa ni bora kuliko ile ya sasa. Wakati ambapo baadhi ya watu wakiipinga na kudai kwamba haiwezi kulivusha taifa letu, wapo watanzania tena asilimia kubwa ambao wanaiona katiba inayopendekezwa kuwa ni chombo madhubuti ambacho kitachochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
hiyo ndiyo afya ya demokrasia iache ichukue nafasi yake. Tupingane kwa hoja bila kuhatarisha amani ya taifa letu.

Hongera Mh. Raisi Dr. Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hili ni jambo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa letu kuandika katiba yake kwa kushirikisha wananchi wake. Yapo mataifa ambayo yaliwahi kuandika katiba zao kwa kutumia Bunge la katiba pekee, wapo waliogeuza Bunge la kawaida na kuwa Bunge la katiba. Kwa taifa letu, mchakato umekuwa wa kidemokrasia zaidi kiasi kwamba wapo wanazuoni, wanasiasa na mataifa mbalimbali ambao wameishangaa Tanzania kwa kuruhusu demokrasia kwa kiwango hiki. Kwa hakika Mh. Rais anastahili pongezi na daima watanzania tutakukumbuka na jina lako haliwezi kufutika katika fikra zao.
 
Kwanza ningependa mnieleweshe rasimu imesema rais wa znz ndo atakua makamo wa kwnza wa rais wa muungano je kama rais wa muungano katokea znz na huyu makamo wa rais nae atatokea serikali ya znz au ni njama za ccm tu kufanya mzanibari asiwe rais wa muungano ?

Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania, kwani sisi huku Tanganika tulimpigia kura yeye mpaka awe mfanya maamuzi wetu?
 
KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI BORA KULIKO YA SASA, HONGERA MH. RAISI, HONGERA WATANZANIA.

Katika historia ya uandishi wa katiba mpya duniani hakuna nchi yeyote ambayo iliwahi kuandika katiba mpya ikakidhi matakwa ya wananchi wote na taifa kwa 100%. Katiba si msaafu wala si biblia kwamba haiwezi kufanyiwa maboresho. Leo hii jambo ambalo tumeliona lina tija na manufaa kwa taifa na tukaliingiza kwenye katiba, kesho tutaliona halina tija na tutakubaliana kuliondoa au kuliboresha. Vilevile jambo ambalo leo tumeliona halina tija na kutoliingiza ndani ya katiba kesho tutaona umuhimu wake na tutakubaliana kuliingiza ndani ya katiba yetu.

Katiba inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wasanii, vijana, wanawake na wengine. Pia katiba inayopendekezwa imetambua haki bunifu, mgombea, binafsi, maboresho katika muungano wetu sambamba na kuweka mfumo bora wa kusimamia rasirimali za taifa na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya rasirimali. Kundi pekee ambalo linadhani halijatendewa haki katika katiba hii ni kundi la wanasiasa wachache ambao kwao tafsiri ya katiba bora ni ile inayokidhi maslahi yao ya kisiasa. Hili ni jambo ambalo watanzania hawana budi kulikataa.

Jambo la msingi ambalo kila mtanzania anapaswa kukubali ni kwamba katiba inayopendekezwa ni bora kuliko ile ya sasa. Wakati ambapo baadhi ya watu wakiipinga na kudai kwamba haiwezi kulivusha taifa letu, wapo watanzania tena asilimia kubwa ambao wanaiona katiba inayopendekezwa kuwa ni chombo madhubuti ambacho kitachochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
hiyo ndiyo afya ya demokrasia iache ichukue nafasi yake. Tupingane kwa hoja bila kuhatarisha amani ya taifa letu.

Hongera Mh. Raisi Dr. Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hili ni jambo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa letu kuandika katiba yake kwa kushirikisha wananchi wake. Yapo mataifa ambayo yaliwahi kuandika katiba zao kwa kutumia Bunge la katiba pekee, wapo waliogeuza Bunge la kawaida na kuwa Bunge la katiba. Kwa taifa letu, mchakato umekuwa wa kidemokrasia zaidi kiasi kwamba wapo wanazuoni, wanasiasa na mataifa mbalimbali ambao wameishangaa Tanzania kwa kuruhusu demokrasia kwa kiwango hiki. Kwa hakika Mh. Rais anastahili pongezi na daima watanzania tutakukumbuka na jina lako haliwezi kufutika katika fikra zao.
 
Mimi siangalii umati, mimi naangalia content ya katiba. Hao waliokusanyika hapo wengi wamesombwa kwa malori, wengine wana maslahi na CCM, na wengine wamekuja kushanga farasi.
Moja ya matatizo makubwa ya nchii ni viongozi kujirundikia mali wananchi wa kawaida kuwa mafukala.

Mfano nimetoa hapo juu.
Mkuu wa mkoa anafanya madudu lakini mwananchi hana mamlaka ya kumwajibisha kwa kuwa yeye ni mteule wa Rais
Wakurugenzi wanaiba pesa lakini wako mwajiri wao ni Waziri mkuu, ambae ni mteule wa Rais
Rais anateua watu wasio na kiwango au marafiki zake anavyotaka yeye bila kudhibitishwa na wabunge
Wabunge wameongezwa zaidi

Haina tofauti na hii ya sasa

Usitishwe na vilio vya wenye njaa za mamlaka....
 
Shame on you Tanzanians! Watawala wakianzisha wimbo wowote nyie mnaitikia tu hata kama hamjui maana ya maneno ya wimbo huo. Tumerogwa kupitiliza? Bora hata na Wagalatia. Rais amesema muda ukifika mambo huwa. Nausubiri muda huo nitakapopata Katiba ya kweli ya Tanzania. CCM sio Tanzania.
 
Kwa hiyo unakubaliana nami kuwa katiba hiyo sio mpya bali ni ile ile ya zamani iliyofanyiwa marekebisho? Kwa msingi huo basi Kikwete alikuwa na haja gani ya kuunda tume ya katiba wakati alijua wazi kuwa anahitaji marekebisho ya katiba na sio katiba mpya? Au tafsiri ya upya kwenu ni kubadili kava la nje? Au ndo namna ya kuwadanganya wananchi na hao wanaojiita bunge la katiba kuwa wameweka historia ya katiba mpya kumbe ukweli wameweka historia ya kurekebisha katiba ya zamani?

Huwezi ukawa na katiba mpya yenye mfumo ule ule. Kama mahitaji yaliopo hayahitaji mfumo kubadilika basi hakukuwa na haja ya katiba mpya. Kilichotakiwa ni maboresho tu ya katiba iliopo. Kazi ilotakiwa ifanywe la bunge la jamuhuri.

Binafsi sioni haja ya mapendekezo haya kupelekwa kwa wananchi maana hayakidhi vigezo vya upya wa katiba.

Kama Hakuna mabadiliko ya mfumo hakuna katiba mpya.
 
Wale jamaa wa upande mwingine walidhani wakisusa basi hakuna katiba itayotengenezwa.
Lkn ni jambo la heri leo hii tuna katiba iliyo pendekezwa na ni nzuri kwa ssbabu imeshika kila mahali.
Ni jambo la kushangaza pale mwana siasa anaposimama na mishipa kumtoka akisema eti usawa wa kijinsia yaani 50 kwa 50 itanufaisha wachache halafu yeye mwenyewe ni mwanamke? Unajiuliza hawa watu wapo serious kweli???
Nasema hongera wabunge wote mliomaliza kazi hii na hongera saaana mh. Sitta na samie.
 
Habari za muda huu wadau, natamani nifanye comparison kati ya rasimu ya warioba na katiba inayopendekezwa na Sitta, so please mwenye softcopy ya katiba inayopendekezwa aiweke hapa.

Natanguliza shukrani.
 
Hiyo katiba ya kufanya wajumbe wa Bunge maalum wacheze disko bungeni, wote wakapiga kura ya ndiyo, ina walakini hii katiba

Mkuu naleo waliandaliwa watu wakukata viuno mbele yajukwaa kuu wamekata viuno na ninaamini bado wataendelea kukata hatauko watakapoenda maana nimesikia wamepewa kazi yakua wajumbe wakuenda kutetea kwa wananchi yale waliyoyapitisha mm wakija kwangu kunishawishi nawaambia katikeni kwanza.
 
Rasimu ndiyo iliyofanyiwa marekebeisho mkuu ndo ikaja hii kitu aliyopewa JK leo, naitaka sasa hiyo ya leo ili nami nijionee mwenyewe yaliyomo na uzuri au ubaya wake.. Katiba inayotumika sasa naifahamu na ninayo
 
Ukiwa na "UKAWA mentality" lazima utadai kuwa Katiba inayopendekezwa ni mbaya!
 
Hapana kaka, siko ukawa na wala sijawahi kuwa ukawa, natamani tu nami niisome hiyo katiba mwenyewe ili nijue ni nzuri kiasi au ina mabaya kiasi gani nikilinganisha na katiba ya sasa na ile rasimu..
 
Back
Top Bottom