NYARAKA: Katiba Inayopendekezwa Oktoba, 2014 (Tanzania's Proposed Constitution)

KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI BORA KULIKO YA SASA, HONGERA MH. RAISI, HONGERA WATANZANIA.

Katika historia ya uandishi wa katiba mpya duniani hakuna nchi yeyote ambayo iliwahi kuandika katiba mpya ikakidhi matakwa ya wananchi wote na taifa kwa 100%. Katiba si msaafu wala si biblia kwamba haiwezi kufanyiwa maboresho. Leo hii jambo ambalo tumeliona lina tija na manufaa kwa taifa na tukaliingiza kwenye katiba, kesho tutaliona halina tija na tutakubaliana kuliondoa au kuliboresha. Vilevile jambo ambalo leo tumeliona halina tija na kutoliingiza ndani ya katiba kesho tutaona umuhimu wake na tutakubaliana kuliingiza ndani ya katiba yetu.

Katiba inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wasanii, vijana, wanawake na wengine. Pia katiba inayopendekezwa imetambua haki bunifu, mgombea, binafsi, maboresho katika muungano wetu sambamba na kuweka mfumo bora wa kusimamia rasirimali za taifa na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya rasirimali. Kundi pekee ambalo linadhani halijatendewa haki katika katiba hii ni kundi la wanasiasa wachache ambao kwao tafsiri ya katiba bora ni ile inayokidhi maslahi yao ya kisiasa. Hili ni jambo ambalo watanzania hawana budi kulikataa.

Jambo la msingi ambalo kila mtanzania anapaswa kukubali ni kwamba katiba inayopendekezwa ni bora kuliko ile ya sasa. Wakati ambapo baadhi ya watu wakiipinga na kudai kwamba haiwezi kulivusha taifa letu, wapo watanzania tena asilimia kubwa ambao wanaiona katiba inayopendekezwa kuwa ni chombo madhubuti ambacho kitachochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
hiyo ndiyo afya ya demokrasia iache ichukue nafasi yake. Tupingane kwa hoja bila kuhatarisha amani ya taifa letu.

Hongera Mh. Raisi Dr. Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hili ni jambo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa letu kuandika katiba yake kwa kushirikisha wananchi wake. Yapo mataifa ambayo yaliwahi kuandika katiba zao kwa kutumia Bunge la katiba pekee, wapo waliogeuza Bunge la kawaida na kuwa Bunge la katiba. Kwa taifa letu, mchakato umekuwa wa kidemokrasia zaidi kiasi kwamba wapo wanazuoni, wanasiasa na mataifa mbalimbali ambao wameishangaa Tanzania kwa kuruhusu demokrasia kwa kiwango hiki. Kwa hakika Mh. Rais anastahili pongezi na daima watanzania tutakukumbuka na jina lako haliwezi kufutika katika fikra zao.
 
Nimejitahidi kusoma katiba pendekezwa. Tofauti yake na ile ya 1977 ni ndogo sana. Bado Rais anaendelea kuwa na madaraka makubwa, yaani Rais anateua watendaji wengi ambapo Wananchi hawawezi kuwaondoa, Rais ameendelea kuwa mfalme.
Waziri kaendelea kuwa Mbunge wa kawaida
Wateule wa Rais hawadhibitishwi na Bunge kama ilivyo kuwa katika Rasimu ya Warioba
Wabunge wameongezwa zaidi, hii ni mzigo kwa walipa kodi


Kwa ujumla ni propaganda tu za kusema eti haki za wafugaji. Hii katiba pendekezwa imekidhi matakwa ya watawala na wala si Raia wa kawaida
 
Watanzania wote hatuwezi kuwa na msimamo mmoja, ila ccm mna msimamo mmoja. Lazima mjitizame, kwanini ccm wote mna mtizamo mmoja?

Hiyo katiba ya kufanya wajumbe wa Bunge maalum wacheze disko bungeni, wote wakapiga kura ya ndiyo, ina walakini hii katiba
 
Katiba nzuri

Uzuri wake nini mkuu? Utakimbilia kusema haki za wafugaji

Rais akiiba unaweza kumshitaki?
Mafisadi ambae ni wateule wa Rais wewe mwananchi unaweza kumuwajibisha?
Wateule wa Rais wanadhibitishwa na Bunge kama ilivyo kwa nchi za kidemocrasia?
Mkuu wa mkoa, wilaya, mkurugenzi wa Halmashauri unaweza kuwawajibisha wewe mwananchi?
Mbona sasa wabunge wameongezeka kuliko mwanzo?
 
Suala sio kuwa na katiba bora kuliko nyingine, tunataka katiba ya kukidhi haja ya miaka 50 ijayo na iliyopendekezwa na wananchi, sio ya mafisadi wanaotaka kufungua akaunti nje ya nchi na wanaotaka wakipewa zawadi wakati wa shuguli za umma wakagawane na mahawala zao badala ya kukabidhi watanzania. Katiba hii ya hovyo ilisababisha JK ahongwe suti na muarabu, katiba mpya inazuia kupewa zawadi za kirushwa rushwa mlizozoea maCCM
 
Hebu mleta mada tupe ufafanuzi wa kifungu no.20 ili tuone wakulima, wafugaji, wasanii kama kweli wamepewa haki zozote au ni kiini macho. Jabirimakame ufafanuzi tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Alinda hujui na huna weledi kwenye hili.
Rasimu ya warioba haikuainisha baadhi ya mambo sababu ni ya nchi husika mf ardhi, wafugaji wakulima, wasanii etc.

Maana yake ni kwamba kila nchi ingetengeneza katiba yake na kuwema mambo yake husika na mwisho wa siku tungekuwa na katika tatu.
Ya muungano
Ya tanganyika
Ya znz


Na hapo ndo watz wengi mumepotea na ccm wametake advantage ya uelewa wenu mdogo na wavivu wa kusoma.

Huwezi kumfukuza mtu kwa sababu kapinga baadhi ya vipengere halafu useme nchi ina demokrasia.

Hii rasimu ya sasa inamnyima mtz haki nyingi na hakuna mahala utaenda kudai maana hakuna hata sheria itatungwa sababu katiba haija state
 
Katiba nzuri

Nyie walamba miguu ya mafisadi kila kitu kwenu kizuri. Hukuona Kenya watu wanahojiwa na kamati ya bunge live kwenye Tv ili wapate nafasi walizoteuliwa, au ndio na wewe walewale ulitoa kiboga ukapata kazi serikalini unataka katiba ibaki kama ya zamani umrithishe nafasi yako hawara yako. Dizaini za akina Vicky Kamata sio
 
Nyie walamba miguu ya mafisadi kila kitu kwenu kizuri. Hukuona Kenya watu wanahojiwa na kamati ya bunge live kwenye Tv ili wapate nafasi walizoteuliwa, au ndio na wewe walewale ulitoa kiboga ukapata kazi serikalini unataka katiba ibaki kama ya zamani umrithishe nafasi yako hawara yako. Dizaini za akina Vicky Kamata sio


Acha hasira bwanamdogo itakugharimu.....

Kwa akili yako fupi watu karibu 500 walioketi chini kutuletea rasimu wewe unawazidi ufahamu??

Hebu kaoge huko usilete kikwapa hapa
 
Uzuri wake nini mkuu? Utakimbilia kusema haki za wafugaji

Rais akiiba unaweza kumshitaki?
Mafisadi ambae ni wateule wa Rais wewe mwananchi unaweza kumuwajibisha?
Wateule wa Rais wanadhibitishwa na Bunge kama ilivyo kwa nchi za kidemocrasia?
Mkuu wa mkoa, wilaya, mkurugenzi wa Halmashauri unaweza kuwawajibisha wewe mwananchi?
Mbona sasa wabunge wameongezeka kuliko mwanzo?


Mazuri we hujayaona?

Hivi hamjisikii aibu umati wote ule kuwashangaa?
 
Mazuri we hujayaona?

Hivi hamjisikii aibu umati wote ule kuwashangaa?

Mimi siangalii umati, mimi naangalia content ya katiba. Hao waliokusanyika hapo wengi wamesombwa kwa malori, wengine wana maslahi na CCM, na wengine wamekuja kushanga farasi.
Moja ya matatizo makubwa ya nchii ni viongozi kujirundikia mali wananchi wa kawaida kuwa mafukala.

Mfano nimetoa hapo juu.
Mkuu wa mkoa anafanya madudu lakini mwananchi hana mamlaka ya kumwajibisha kwa kuwa yeye ni mteule wa Rais
Wakurugenzi wanaiba pesa lakini wako mwajiri wao ni Waziri mkuu, ambae ni mteule wa Rais
Rais anateua watu wasio na kiwango au marafiki zake anavyotaka yeye bila kudhibitishwa na wabunge
Wabunge wameongezwa zaidi

Haina tofauti na hii ya sasa
 
Kwanza ningependa mnieleweshe rasimu imesema rais wa znz ndo atakua makamo wa kwnza wa rais wa muungano je kama rais wa muungano katokea znz na huyu makamo wa rais nae atatokea serikali ya znz au ni njama za ccm tu kufanya mzanibari asiwe rais wa muungano ?
 
Ingekuwa ni katiba ya wananchi wangeweka ulinzi mzito kiasi hicho?, yaani sehemu kubwa ya polisi wamehamia Dodoma kwa muda, ulinzi mzito kuliko sherehe za Muungano
 
Back
Top Bottom