Nyani aua mtoto

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,854
WATU wawili, akiwemo na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, wakazi wa vijiji vya Nakiu na Njenga Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, wamefariki dunia baada ya kushambuliwa na nyani pamoja na tembo.


Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kikole, Said Ally Mkumbau na Mkuu wa wilaya hiyo, Nurudini Babu, kwa nyakati tofauti walisema watu hao, wamepoteza maisha katika matukio mawili tofauti mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya mchana.

Marehemu hao ni Mayasa Ally Kimbuga (55), mkulima wa Kijiji cha Nakiu na Zahara Khalidi Kulase (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kijiji cha Njenga Kata ya Kikole.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kikole, alimwambia mwandishi wa gazeti hili kwamba mtoto Zahara Khalidi alifarikid dunia mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya asubuhi baada ya kushambuliwa na nyani.

Mkumbau alisema siku hiyo, marehemu akiwa na watoto wenzake nyumbani kwao, kundi la nyani lilivamia eneo la nyumba yao na kushambulia mazao mbalimbali zikiwemo mbaazi, kunde na mtama.

Alisema wakati watoto hao, wakiwafukuza nyani hao, mmoja, alimshambulia mtoto huyo aliyekuwa nyuma ya wenzake kwa kumgawanyisha miguu yake yote miwili, na kumng’ata sehemu ya paja na kufariki papo hapo.

“Wakati watoto wenzake wakiwafukuza kundi la nyani, mmoja alipiga chenga na kubaki nyuma na kumshambulia marehemu,” alisema Mkumbau.

Naye, mkuu wa wilaya hiyo, Babu alisema Kimbuga amefariki dunia baada ya kushambuliwa na tembo mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya mchana, alipokuwa akirejea nyumbani kwake kutoka shambani.

Babu alisema tembo huyo aliyekuwa na watoto alimshambulia mama huyo kwa kumkanyaga, wakati walipokuwa wakivuka barabara

Mkuu huyo wa wilaya alisema tayari askari wanyama pori wamekwenda kijijini hapo kumsaka tembo aliyesababisha kifo cha mkulima huyo.
 
Sijakipenda hiki kichwa cha mada! Yaani moyo wangu baada ya kukiona ukawaka paaaaaaaa......nikasema what? Nimeua mtoto? Haya majina haya....I'm seriously considering switching to just NN....

nyani umeua mtoto?
 
Sijakipenda hiki kichwa cha mada! Yaani moyo wangu baada ya kukiona ukawaka paaaaaaaa......nikasema what? Nimeua mtoto? Haya majina haya....I'm seriously considering switching to just NN....
Ahahahaaaah pole!
 
Back
Top Bottom