Nusura Nitapike!

Nipo hapa Lumumba napata kifungua Kinywa lakini pia naangalia kipindi cha "Tuongee Asubuhi" kutoka Startv. Mwendesha kipindi Pascal Mabuga anang'ang'ania kwamba kwenye Jf wanauponda uamuzi wa CHADEMA kutoka nje ya bunge wakati Kikwete anahutubia bunge.

Kila akieleweshwa kwa upana dhana ya demokrasia na kukomaa kisiasa na wageni aliowaalika, yeye hoja yake kuu kama CHADEMA hawamkubali Kikwete ni kwa nini walienda kuomba kura kwa wananchi.

Kwa kweli nusura nitapike kwa jinsi Mabunga anavyoonekana kuwa kama zuzu kwa lengo tu la kuitetea CCM na Kikwete wake.

Kuna mtu alipiga simu akamwambia huyo mabuga aache kuonyesha yeye ana base upande gani,

Nadhani hili swala baadhi ya watu hawaangali mitazamo ya miaka ijayo wao wanajiangalia leo hii ni kosa kubwa sana haya mambo yanatakiwa yatatuliwe mapema sana na sio kila kukicha ni kuwaomba wananchi ati tunzeni AMANI tuliyo nayo huku HAKI haitendeki ni kujidanganya na kujipalia mkaaa, Wao CHADEMA wanaitaka Tume ya NEC iwe huru, na walituma malalamiko kwa tume kutokana na mapishano ya matokeo ya uchaguzi yaliyo tangazwa na Tume na huku kutoka kwa mawakala nako yako tofauti ni swala la kushughurikia kabla ya kutangaza sasa tume ikatangaza na ikasema ita shughurikia kumbukeni matokeo ya Urais haya pelekwi mahakamani kupingwa sasa hapo tume itashughurikia nini na hata kama ikiundwa tume huru majibu yake ni kuwa tume itavunjwa na kuundwa tume upya na kurekebisha baadhi ya vipengele.

Nadhani sasa imefika wakati wa kutega siasa na ukweli na maisha ya watanzania tuangalie ni jinsi gani tunaiboresha Democrasia iliyo ya Haki na kweli na sio kuikibeba chama fulani tuache fitna hapa.

 
Back
Top Bottom