NSSF Hifadhi House (Social House) Hakuna Umeme

SinaChama

Senior Member
May 1, 2012
109
59
Kwa zaidi ya wiki tatu sasa kumekuwa na tatizo kubwa la umeme katika jengo hili.

NSSF Hifadhi house, ipo makutano ya barbara ya Samora na Azikiwe likitazamana na mnara wa askari.

Jengo hili lipo mahali pazuri sana kibiashara, pia ni barbara maarufu za kibiashara hizi.

Jambo la kusikitisha ni kwamba, hili jengo lina matatizo lukuki pamoja na Mheshimiwa Rais kubadilisha uongozi wa NSSF lakini bado uongozi huo mpya haujaweza kuleta mabadiliko yoyote yanayoonekana katika uendeshaji wa biashara katika jengo hili. Tena naweza kusema kwa sasa mambo ndio yamekuwa mabaya zaidi.

Pamoja na kuandika ratiba ya jenereta kuwashwa kipindi hiki cha umeme. Jana na leo halijawashwe, na siku za week end haliwashwi pia. Hiyo inalazimisha watu ambao wana kazi za ofisini week ends wapete shida ya umeme kama wakija ofisini.

Katika hil jengo kama sio umeme kukosekana kwenye lift, basi ni jengo zima. Au kuwepo kwenye lift na kwenye jengo usiwepo. Haya ni mambo ya kawa ida sana.

Vyoo vinanuka, ukifungua mlango kutoka kwenye lift, vyoo vinanuka choo cha jiji kina nafuu.

Kuna milango ipo kwenye loby area, ambayo inaruhusu watu wa maintanance kufikia mabomba ya maji taka na umeme, iko wazi na kuna mabomba ya majitaka yaliyochakaa yako wazi na baadhi ya wakati harufu inatokea humo badala ya coni.

Hata hivyo tofauti na majengo mengine, wafanyakazi wa ufafi wa chooni hapa, wakishasafisha vyoo asubuhi wanaenda kukaa juu ofisini kwao mpaka siku inaisha. Wakati majengo mengine wafanyakazi wanaingia kila baada ya muda kuangalia kama vyoo ni vichafu na wanasafisha.

Vyoo vya hapa vina Ufunguo. Kila ofisi ina ufungua wa kuingilia chooni. Lakini vinanuka. Sasa jiulize ingekuwa viko wazi ingekuwaje?

Jengo halina maji ya bomba. Miundombinu imeharibika, maji yanafunguliwa asubuhi kusafisha vyoo kisha yanafungwa.

Varanda hazina taa. Usiku huwezi kutembea .

Mchanga umeme ukikatika mnabaki mnatazamana , maana mara jenereta itawashwa, mara haiwashwi, basi mradi vurugu mtindo mmoja.

Inasikitisha kuona tunashindwa kuendesha haya mashirika yakiwa na rasilimali nzuri, nyingi. Ni aibu sana.

Wateja wengi wamehama katika hili jengo. Na hivi karibuni wamepunguza kodi karibia nusu. Lakini kwa utaratibu huu, watu watazidi kuhama tu.
 

Attachments

  • 20180710_132027.jpg
    20180710_132027.jpg
    134.9 KB · Views: 62
Hahahaa nchi ya viwanda. kinacholighalimu hili taifa, hakuna mfumo mzuri wa kudeal na issue. kiongozi anajifanya nyapala anataka aguse kila mahali kitu ambacho hakitalisaidia taifa.
Kukiwepo na mfumo mzuri wa kimaamuzi, mambo yatapiga hatua lkn ohh mara sfari za kushutukiza, utaingia kila mahali na kwa wakati?
 
Back
Top Bottom