Novemba 21: Matola kasome kozi ya CAF A Diploma, usikimbie

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,665
Ni kama vile Suleiman Matola hapendi kusoma hizi kozi bila kujua anajinyima fursa za maana, ndugu yangu Matola, TFF washatangaza hii nafasi nenda kasome sasa we mzee.

Uongozi wa Simba pangeni ratiba kabisa huyu jamaa apewe nafasi akapate cheti hicho, ikibidi hata yule Sebastian Nkoma naye aende akapate hiko cheti.

Tayari una B Diploma malizia tu kipande kilichobaki uwe na A Diploma upunguze aibu ndogondogo kila mara kuambiwa hutambuliki CAF.

diploma a.JPG
 
Duh! Ila kufeli ukiwa mtu mzima noma sana. Sasa hadi watoto wanajua kuwa umefeli. Mwanzo wa mke kukudharau 🤣🤣🤣🤣
kawaida tu waende tarahe 21 waanze tu masomo, simba queens ya nkoma ilikuwa ni nooma hata matola akiwa lipuli na diploma c ikabidi afanywe msaidizi wa amri saidi lakini in reality matola alikuwa ndiye mwenye maamuzi kama kocha mkuu cheti kikawa kinamuangusha
Wote wawili matola na nkoma kazi wanaweza kinachohitajika hapa ni makaratasi ya CAF tu kuondoa kelele
 
Simba imuwezeshe kama Ina mpango nae wa mda mrefu.
kwa kweli hata sebastian nkoma naye pia..kama kutakuwa na mechi za ligi musa mgosi awe msaidizi wa mgunda kwa muda uzuri ni kwamba kama sikosei michezo ya afrika itakuwa imesimama muda huo
 
Watanzania wengi hawapendi kusoma
matola akasome, anaadhirika sana na hiyo diploma b yake , kila ikitokea dharura simba wanahaha mtu wa kukaa benchi mwenye diploma A..mara ettiene hitimana mara mgunda, na akimaliza kusoma asome na kiingereza pia mbona mgunda anajitahidi english?
 
English anaweza hata akajifunza youtube iwapo atapenda
 
Alifeli ...bado anahesabika ana diploma b,ndiyo maana simba queens wameleta kocha mganda kwa ajili ya klabu bingwa huko morroco
Huenda na Matola naye basi anaogopa kuangukia pua, kama huyo kocha mwenzake Nkoma!

Kama vipi mashabiki wa simba waandamane kumshinikiza arudi shule. Siyo mara zote wanamshinikiza tu kuachia ngazi.
 
Huenda na Matola naye basi anaogopa kuangukia pua, kama huyo kocha mwenzake Nkoma!

Kama vipi mashabiki wa simba waandamane kumshinikiza arudi shule. Siyo mara zote wanamshinikiza tu kuachia ngazi.
Hii nafasi ikipita nitajua yeye matola na uongozi wa simba hawako serious na elimu yake...kuelekea december ya world cup michezo hata ya afrika nafikiri inasimama kidogo ,muda sahihi kabisa hiyo november 21
 
Back
Top Bottom