Elections 2010 Nov 2015

Jul 4, 2011
14
6
Je kama Mungu akikujalia uzima na afya tele Novemba 2015 atakapo apishwa raisi mpya utajisikiaje? Je uta huzunika JK kuondoka? Je utafurahia yoyote yule kuingia ikulu ilimradi tu JK anaondoka? Au je una matumaini mengine ambayo ungependa kuona yatumie?

Binafsi mimi nitafurahi sana serikali mpya itakavyo ingia madarakani. Najua bado sijui nani atakuepo madarakani ila naamini Watanzania kwa sasa wamechoshwa vya kutosha kiasi kwamba wao wanataka kuona tu sura zikibadilika.

Japo natambua kila serikali ina mazuri yake na mabaya yake ina awamu hii kiujumla imeshindwa kufanya chochote cha maana na sioni mabadiliko yoyote muhimu yatakayo tokea ndani ya hii miaka minne. Kibaya zaidi ni kwamba hakuna raisi aliyeingia madarakani akibeba matumaini makubwa zaidi kama alivyo beba JK 2005. Hakuna kitu kibaya kama matumaini kuwa juu sana na matokeo kuwa chini sana.

Ila nataka tu kumpongeza JK. Umefanikiwa kutimiza ndoto yako. Umeshaingia kwenye vitabu vya historia kama raisi wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mafanikio yako kama raisi yana anzia hapo na kwa bahati mbaya yanaishia hapo hapo.
 
JK watu walimpenda sana. Unajua kuna msemo mmoja unaopendwa na wanasiasa wa Marekani "Promise little and deliver more." Sasa kwa JK imekua kinyume chake na kuwa "Promise a lot and deliver a little". Anyway miaka hii kumi itakua fundisho kwa taifa na tutajifunza nini vigezo vya kuzingatiwa na vipo vya kupuuzia.

Binafsi nina "fatigue" tayari na hii awamu ya nne. Siku hizi nisha poteza matumaini mpaka chochote ninacho sikia wakisema napuunzia tu kwa maana najua ni lip service. Nasubiria tu muda ufike nione kama tumeelimika au la.
 
Back
Top Bottom