Noti mpya ni Ufisadi mwingine? Nani awajibike?

tatizo kubwa hapa ni ufisadi.NYERERE ALIKUWA ANATANGAZA MWISHO WA MATUMIZI YA PESA YA ZAMANI HALAFU ANATOA MPYA HAPA KWETU SASA KILA MTU INAONYESHA ANAMAMLAKA YA KURTOA PESA AS IF WAZIRI WA FEDHA KATOa yake na mkuu wa kaya nae katoa yake then wakakuta zik mitaaani zote. mambo ya managment
 
Hivi kuna ubaya gani tukichukua style ya noti za zamani kama vile mia nyekundu/ mia ya bluu na kuziapply kwa noti za siku hizi kama vile noti ya 10000? Na ishirini ya zamani kuwa kama 2000 ya siku hizi?- maana style ya pesa ya zamani ilikuwa nzuri sana na quality yake pia
 
Nimekaa najiuliza sana sababu hasa za msingi ni kwanini benki kuu iliamua kuchapisha noti mpya? zipo sababu kadha wa kadha zinazoweza kusababisha benki kuu ichapishe pesa mpya na baadhi ni kama

1.Quality purpuse-labda pesa zilizopo kwenye mzunguko zimekosa ubora, which at this case it seems sio kweli make noti mpya hazina ubora hata kidogo.
2. Control purpose- Labda central bank inataka kukontrol pesa zilizopo kwenye mzunguko (either kuongeza au kupunguza)
3. Inawezekana kuna pesa nyingi sana hazipo kwenye mzunguko so unapobadilisha pesa lazima watu walio na pesa nje ya mzunguko lazima wazilete ili kuziibadilisha which seems it is not serving the purpose nk.

na wakaiingiza pesa lazima itolewe dedline ya pesa za zamani ili mpya ndo zionekane kwenye mzunguko kitu amabacho sio kweli hakuna deadline kinachosemwa ni kuwa pesa ikipelekwa Central bank hazirudi kwenye mzunguko a,bacho naamini ni siasa!

sasa je Govonor wa Bot naomba aautueleze make sasa ni mwaka wa pili tangu pesa ziingiigie kwenye mzunguko lakini cha ajabu tunatumia noti mbili tofauti zinazolingana thamani na zinatumika as a legal tender!

jamani ubabaishaji huu unatupeleka wapi na hasa sababu ya kuprint notes mpya ilikuwa ipi?
 
Pana mengi yaliyojificha, ipo siku tutayajua, me nataka kujua mbinu walizotumia ktk kuipa value shiingi Vs $$$
maana mfumuko ulifika 20%, waliwezaje kuurudisha mpaka 15%?? wakati tunaona nyingi ya nchi kubwa zilizofilisika mpaka na leo imewachukua muda na bado hawajaweza kufufua chumi za nchi zao
 
Pana mengi yaliyojificha, ipo siku tutayajua, me nataka kujua mbinu walizotumia ktk kuipa value shiingi Vs $$$ maana mfumuko ulifika 20%, waliwezaje kuurudisha mpaka 15%?? wakati tunaona nyingi ya nchi kubwa zilizofilisika mpaka na leo imewachukua muda na bado hawajaweza kufufua chumi za nchi zao

formula nyepesi ya kuimarisha pesa ni kuuza zaidi nje kuliko unavyonunua. demand ya dola inapopungua thamani ya local currency hupanda
 
Ndugu wana JF majuzi kati nimestushwa kuona Noti ambazo zinatakiwa zipotee kwenye mzunguko wa sasa zikiwa mpya yaani kitu kinyukri zinangaa na harufu ile yake ambayo ukiinusha lazima upige chafya... chyaaaa!!

Sasa sielewi why zinatoka wapi au Benki kuu wanaendelea kuzifyaua tena kwa kasi maana jinsi Dollar ya kimarekani inavyozidi kwenda juu hadi kwa statics ikifika Dec Dollar Moja ya Kimarekani itafika 2000 au 2200 BOT wakiendelea na kamchezo kao usioeleweka Sababu ya Kuchapisha Noti Mpya za Zamani na Noti Mpya za Sasa.

Hivi Bunge huwa halishilikishwi kutoa uamuzi wa kuchapisha noti Mpya? yaani Wakiishiwa Pesa dawa ni Kuchapisha tu Hii imekaa Fresh kama Zaire ya Mabutu..

Mkaguzi wa Hesabu sijawahi msikia akitoa Neno kuhusu ukaguzi nawasiwasi Noti Mpya zimechapishwa kwa sababu maalum ya Kisiasa.

Naombeni kujua mwenye ufahamu zaidi na hili linatitatiza sana sababu sioni umuhimu wa Kutumia Pesa Za Aina Mbili Tofauti kwa Muda Mrefu sana

Mlaleo,

Naomba nikukosoea kidogo hapo, sio kila ukiona noti mpya umepewa benki ujue kwamba hizo pesa ndio zimetoka kiwandani. Kwa sasa BOT haichapishi noti za zamani, ila zipo noti ambazo zipo kwenye hali nzuri ambazo bado zitatumika hadi hapo zitakapokwisha.Hii nadhani pia ni katika kupunguza gharama za uchapishaji kwa BOT.

Inawezekana kabisa hizo pesa hazijapita kwenye mikono yetu michafu na ya wauza mkaa ndio maana ukaziona mpya. Kwahiyo mheshimiwa usije ukaona noti ina hali mbaya ukafikiri ndio imekaa sana kwenye mzunguko, uchakavu inategemea na mikono mingapi imeishika na nyie washika noti mmezihifadhi vipi.
 
Wadau, naomba kufamu juu ya mwenendo nzima wa Noti mpya, nahisi kama kuna kaharufu ka UFISADI. Sijawahi kusikia nchi yoyote ikitumia noti mbili za kiwango kimoja kwa wakati mmoja. Tuliambiwa zitatoweka taratibu lakini mpaka sasa bado zipo na hizi noti mpya zinaonekana kutokuwa na viwango kabisa kana kwamba zimetengenezwa na Publishers wa kariakoo. Hivi hakuna ufisadi hapo? Kama upo nani anatakiwa kuwajibika/kuwajibishwa?
 
Hivi nani anakumbuka maneno ya majigambo ya ubora wa hizo noti aliyokuwa anayatoa prof. Wakati akizipromote hizo noti?
 
Nashindwa kuelewa Noti mpya zilianza kwa sababu zipi, na kama sababu ziliridhisha kwanini ilishindikana kuleta noti ambazo zipo kwenye viwango, Maana hizi noti sasa zimechakaa mno na hata miaka miwili hazijamaliza, Mbona noti za nchi za wenzetu hazipo hivi, na zinatumika miaka nenda rudi. Mi nahisi kuna harufu mbaya hapa.
 
Noti gani hizi zinatoka rangi kama buku kumi na jelo ni za hovyo sana
 
Wadau, naomba kufamu juu ya mwenendo nzima wa Noti mpya, nahisi kama kuna kaharufu ka UFISADI. Sijawahi kusikia nchi yoyote ikitumia noti mbili za kiwango kimoja kwa wakati mmoja. Tuliambiwa zitatoweka taratibu lakini mpaka sasa bado zipo na hizi noti mpya zinaonekana kutokuwa na viwango kabisa kana kwamba zimetengenezwa na Publishers wa kariakoo. Hivi hakuna ufisadi hapo? Kama upo nani anatakiwa kuwajibika/kuwajibishwa?
Uingereza mpaka mwaka juzi walikuwa wanatumia version mbili za GBP. Sio kitu cha ajabu labda wewe hoja yako ijikite kwenye viwango vya ubora wake na gharama zilizotumika kutengenezea hao mafafa
 
Back
Top Bottom