Nokia 2330

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
KAMPUNI inayotengeneza simu za mkononi duniani aina ya Nokia, imesogeza huduma za internet katika masoko yake mapya kwa kutoa aina mpya za simu zinazowawezesha watumiaji kuwa karibu na ndugu na marafiki zao.
Huduma hiyo inawapa mawasiliano zaidi pamoja na burudani ya uhakika.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Nokia, Alex Lambeek, alisema simu hizo ni Nokia 2330 Classic na Nokia 2720, ambazo zimeunganishwa moja kwa moja na mawasiliano ya internet, huku zikiwa na vifurushi vya huduma za kisasa zitolewazo na watengenezaji wa Nokia kama vile, Ovi Mail.
“Nguvu na uwezo wa mawasiliano ya internet ni vitu visivyoepukika. Tumeshuhudia jinsi teknolojia ya simu za mkononi ilivyo chachu ya ukuaji wa sekta isiyo rasmi duniani, ikiwawezesha wajasiriamali, huku ikiwa na umuhimu mkubwa na wa kudumu kwa maisha ya watu.
‘‘Huduma kama Ovi Mail ambayo imeunganishwa kwenye simu tunazozizindua leo hii ni moja ya vyanzo na milango ya ufahamu na burudani pasipo kuhitaji kuwa na kompyuta,” alisema Lambeek.
Alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa kwa wateja wa bidhaa za Nokia, karibu nusu ya wateja kutoka katika masoko mapya ya Nokia, wanapendelea kutumia internet iliyopo kwenye simu na si ile inayopatikana kwenye kompyuta za kawaida. Lambeek aliongeza kuwa wakati watu wakiendelea kutegemea simu kwa kutuma ujumbe wa maandishi na sauti pekee, simu za Nokia zenye internet zinawapa watumiaji huduma zote za mawasiliano zinazopatikana kwenye simu na kwenye kompyuta kwa wakati mmoja. Lambeek alimalizia kwa kusema: “Kutokana na jinsi Kampuni ya Nokia inavyowajibika katika masoko yake mapya, wateja wa simu za Nokia sasa watakuwa na uhakika wa kupata bidhaa za Nokia zilizo bora na za viwango vya hali ya juu. Hii ni muhimu sana kwa maeneo ambayo huduma za msaada na ushauri wa kiufundi hazipatikani kwa urahisi.”
 
Back
Top Bottom