Nmemwambia Mpenzi wangu aweke TV Yake bond ndo nimkopeshe pesa

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,292
Habar wakuu,
Kipind flan Nilipata dili la kusambaza mizigo Ofsini alikoajiriwa mpenz wangu, Baada ya malipo kufanyika wakapungukiwa pesa kiasi flani ya kulipia makufuli ya milango yao.

Wakaomba niwapatie makufuli waende nayo ila hiyo pesa italipwa baadae boss akishafahamishwa kua kulikua na mabadiliko kwny order yao, makufuli yalisahaulika kupigiwa hesabu kwenye Order ya mwanzo. Nikasema sawa haina shida.

Ila Nikawaambia siikopeshi ofisi Bali namkopesha mtu binafsi, biashara ya kudaiana na ofisi skuhizi sifanyi mimi. Jichagueni Ni Nani Deni hili nimuandike,ili shughuli ya kudiana iwe Kati yangu na yeye, sio Tena ofisi.

Basi mpenz wangu ndo akajiweka dhamana kua Ni uhakika ile pesa italipwa, jina la Deni nimuandike yeye.
Kwenye Daftar langu la madeni nikamuandikia mpenz wangu Deni la 80,000.

Aisee Lile Deni limekaa MDA mrefu sana kila nikimuuliza mpenz wangu anasema hiyo pesa haijatoka. Akipewa na boss atalilipa TU haina shida.
 
Siku nmekutana na boss wao nikamfahamisha kua nawadai pesa ya makufuli ofsin kwao, boss akasema anajua ila mbona iyo pesa ishalipwa MDA mrefu Sana, Tena siku Iyo Iyo makufuli yamefungwa mpenz wangu alipewa iyo pesa aniletee.

Nmerud kwa mpenz wangu namwambia anabisha hajapewa pesa, nikamwambia taarifa hizi nmepewa na boss wako mwnyw, Kama unabisha nimpigie hapa hapa ukatae ukupewa pesa yangu uniletee.

Akasema Basi yaishe usimpigie, Iyo pesa Kweli nilipewa na boss ila nilitumia kwenye mambo yangu. Nikamuuliza sawa, kwaiyo Iyo pesa unanipatia lini. Akasema Iyo pesa sikulipi maana mimi Ni mpenz wako, haustahili kabisa kunikopesha na kunidai pesa ndogo Kama iyo.

Nikamwambia iyo pesa Ni ya biashara, kwenye biashara hakuna pesa ndogo, hizo sio pesa binafsi, lazima irudi ili niendeleze mzunguko wangu, mpenz wangu Kakataa kata kata kurejesha ile pesa na kusema liwalo na liwe HALIPI.

Basi nikamwambia biashara ya kukopesha mimi na Wewe,leo ndo mwisho maana umenidhurumu na huheshimu Makubaliano na hujui kutenganisha biashara na mahusiano. Akasema utajua mwenyewe, Mimi Hilo Deni silipi ng'oo. Nikasema "POA".
View attachment 2687796
 
Jana kanitaarifu kua kapata likizo kazin kwake na inatakiwa kuanza tar 23 mwezi huu hivyo atapaswa kusafiri Kwenda mkoani kuwasabai wazazi wake. Nikasema sawa,Jambo la heri.

Leo ananipigia anaomba nimkopeshe LAKI 2 wkt wa kukabidhi ofisi kakutwa na shoti ya 220,000 kwenye mahesabu Yake. Nikamwambia kumkopesha ni ngumu maana akikopeshwa huwa halipi, anachanganya mahusiano na biashara.

Kasema sahv uhakika akikopeshwa atarejesha pesa yangu atakapolipwa pesa yake ya likizo tar 23 mwezi huu.

Nimempa sharti moja kua ili nimkopeshe LAKI 2 na 20 atapaswa alete tv yake ikae BOND dukani kwangu, ili akishindwa kulipa deni tusibembelezane, Bali naiuza moja kwa Moja ili kufidia Deni langu. Kasema sawa haina shida.

Pia nikampa sharti jingine kua anaporejesha Iyo laki 2 na 20 atapaswa pia alipe na Deni lake la nyuma 80,000 la makufuli ili ajijengee uaminifu Tena. Maana ake atapaswa kunilipa jumla laki 3 taslimu iyo tar 23 alosema atalipa.

Hapa kagoma kata kata kua Hilo Deni lake la nyuma yeye halipi na halihusiani kabisa na hili deni, nami nmemwambia Kama hawezi hayo masharti nilompa Basi akakope kwingine, Huenda uko atakua serious kuwalipa na sio kwangu maana ananichukulia POA. Kasema sawa.

Nawasilisha View attachment 2687790
 
Nawasilisha View attachment 2687790View attachment 2687791
Mwambie na Kodi ya meza inafutwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom