Njooni tushare ideas, kati ya kununua trekta au bajaji kipi ni kitega uchumi kizuri?

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
4,020
5,439
Amani ya allah iwe juu yenu.

Katika harakati za maisha, watu wanapambana sana ili kuona wanajikwamuaje katika dimbi la umaskini.
Kila mtu kuna kitu anafikiri ni bora zaidi akikiweka kwenye kitega uchumi, basi kitampatia mafanikio mazuri.

Basi nami niko kwenye tafakuri kubwa, kati ya trekta na bajaji ni kipi bora zaidi?

Njooni tupeane mawazo na uzoefu.
 
- Swali: Je kwa "investment Capital" ya TZS ngapi?, dimaa

Jibu ya hili swali litasaidia wadau kukupa mchanganuo na pendekezo stahiki.

Ila tambua hakuna kitega uchumi ambacho kizuri au kibaya
Kwenye 20m, uzuri ninao manisha ni mzunguko wake na profit yake
 
Bei ya chini zaidi ya tractor inaweza kuwa 40,000,000 ambapo ukiwa unakodisha inaweza kukuingizia shilingi 40,000 faida kwa ekari 1 baada ya kutoa gharama za uendeshaji.

Ukilimia ekari 1000 kwa Mwaka ina maana utaingiza 40,000,000 faida baada ya miaka 2 hela yako ya mtaji na faida inakuwa imerudi. Hapo sijapiga gharama za kusomba mizigo n.k

Milioni 40,000,000 kwa bei ya Bajaji kwasasa utapata Bajaji 5 na iwapo itakuingizia 30,000 kwa siku ina maana kwa mwezi utaingiza 30,000x5@30=4,500,000

Ambapo utaingiza 54,000,000 kwa Mwaka.

NB; Upande wa Bajaj sijapiga factor ya Kutoletwa hela ya kipande kwa siku maana Vijana wa Bajaj wote kama wanafanana kwenye usumbufu wa hela, ajali n.k

Binafsi ningeenda na mradi wa Tractor maana risk zake ni Chache kuliko Bajaji
 
Swali la ajabu kweli. Unalinganishaje Bajaj na tractor, au ukute unasema power tiller wewe?
Kwanza uko mbali na eneo unalotaka kufanya uwekezaji. Uko Mwanza unataka uwekeze Dar na Dodoma ni bora uchukue tractor kama hela ipo. Litadumu na kurudisha hela bila usumbufu mkubwa kuliko bajaj.
 
Changamoto inaweza kuwa trekta nazo zimekuwa nyingi sana siku hizi, kufikisha ekari hizo 1000 ni ishu kwa mwaka.
 
Swali la ajabu kweli. Unalinganishaje Bajaj na tractor, au ukute unasema power tiller wewe?
Kwanza uko mbali na eneo unalotaka kufanya uwekezaji. Uko Mwanza unataka uwekeze Dar na Dodoma ni bora uchukue tractor kama hela ipo. Litadumu na kurudisha hela bila usumbufu mkubwa kuliko bajaj.
Nalinganisha mzunguko wa pesa mkuu, ila shukrani kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom