Povu la nn kamanda, kama una hasira si uandamane??Tunamtaka Magufuli mwenyewe na ahadi zake hewa
Ukuanza na kuhama kwa nyalandu mpaka tetesi za nape,kuna kitu kinakuja.Malengo ni maendeleo kweli au mbio za urais zimeanza ?
Natamani hili swali liwe ndo la kwanza kuulizwaImepita miaka mingi nyumba ya mama Lwakatare haijabomolewa pamoja na NEMC kutoa notisi ya kuvunja nyumba kwa sababu za kimazingira ambapo inadaiwa ujenzi wake unazuia mto Numbwi na uko jirani na Mikoko, wizara imefikia wapi? Hawaoni kwamba watu waliobomolewa wanajisikia vibaya pamoja kuwa walikuwa na zuio la mahakama kama mama Lwakatare?
Na pia huyo mama ni "mpiga kura wake"Unaota wewe. Hilo jengo halitakaa liguswe maana hata Magufuli kamteua huyo mama kwa moyo safi kuwa Mbunge viti maalumu.. Kuna watu na viwatu!
Ameshindwa kuondoa mifuko ya plasiki Sasa tunashuhudia madaraja yakibomoka kutokana na uchafu wa maplastiki.
Kwa ushirikiano wa karibu na JamiiForums, tunatarajia kuanza kwa kipindi kipya kiitwacho 'Njoo Tuongee' ambacho kitahusisha mjadala na Mawaziri kutoka Serikalini kuhusiana na masuala ya wananchi.
Kwa muda wa wiki 7, Mawaziri mbalimbali watawekwa 'Kitimoto' LIVE kupitia Star TV ili kujibu maswali kutoka kwa wanaowaongoza.
Kipindi cha kwanza kitaanza kurushwa kesho (Ijumaa O3, 2017), SAA 12:30 JIONI na Waziri tutakayeanza naye atakuwa ni Mheshimiwa January Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira.
Lengo kuu la kipindi hiki ni kuwapa nafasi wananchi kujua wanachokifanya Mawaziri na kuwauliza ni wapi wanakwama katika kutatua changamoto mbalimbali.
Sasa kupitia JamiiForums, unaweza kuuliza maswali au kutoa maoni ambayo baadhi yao yatakayopata nafasi, yatakusanywa na kuwasilishwa kunakohusika kisha kuulizwa moja kwa moja kwa mgeni wa siku hiyo.
Je, una swali, maoni, jambo lolote unataka kuliwasilisha kwa Ndg. January Makamba?
Karibu sana..
hili swali hujui jibu lake?Kuna miti inachomwa na kukatwa hovyo. Huyu makamba anasaidiaje?