Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo Januari 22, 2024 Wilayani Makete Mkoani Njombe katika ziara ya kikazi na kukagua utekelezaji wa mradi huo ambao upo nyuma kwa mujibu wa mkataba.
“Natoa wiki tatu kuanzia sasa vifaa na mitambo yote inayohitajika pamoja na wataalaam wa usimamizi wa mradi wawe hapa, hawa Wananchi hawawezi kusubiri wataalamu wapo likizo China wakati sisi shida yetu ni barabara,” amesema Bashungwa.
“Tunaposaini mikataba, nataka mikataba isimamiwe, namuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kusimamia kitengo kinachoshughulikia mikataba na kama wameshindwa kufanya kazi basi fukuzeni wote”, amesisitiza Bashungwa.
Ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta Bilioni 82 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kutokana na umuhimu wa wananchi wa Wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe katika kuleta maendeleo na kuinua uchumi wa wananchi.
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa amepokea maombi ya kuunganisha Wilaya ya Makete na Busokelo mkoani Mbeya na tayari usanifu unakwenda kuanza kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe.
Naye, Mbunge wa Makete, Festo Sanga ameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwani ni kiungo muhimu kiuchumi kati ya mkoa wa Njombe na Mbeya.
Akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Jephason Nko, ameeleza kuwa mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 4.2 ambapo unasimamiwa na Kitengo cha TECU kutoka wakala huo huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2026.