Njia mbali mbali za kutoa ushahidi Mahakamani

Apr 26, 2022
69
104
Ushahidi Mahakamani (kwenye kesi za madai) unaweza kutolewa kwa njia ya mdomo (orally) au kwa njia ya maandishi (witness statement). Rejea Order XVIII (2) (1) ya CPC (amendments za mwaka 2021).

Sasa, ukiomba kwenye kesi yako utoe ushahidi kwa njia ya maandishi (witness statement), ukakubaliwa alafu ukashindwa kuleta huo ushahidi kwa wakati Mahakamani, hiyo tafsiri yake kisheria ni sawasawa na shahidi kushindwa kufika Mahakamani, na matokeo yake ni kwamba kesi yako itafutwa na kwa sababu kwa kutoleta shahidi unakuwa pia umekiuka amri ya Mahakama.

Hii ni kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye kesi ya FAIR DEAL AUTO PVT LIMITED Vs CITY BOYS ELECTRONICS CO. LIMITED, CIVIL CASE NO. 187 OF 2019.
 

Attachments

  • FB_IMG_1714574948480.jpg
    FB_IMG_1714574948480.jpg
    95.5 KB · Views: 6
Back
Top Bottom