njia ipi atashika Magufuli?

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Mtawala yeyote mpya hususan kwenye Vyama vya Siasa kiritimba ( dominant parties ) huchukua njia moja kati ya mbili ili kudumu kwenye madaraka. 1) kujikita kwenye kutekeleza matakwa ya Chama kilichomweka madarakani kwa kukubali kuwa kwa njia hii Chama hicho hakitamwondoa/mpindua na hivyo kutawala bila shida. 2) Kupunguza nguvu za Chama na waliomweka madarakani. Mtawala anayechagua njia (1) atatawala kwa mashaka muda wote na ataishia kuwa kibaraka wa Chama chake. Akichukua njia (2) wenzake wa Chama chake watajaribu kumzuia kwa sababu wanajua maslahi yao yataguswa akifanikiwa. Hivyo mwanzoni mwa utawala wowote mpya kunakuwa na harakati nyingi za kugombania madaraka.

Maelezo haya ni tafsiri isiyo rasmi ya Mwanazuoni Stephen Haber. Tanzania ipo kwenye mpito huu unaoelezwa na mwanazuoni huyu na ni dhahiri kuwa Mtawala mpya amechagua njia ya pili ili aongoze kwa maono yake. Hata hivyo swali muhimu sana kwa wanasiasa, hasa Sisi Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani, na kwa wachambuzi wa Siasa ni - Mtawala mpya ana/atatawala na Nani? Tutajibu swali hili kwa kumsoma Louis XIV wa Ufaransa ' hakuna anayetawala peke yake; hakuna mwenye mamlaka ya mwisho peke yake. Maslahi ya makundi na Nani anapata nini ndio huwezesha Mtawala kufanikiwa ama la'. Hatuna budi kwanza kujua ' kundi Lina/Litakalotawala ' ni lipi na maslahi yao yanashughulikiwaje. Baada ya hapo itawezekana kuunda mbinu na mikakati ya kukabiliana na Mtawala.
Ni dhahiri Siasa zile zile za miaka na miaka hazina nafasi tena. Ni muhimu kujipanga upya ili kukabiliana na changamoto mpya za kujenga na kuimarisha demokrasia nchini. Siasa zitakazoshinda ni Siasa za majawabu ya kero za wananchi na zinazokonga nyoyo zao bila kuvunja misingi.
 
( from readings, comprehensively ) A new Ruler may then do one of the three 1) terrorizes the leadership of the party that launched him to power or 2) co-opt the leadership of the party that launched him to power or 3) creates a rival or complimentary party.
Based on the experience of previous months, In the next few months if not weeks we will observe the above options and how it plays in Tanzanian body politic.
 
Back
Top Bottom