Maimu ndio mwekezaji alienunua Ardhi ya wana Njedengwa

eviction order
Demotion order
Hz zote order zitatumika kwa wafuatao bila kuvunja wala kuathiri vifungu vya sheria vingin
Wananchi wasiojiweza
Wananchi wenye kipato cha chini.
Wananchi wasiojua haki na sheria za nchi.
Mahakama itaamua pale tu mwekezaji atakapo kuja na MIHELA MINGI.
 
Japo sijaona makaratasi, lakini naamini Maimu atakuwa ameshinda kesi, eviction order ikatolewa, demolition order pia ikatolewa na ndio maana vyombo vya dola vikatumika.

Pasco, ukisoma magazeti ya leo kuna gaps nyingi sana ambazo zinahitaji maelezo ya Kina.

1. RPC hajui kuhusu hii sakata

2. Zoezi limeanza saa nane na nusu usiku Amri za mahakama hazitekelezwi njee ya saa za kazi for reasons which are obvious

3.Polisi walipiga risasi na mabomu, was it necessary kutumia mabomu na silaha za moto kwenye kutekeleza amri za madai za mahakama

4.Baadhi ya watu wamekamatwa na polisi na kuwekwa ndani- kwa kosa gani na nani ni mlalamikaji

5. Madalali walificha nyuso zao, wafanyakazi wanaofanya kazi za serikali kila siku wanafanya kwa uwazi bila kujificha ili chochote kikitokea kuwe na uwajibikaji

Nadhani uchunguzi wa kina unahitajika
 
Pasco, ukisoma magazeti ya leo kuna gaps nyingi sana ambazo zinahitaji maelezo ya Kina.

1. RPC hajui kuhusu hii sakata

2. Zoezo limeanza saa nane na nusu usiku Amri za mahakama hazitekelezwi njee ya saa za kazi for reasons which are obvious

3.Polisi walipiga risasi na mabomu, was it necessary kutumia mabomu na silaha za moto kwenye kutekeleza amri za mahakama

4.Baadhi ya watu wamekamatwa na polisi na kuwekwa ndani- kwa kosa gani na nani ni mlalamikaji

5. Madalali walificha nyuso zao wafanyakazi wanaofanya kazi za serikali kilasiku wanafnya kwa uwazi bila kujificha ili chichote kikitokea kuwe na uwajibikaji

Nadhani uchunguzi wa kina unahitajika
Kaka wamesema humu jamvin huo mchezo wote ni Uwepo wa mikono ya AGREY MWANRI.
 
Yes ni Calvin Maimu.
Yeye ni mwekezaji mzawa, amepewa eneo hilo kihalali kwa ajili ya uwekezaji.
Wakati alipopewa hakukuwa na wananchi ndani ya mipaka yake ila wananchi walishajitwalia maeneo ya jirani.
Alipoanza kujenga ukuta kulizungushia eneo lake, ndipo wananchi jirani nao wakavamia kwa ujenzi.
Zikufuatia danadana za mahakamani, mahakama ikimpa haki mmiliki, huku wakazi wakiweka zuio na kukata rufaa huku ujenzi ukiendelea na wananchi wengi zaidikujitokeza ili kuweka 'human shield'.
Japo sijaona makaratasi, lakini naamini Maimu atakuwa ameshinda kesi, eviction order ikatolewa, demolition order pia ikatolewa na ndio maana vyombo vya dola vikatumika.
Kwa wenye kumbukumbu, hii sio mara ya kwanza kwa ubomoaji wa aina hii, ulifanyika kwa Wakazi wa Loliondo na Waamasai wa Ngorongoro ambao wao walichomewa nyumba zao wengine wakiwa ndani. Uhamishaji wananchi kwa mtindo huu pia ulifanyika bonde la Yaeda Chini na kuwahamisha wananchi waliovamia msisitu wa Kazi Mzumbwi na hata wakazi wa eneo la Kipawa.

Nasisitiza binafasi siungi mkono matumizi ya nguvu zilizipitiliza kiwango na umwagaji damu, iula lazima tufike mahali, Watanzania tuzingatie sheria, taratibu na kanuni.
Pascal usiongee kitu usichokijua Maimu ni kawaida yake kufanya hivi na akilipenda atakuondoa at any cost kama anavowinda eneo la shule ya Nuru pale Ipagala, huyu jamaa ana mabavu na ubabe......
 
Pascal usiongee kitu usichokijua Maimu ni kawaida yake kufanya hivi na akilipenda atakuondoa at any cost kama anavowinda eneo la shule ya Nuru pale Ipagala, huyu jamaa ana mabavu na ubabe......
Mimi nimefanya Documentary hapo, matatizo ya ardhi Dodoma ni makubwa, wakati CDA ikichukua maeneo, wenyeji walitatoa bure bila fidia kwa sababu yalikuwa mapori. Maimu ndio mwenye makaratasi. Kunapotokea mgogoro wowote wa ardhi kati ya aliyepo na mwenye makaratasi, kisheria mwenye makaratasi ndiye mshindi, na aliyepo hugeuka mvamizi.

Huu mgogoro ni wa muda mrefu, kesi zimeendeshwa kwa miaka. Hata wanaomtaja Agrey Mwanri, wanachapia tuu kwa sababu Mwanri kaja juzi, labda kwa vile Maimu na Mwanri wanatoka kijiji kimoja kule Sanya Juu, labda Mwanri kaweka tuu mkono kumsaidia homeboy wake.

JF ni ukumbi wa kuelimishana, akizungumza mtu na kumwambia hajui chochote, sasa wewe unaejua ndio sema unachokijua.
P
 
Kumbe huyu Marehemu Calvin Itael Maimu ndiyo fisadi hivi? Zulumati? Sasa jana alikuwa kwenye jeneza ameondoka na nini zaidi ya sanda? Tujitafakari mno kabla hujadhulumu mtu. Kisa cha hilo eneo au ardhi na mgogoro wake sielewi ila inaonekana alitumia nguvu kubwa mno kunyanyasa hao wagogo maskini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom