ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Aliyekuwa Mbunge wa Igunga Dr. Dalaly Peter Kafumu kwa tiketi ya "Magamba"(CCM) ambae alivuliwa Ubunge na Mahamaa Kuu Kanda ya Tabora mwezi Agosti, 2012, pichani juu kulia, "amefumuka" kwenye Kipindi cha Medani za Siasa kinachorushwa na STAR TV na kusema kuwa anatarajia kushinda kwenye Rufaa kuhusu kutenguliwa kwake ubunge kutokana na sababu zilizotolewa na JaJi wa Mahakama Kuu kuwa dhaifu na hazimuhusu yeye.
Kafumu amesema sababu hizo ni pamoja na: (i) yeye kuhusishwa na vurugu zilizopelekea aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Igunga Fatuma Kimario kuvuliwa Hijab na wafuasi wa Chadema jamba ambalo haoni kuwa na mantiki kwani vurugu zilihusisha vyama vyote CDM, CCM na CUF na kwake hajaona ni kwa nini ahusike moja kwa moja ; (ii) kitendo cha Magufuli kutoa ahadi ya Daraja wakati hizo zilikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na yeye hakuhusika kutoa ahadi hiyo na (iii) ni Wananchi kugawiwa Mahindi ya njaa wakati wa Kampeni za Uchaguzi, jambo ambalo kwake anasema linaihusu Serikali zaidi na sio yeye binafsi na kuwa mgao huo ulianza kabla ya kampeni kuanza na kuwa ulilenga kuwanusulu wananchi na janga la njaaa ambalo Mahakama ingepaswa kuona kuwa ulifanyika kwa nia njema.