Mwaka huu tumejaliwa kupata mgombea bora kabisa katika kiti cha uraisi naye ni Dr. Silaa., Ana kila sifa ya kuwa raisi wa nchi yetu. Mpaka sasa hakuna mtu au chama ambacho kimeshasema udhaifu au ubaya wa Dr. Silaa tangu akiwa kiongozi katika mashirika ya kidini mpaka ubunge na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa. Hakuna awezaye kupinga maendeleo ya karatu chini ya uongozi wake. Dr. Silaa amesimamia vizuri kabisa hesabu za serikali za mitaa. Asingekuwa silaa na wenzake nani leo angejua ufisadi uliofanywa na CCM. Umewahi kuona wapi kiongozi anasema mshahara wangu mkubwa inabidi upunguzwe ili na wengine wafaidike!! Lakini ni Dr. Silaa alidiliki kuutangazia umma jambo hilo. Ni Dr. Silaa ambaye amehaidi kubadilisha Katiba akiweka wazi kwamba Raisi ana madaraka makubwa mno, na haiwezekani hatima ya watu mil 40 ikawa tu chini ya mtu mmoja. Dr. Silaa afanye nini ili watanzania mjue kwamba tumejaliwa kupata mtu makini baada ya kulia kwa miaka mingi? Watu wanaompinga Dr. Silaa wanampinga kwa lipi baya alilofanya?
Ukija kwa kikwete ni ukweli usiopingika kuwa mafisadi ndo watu wanaomsupport na hata serikali yake ilikiwa kupambana na mafisadi ni kazi sana, alipokuwa mawziri wa nishati na madini alisign mikataba mingi mibovu.
Sielewi wanaomsifia kikwete wanamsifia kwa lipi? wanaagenda gani? Je wanamacho lakini hawaoni? wanamasikio lakini hawasikii?
NITASHANGA WATANZANIA WAKIMKUBALI KIKWETE NA KUMKATAA DR. SILAA. NASEMA TENA NITAWASHANGAA SANA WATANZANIA