Nitamdai vipi hela ndugu yangu?

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,475
9,928
Ni dada yangu wa mama mmoja ila baba tofauti. Namdai milioni 1.5. Mwaka jana Octoba kuna mishe nilifanya jamaa niliefanya nae kazi Disemba mwishoni akaleta hela home milioni 1.5 ila nilikua nimesafiri kwa sababu anamjua sister akampa ile hela. Sister akaipiga akauchuna.

Nilivyorudi mwezi wa kwanza nimefatilia malipo yangu kwa jamaa ndio akaniambia hela alipeleka home.

Kuulizia home sister kasema ni kweli alipokea iyo hela mambo yakaingiliana akaitumia kwaiyo atanirudishia mwezi wa 3. Mwezi wa 3 ukaisha hajalipa nikaulizia akanipiga sound za kujilizaliza tu.

Ooh baba angekuwepo angenilipia sijui nini nini.. Mpaka leo hajanilipa chochote na wala sioni kama ana mpango huo.

Najua hawezi kulipa kwa mara moja lakini hata kupunguza kidogo kidogo tu hakuna.

Nilijaribu kuwashirikisha wakubwa jibu nililopewa nimeambiwa nimuachie Mungu tu.

Kiukweli hela yangu inaniuma sana mbaya zaidi am jobless kila nikikosa mchongo wa kunilinda hata kwa siku moja tu naikumbuka hela yangu. Bora ningekua na kazi ningeipotezea tu iyo hela.

Nitadai vipi hela yangu hata kwa njia aggresive kidogo? Ana mpango wa kufungua saluni, kuna vifaa vyake vya saluni pale home anapoishi mpaka sasa ninachofikiria ni kwenda kuvichukua ivyo vitu wakati hayupo halafu niiuze kufidia hela yangu.
 
Ndugu wana lostisha sana... mimi kuna kaka yangu wa damu baba mmoja mama mmoja ila hata akinikopa buku sahiv simpi.

Maana mimi nina udhaifu wa kumuamini mtu, alishanikopa elfu sitini akasema atanipa chap alikuwa amekwama kidogo..

Ni mimi sipendi kumkumbusha mtu deni, sasa akajisahaulisha kwamba namdai, hiyo siku amekuja anataka nimkopo elfu kumi sijui usiku luki imeisha, nikamuambia sina kitu.

Akaniambia fanya hata buku, nikamuambia aisee sina.

Nimeamini ndugu wa kweli ni mzazi wako na kidogo mkeo na watoto... hao wengine ni watu watakuja kuwa na life lao na nyumba zao.

Kuwa makini na ndugu kuliko kitu chochote
 
Walikujibu Muachie Mungu?..na wewe hutaki?
Mkuu hali ya kimaisha ninayoipitia ilo jibu la kumuachia Mungu halikunitosheleza kabisa mkuu. Kuna siku ambazo nashindia maji tu nakosa hata hela ya kula, nishakosa kodi ya geto karibia mwenye nyumba anitimue kwake, sometimes inafika zamu ya kutoa hela ya umeme au inaletwa bill ya maji mfukoni sina chochote halafu naambiwa milioni 1.5 nimuachie Mungu tu, sio rahisi kuelewa jiweke kwenye nafasi yangu
 
Nashauri mwambie unayopitia kuhusu yeye kuchelewesha deni lako mwambie unapitia magumu mpe mwezi tena..baada ya hapo usimkumbushe tena...Hii atajifumza
Kwa jinsi nilivyomsoma sioni kama ana mpango wa kunilipa ndio maana nafikiria kutumia njia aggressive kidogo, lakini nitafanya kwanza kama ulivyonishauri
 
Back
Top Bottom