Nisaidieni niokoe maisha ya Kijana huyu

elimumali

Senior Member
Jan 13, 2010
149
8
Nina mtoto wa jamaa yangu wa karibu anatumia madawa ya kulevya muda mrefu – miaka kumi. Katika kipindi chote hicho, Mzazi wake (Mama) kamsumbukia sana kupata suluhu ya kumfanya aache madawa mpaka sasa hajafanikiwa. Kusumbuka huko ni pamoja na matibabu (detoxification), Maombi mbali mbali, Ushauri nasaha (councilling), nk. Athari zake zimekuwa kubwa, anajidunga sindano na mishipa yake sasa imekuwa tabu kupatikana. Alishapelekwa Lutindi (Korogwe) ambako ndiko panaaminika kuwasaidia vijana hawa mara tatu, lakini bado hali ile ile. Yeye mwenyewe anaonyesha nia ya kuacha, lakini anasema mwili unamuuma sana anapojaribu kuacha. Wanafamilia walimshauri kuwa suluhu ni kumpeleka Rehabilitation Centre inayoaminika kwa muda mrefu akae huko. Hapa Tanzania Rehabilitation Centre inayoweza kuwadhibiti na kuwatibu vatu hawa iko papi? Naomba ndugu wapendwa anayejua anielekeze nimsaidie vipi mtoto wa ndugu yangu.
 
sidhani kama anaitaji hilo tu,jaribu kumpeleka maeneo ya ubungo mwenge jengo refu sana.wasiliana na number 0653425930 atakuambia wako wapi uongee na muhusika ni clinic inayosaidia mambo mengi na hilo ni majour.
 
Back
Top Bottom