Nisaidieni nifanye biashara gani? Nina mtaji wa 3,000,000/=, nipo Himo-Moshi

Mnashauri vema, lakini hamtoi vigezo vya msingi ktk uanzishwaji wa mradi husika, so many things to take care when starting a new business; NI kweli ufugaji unalipa, au kilimo, au uuzaji wa vyakula/nafaka, au vipodozi au pikipiki nk!! lakini mimi nahitaji apewe ushauri kitaalam zaidi ili mwisho wa siku Aanzishe biashara kati ya hizo mlizo shauri kutokana na vigezo vya kimazingira, kiuchumi na kijamii. Asisahau pia kuwa na Business Plan!
 
The best Idea ya Biashara inatokana na wewe mwenyewe, Unless mleta maada awe ni kipofu, kiziwi, na hata bubu na hajawahi tembea, kabisa,

Na mafanikio yoyote ya Biashara huanza na Idea, Idea ndo hubeba biashara yako ndo itakayo determine mafanikioa au kuto fanikiwa, sasa kama mimi siwezi jua ni fanye nini, hata biashara vilevile sitaweza kufanya, na kushindwa katika biashara huanzia kwenye wazo na si mahali pengine popote pale

Nawashangaa watu wanao kuja na ushauri mara fuga, mara hoteli, Hivi mimi niko Arusha, halafu na mshauri mtu alieko mbeya kwamba Afungue hoteli, inawezekana vipi? Je mimi nafahamu fika mazingira na ya huko? triends ya huko naijua? je Competition naifahamu vyema? Wakuu tuwe siriasi ,make hapa watu ni kupotezana badala ya kusaidiana, ni kichekesho sana,

Na mafanikio yoyote katika biashara huanza na juhudi zako bianafisi, ikiwemo kuumiza kichwa kutafuta wazo la biashara ambalo ni bora kabisa na ambalo linabeba feature yako ya baadae, problems ni kwamba watanzania hawataki kuumiza vichwa that is why Biashara za watanzania zinafanana Nchi nzima, P-PESA, STATITIONARY, BAA, HOTELI, DUKA LA JUMLA NA REJAREJA, KUUZA MITUMBA, SALOON, KUNUNUA TOYO, hizo ndo idea zetu, na that is why watu wanishia kwenda kwa waganga na kukata mikono ya alibino ni kutokana na haya, ubunifu wetu ni negative,

Unapo fikilia kuanzisha hata hiyo M-PESA, jiulize je baada ya miaka 10 hadi 15 nitakuwa wapi na hii M-PESA yangu?

So IDEA iliyo bora kabisa inatoka kwako wewe mwenyewe, na that is why unapo kuwa na Idea yako na ukaanza project mfano ya Ufugaji, unatakiwa uwe msimamiz mkuu kwa sababu wewe ndo mwenye idea na wewe ndo unaye jua malengo yako, sasa inapelekea mtu anawazo zuri sana la biashara na kinacho fuata baada ya kuanza ni kuweka Mke/ mme. shemeji, sijui Mjomba, sijui Mchumba, mara binamu, mara Baba mdogo. mwisho wa siku ni biashara kuto kukua au hata kufa kabisa, kwa sababu wewe initiator wa idea umeshindwa kusimamia idea yako na umebakia kuongoza kwa Limoti control
 
Fanya biashata mbayo itahitaji ujuzi wako
Fungua tution center

Au funguq nusery center
 
Mawazo ya wanajamii ni mazuri. JARIBU BODA BODA!!!!

Nunua piki piki 2 tbeter au yoyote ya kichina Bei moja ni milioni moja na laki nne 1.4
nakushauri ununue mbili so ni milioni 2 na laki 8

tafuta vijana wawili waaminifu wafanye boda boda kwa siku ni elfu 10 so kwa mbili ni elfu 20

easy money japo zipo nyingi huwezi lala njaa. kwa wiki unaingiza laki 140 mara wiki 4 so

kwa mwezi laki 5 na 60:

here is how:

kwa siku 10,000 * 2 =20,000

kwa wiki 20,000 * 7 =140,000

kwa mwezi 140,000 * 4= 560,000

kumbuka service ni elfu 50. ikipata ajari kuirekebisha vifaa na spea haizidi elfu 50

pia usisikilize maneno ya watu kwamba zipo nyingi sababu ili ufanikiwe ni lazima uwe RISK TAKER. pia wakisema zipo nyingi jua kuwa kwenye vingi ndio pana mengi more faida i mean.

Nielimishe kidogo,
1. unataka kuniambia kuwa boda boda inaingiza si chini ya 10,000 kwa siku?
2. Mbona katika hesabu zako hukuweka malipo ya dereva wako?
3. Gharama za petroli/diessel ziko wapi?
4. Naona hukuainisha ni muda gani itachukuwa kuwa even na gharama za kuanzisha biashara yote?
5. Insuarance iko wapi?
6. Ni kwa kipimo gani utajua kama dereva alipata pesa zaidi au chini ya 10,000 kwa siku?
 
Tumia taaluma yako kuwa mtaji wa kukuingizia kipato ili ikurahisishie kukua kibiashara zaidi. Fungua kituo cha kutoa mafunzo ya ziada (TUITION) then tafuta vijana wenye ujuzi na uwezo wa kufundisha masomo mbalimbali then wawe wanakulipa kila siku. Pia unaweza kuongeza na darasa la chekechea ukaajiri mwalimu mmoja afundishe huku ukiwa na malengo ya kuja kufungua shule yako kubwa.
 
Am also in moshi am gonna show you an amazing business with a very little investiment and its worthy milions of money in 3-5 years or less.am specifically at kcmc you can reach me through 0752720276.
 
Am also in moshi am gonna show you an amazing business with a very little investiment and its worthy milions of money in 3-5 years or less.am specifically at kcmc you can reach me through 0752720276.
Mkuu we semea hapa hapa jamvini. Unaweza ukakuta kuna watu wengine wana uzoefu zaidi na hiyo bussiness yako wakakupa mawazo bora kuliko yale uliyokuwa nayo.

Weka hapa watu wachangie.
 
Mkuu we semea hapa hapa jamvini. Unaweza ukakuta kuna watu wengine wana uzoefu zaidi na hiyo bussiness yako wakakupa mawazo bora kuliko yale uliyokuwa nayo.

Weka hapa watu wachangie.

Kweli na wengine tunufaike
 
Am also in moshi am gonna show you an amazing business with a very little investiment and its worthy milions of money in 3-5 years or less.am specifically at kcmc you can reach me through 0752720276.

mtoa post alitaka ashauriwe miaka miwili nyuma 2011, now 2013
inawezekana hizo pesa hanazo tena, au yupo mishe nyingine kabisa hana tena mawazo ya biashara.

kwahiyo weka hayo mawazo yako hapa, wana-jf wote tufafaidike na hayo mawazo.
 
Am also in moshi am gonna show you an amazing business with a very little investiment and its worthy milions of money in 3-5 years or less.am specifically at kcmc you can reach me through 0752720276.

Isije kuwa ni Sijui GNLD, sijui Forever Living. Kama ni hiyo usijaribu kimbia mbio nyingi achana nayo. Other wise utakuwa Marching Army
 
mtoa post alitaka ashauriwe miaka miwili nyuma 2011, now 2013
inawezekana hizo pesa hanazo tena, au yupo mishe nyingine kabisa hana tena mawazo ya biashara.

kwahiyo weka hayo mawazo yako hapa, wana-jf wote tufafaidike na hayo mawazo.

ndg yng mawazo ya humu sio kwa ajiri ya mtu moja na kwa mtazamo wangu huu ushauri huwa unaishi siku zote ndo maana unaweza kuta uzi wa kitambo lakini ukawa msaada mkubwa sana
 
Nielimishe kidogo,
1. unataka kuniambia kuwa boda boda inaingiza si chini ya 10,000 kwa siku?
2. Mbona katika hesabu zako hukuweka malipo ya dereva wako?
3. Gharama za petroli/diessel ziko wapi?
4. Naona hukuainisha ni muda gani itachukuwa kuwa even na gharama za kuanzisha biashara yote?
5. Insuarance iko wapi?
6. Ni kwa kipimo gani utajua kama dereva alipata pesa zaidi au chini ya 10,000 kwa siku?

Nitamsaidia kujibu baadhi ya maswali
1.Mnaingia mkataba na dereva wako kuwa akuletee 10000 kwa siku..Baada ya mwaka pikipiki ni yake,ila hii inategemea uko wapi.Wengine huleta sh elfu 7 au 5 kwa siku,inategemea uko wapi na mmekubaliana vipi.
2.Dereva wa bodaboda hana mshahara ndugu yangu.
3.Gharama za petrol ni siku ya kwanza unapomkabidhi tu unaweza ukampa hata mafuta ya elfu 10 tu.
4.Swali la nne sijalielewa.
5.Insurance ni sh 50,000.
6.Mkishaweka makubaliano ya kuletewa sh elfu 10 kwa siku hata apige kazi apate sh 20 utaletewa kiwango chako kilekile mlichokubaliana.
Kutokana na uelewa na uzoefu wangu hayo ndo nnayoyafaham kuhusu biashara hii ya bodaboda
 
Back
Top Bottom