Nisaidieni nifanye biashara gani? Nina mtaji wa 3,000,000/=, nipo Himo-Moshi

damashizo

Member
Jan 20, 2011
61
15
Waheshimiwa wana JF.

Wengi wanasema wanashidwa kuanzisha biashara kwasababu hawana mitaji lakini mimi ni kinyume chake nina mtaji wa tsh 3,00,000/=, mimi ni mwalimu naomba msaada wa mawazo ya biashara ambayo naweza kuifanya himo-moshi.

Biashara iwe ile ambayo angalau kwa siku lazima nipate wateja.

Asante wadau.

WAHESHIMIWA WANA JF. WENGI WANASEMA WANASHIDWA KUANZISHA BIASHARA KWASABABU HAWANA MITAJI LAKINI MIMI NI KINYUME CHAKE NINA MTAJI WA Tsh 3,00,000/=, MIMI NI MWALIMU NAOMBA MSAADA WA MAWAZO YA BIASHARA AMBAYO NAWEZA KUIFANYA HIMO-MOSHI. BIASHARA IWE ILE AMBAYO ANGALAU KWA SIKU LAZIMA NIPATE WATEJA. ASANTE WADAU.

Uza unga haukosi wateja.

jiunge kwenye zile kampuni za kuuza sabuni, dawa za magonjwa mbalimbali....kampuni hizo ni kama aloevera, gnld na zingine kibao

Sina hakika una laki tatu au milioni tatu ndugu yangu..ila kwa himo biashara baina ya Kenya na Tanzania nasikia huwa zinalipa..Bahati mbaya siwezi kushauri usafirishe mazao nje ingawa inalipa sana maana kuna wabinafsi wamekataza hilo.

Fanya biashara ya mazao ndugu kenya yanalipa sana, pale chura hamna shida siunaelewa tena

nakushauri kama upo unaweza pata sehemu ya biashara nzuri uza vipodozi maana vinalipa sana

nenda same ulime tangawizi acha na na ujinga wa kuuza maji ,pipi,unga its a risk hata wapuuz can take ,hii ndani ya mwaka umetusua

GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO

GHARAMA YA HEKTA MOJA:
Mbegu Tshs. 240,000/-
Vibarua 250,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 150,000/-
Jumla 640,000/-
MAPATO:
Kilo 20,000 X300 =6,000,000/-

nenda same ulime tangawizi acha na na ujinga wa kuuza maji ,pipi,unga its a risk hata wapuuz can take ,hii ndani ya mwaka umetusua

GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO

GHARAMA YA HEKTA MOJA:
Mbegu Tshs. 240,000/-
Vibarua 250,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 150,000/-
Jumla 640,000/-
MAPATO:
Kilo 20,000 X300 =6,000,000/-

Mkuu usisahau ku factor in issue zingine kwa mfano...upatikanaji wa mvua, u need to value na hilo shamba (kwa case yako umeassume jamaa tayari ana shamba lililo idle), gharama za usimamizi mpaka utakapovuna, usafiri na storage n.k n.k.

So kwa ushauri wangu, unahitaji kufanya upembuzi wa kutosha kabla hujaamua biashara gani ufanye. kwa maana hiyo Business Plan (Andiko la Mradi) kwa biashara yoyote ile ni muhimu sana.

Kuanzisha biashara si sawa na radio unayonunua dukani na ku plug and play.

Kama utahitaji kutayarishiwa Business Plan kwa gharama nafuu usisite kuwasiliana na mimi (just PM me).

Mwalimu nakushauri ufuge kuku wa mayai, kwa kuwa utakuwa na muda wa kutosha kuwacheki asubuhi mchana na jioni.
kama ujawahi fuga kabisa nenda kwa bwn mifugo anza na kuku 200 au chini ya hapo, utahitaji.
banda, 200@3,000 600,000
vifaranga 200@2500 = 500,000
vifaa vinginenyo 120,000
jumla 1,220,000
baada ya miezi 4-5 wataanza kutaga mayai 180 kwa siku.
Mauzo ya mayai tray 180 kwa mwezi @5000 900,000
Chakula cha kuku bags13 ya kg50@33,000 525,000
Madawa na mengineyo 50,000
Faida kwa mwezi 325,000.
then faida mpaka wamalize kutaga mayai 2,600,000 miezi 8 had 12 ivi.
jaribu apo ticha, my queen does that. for any question you are welcome

Mawazo ya wanajamii ni mazuri. JARIBU BODA BODA!!!!

Nunua piki piki 2 tbeter au yoyote ya kichina Bei moja ni milioni moja na laki nne 1.4
nakushauri ununue mbili so ni milioni 2 na laki 8

tafuta vijana wawili waaminifu wafanye boda boda kwa siku ni elfu 10 so kwa mbili ni elfu 20

easy money japo zipo nyingi huwezi lala njaa. kwa wiki unaingiza laki 140 mara wiki 4 so

kwa mwezi laki 5 na 60:

here is how:

kwa siku 10,000 * 2 =20,000

kwa wiki 20,000 * 7 =140,000

kwa mwezi 140,000 * 4= 560,000

kumbuka service ni elfu 50. ikipata ajari kuirekebisha vifaa na spea haizidi elfu 50

pia usisikilize maneno ya watu kwamba zipo nyingi sababu ili ufanikiwe ni lazima uwe RISK TAKER. pia wakisema zipo nyingi jua kuwa kwenye vingi ndio pana mengi more faida i mean.

Mwalimu nakushauri ufuge kuku wa mayai, kwa kuwa utakuwa na muda wa kutosha kuwacheki asubuhi mchana na jioni.

kama ujawahi fuga kabisa nenda kwa bwn mifugo anza na kuku 200 au chini ya hapo, utahitaji.

banda, 200@3,000 600,000

vifaranga 200@2500 = 500,000

vifaa vinginenyo 120,000

jumla 1,220,000

baada ya miezi 4-5 wataanza kutaga mayai 180 kwa siku.

Mauzo ya mayai tray 180 kwa mwezi @5000 900,000

Chakula cha kuku bags13 ya kg50@33,000 525,000

Madawa na mengineyo 50,000

Faida kwa mwezi 325,000.

then faida mpaka wamalize kutaga mayai 2,600,000 miezi 8 had 12 ivi.

jaribu apo ticha, my queen does that. for any question you are welcome

kuna Gomboro usisahau inaua kuku bila huruma.

Back
Top Bottom