Nisaidieni, naweza kufa kwa mawazo

Mimi ni mwanaume,
Nimefikiria sana mambo mengi, nimepitia uzoefu mgumu sana maishani, kijamii na kimahusiano.
Kimaisha (uchumi) sijafeli sana, niko vizuri. Ila kwa changamoto nilizopitia, nimekuwa na mtazamo tofauti kuhusu maisha.
Nimejikuta nachukia wanawake kuliko maelezo, nikimwona mwanamke naona kama jambazi anapita pembeni yangu.
Nimejawa na roho ya ukatili na kisasi. Kitu kinachoitwa mapenzi kwangu ni kama hadithi (myth).

Nilipogundua hali yangu nikaamua kuwa busy na shughuli za kiuchumi, lakini naona hakuna nafuu. Siwezi kueleza yote hapa nishaurini nifanyeje nirudishe ubinadamu wangu na furaha yangu. Naumia sana

Updates!!!!
Nashukuru kwa ushauri, kejeli na mitazamo yenu.
Kwa ujumla Mambo yaliyoniumiza sana katika maisha yangu ni;
  1. Ndoa haiko vizuri. Matarajio yangu kwa niliyempenda na nilivyokuwa namfahamu, yamegeuka kuwa jehanamu ndogo. Sina furaha wala hamu tena, ninapotazama nyuma na nilipo, majuto yananiumiza. Sometimes nawaza kuwa nilifanya makosa fulani katika kufanya maamuzi, sasa ndo yananigharimu.
  2. Pale nilipoamua kujiliwaza kwa kutafuta relief kwingine kila mara huishia kwa maumivu zaidi kuliko faraja. Maumivu ya kutendwa ni afadhali ya jana.
  3. Sioni faida ya elimu yangu niliyoisotea muda mrefu, wala mali ninazomiliki.
  4. Nimegundua ni vigumu sana kumweleza rafiki wa karibu sana ambaye unadhani ni msaada, kumbe ni wanafiki. Sasa kubaki na majipu moyoni naona nakaribisha kifo bila kujielewa.

Una umri gani? Naweza kupa ushauri nasaha km uko radhi na si zaidi ya hayo. Pole na kuwa makini maisha ni yako. Gimme a PM if u r serious
 
Fanya meditation,tafuta hobby au mchezo wa kukuliwaza,toa sana misaada kwa wasiojiweza,jipende na jitunze pia ikuwezekana onana na mtaalamu wa saikolojia na ushauri nasaha
 
Pole sana ila nakushauri usiogope kuliwa mwanaume kuliwa ni kawaida. Nachokiona hujapata chaguo lako. Tust me kuna sehemu utapata na utapunzisha mawazo yako yote. Tafta fatuta bana mbona wenzio wamepata? Ila hususahau kufanya kazi kwa nguvu.

Ndoa ivumilie hata baba yako alivumilia. Tumia akiri usitafte wrong choice.mfano, shida yako kwa sasa epuka kutafuta mwanamke alieko chuo chochote kamwe husijalibu.how old a u?ili niendelee, nisiwe naongea na under 30 boyz wanaotongoza hadi wa primary.
 
Wala hizo ndo za kukujenga. Mikasa nilioisikia mikubwa zaidi. Lakin wanaume waliotendwa wapo strong bro
 
Mimi ni mwanaume,
Nimefikiria sana mambo mengi, nimepitia uzoefu mgumu sana maishani, kijamii na kimahusiano.
Kimaisha (uchumi) sijafeli sana, niko vizuri. Ila kwa changamoto nilizopitia, nimekuwa na mtazamo tofauti kuhusu maisha.
Nimejikuta nachukia wanawake kuliko maelezo, nikimwona mwanamke naona kama jambazi anapita pembeni yangu.
Nimejawa na roho ya ukatili na kisasi. Kitu kinachoitwa mapenzi kwangu ni kama hadithi (myth).

Nilipogundua hali yangu nikaamua kuwa busy na shughuli za kiuchumi, lakini naona hakuna nafuu. Siwezi kueleza yote hapa nishaurini nifanyeje nirudishe ubinadamu wangu na furaha yangu. Naumia sana

Updates!!!!
Nashukuru kwa ushauri, kejeli na mitazamo yenu.
Kwa ujumla Mambo yaliyoniumiza sana katika maisha yangu ni;
  1. Ndoa haiko vizuri. Matarajio yangu kwa niliyempenda na nilivyokuwa namfahamu, yamegeuka kuwa jehanamu ndogo. Sina furaha wala hamu tena, ninapotazama nyuma na nilipo, majuto yananiumiza. Sometimes nawaza kuwa nilifanya makosa fulani katika kufanya maamuzi, sasa ndo yananigharimu.
  2. Pale nilipoamua kujiliwaza kwa kutafuta relief kwingine kila mara huishia kwa maumivu zaidi kuliko faraja. Maumivu ya kutendwa ni afadhali ya jana.
  3. Sioni faida ya elimu yangu niliyoisotea muda mrefu, wala mali ninazomiliki.
  4. Nimegundua ni vigumu sana kumweleza rafiki wa karibu sana ambaye unadhani ni msaada, kumbe ni wanafiki. Sasa kubaki na majipu moyoni naona nakaribisha kifo bila kujielewa.

Umetendewa nn?eleza kilichokuumiza ili tukushauli,lazima Tujuwe sos kaka.
 
Usijali hauko peke yako wanaopitiahali hiyo.

Fuata approach hii itakusaidia.

Kinachokusumbua ni majeraha ya nafsi na roho yaliyotokea maishani mwako.

Ufumbuzi lazima uzingatie upanywaji wa nafsi na roho yako.
Kwanza mkaribishe Mungu kwa njia ya Yesu kristo awe Bwana na mwokozi wako yaani uokoke.

Pili tumia muda wako vizuri kuulisha moyo wako kwa neno la Mungu yaani biblia,sikiliza nyimbo za injiri, fuatilia mafundisho ya neno la Mungu kwa njia mbalimbali ili kuihuisha nafsi na roho yako.
Anza mazoezi ya kiroho kama kufanya maombi, anza zoezi hilo na marafiki waliokubali kukusaidia hasa waliookoka ili usivutwe na dunia tena.

Hatua hizo zitavuta nguvu za uungu kukusaidia na kukupa maono mapya juu ya maisha yako.

Zingatia hayo, nakupa mwezi mmoja tu utakuja kutoa ushuhuda hapa ndani.

Jina la Yesu lisifiwe. Aliweza kwetu hatashindwa kwako.
 
Pole sana na matatizo. Njia moja ambayo imenisaidia mimi ambayo inaweza kukusaidia pia ni kumpa Yesu maisha yako yeye ndiye nji na kweli na uzima, Mat11:28, Yesu anasema " Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na mizigo nami nitawapumzisha".
 
Kwa nilivokuelewa una tabia ya kutokuamini mtu yeyote na pia una matarajio makubwaa sana kutoka kwa mke/ girlfriend km vile umepata malaika. Utakapokubali kuwa watu tumeumbwa tofaut na kuona kuwa kila mmoja ana uwezo wa kufanya jambo fulan na sio ww kujiona unaweza kila kitu na wengine wote ni wajinga hapo ndo unapokosea. Punguza userious wako shirikiana na wengine sio lzma uchukue kila walisemalo lkn kwa kuchanganya mawazo ya watu mbalimbali utaibuka na wazo zuri. Ulijiona unajua na kuweza kila kitu huyo mkeo akajisikia kutengwa hivo na yy akaendelea kuishi kivyake ulivoona hivo wewe ukaanza kuumia. BADILIKA MKUU. Jitahidi kubadilika wewe mwwnyewe kwa kuukubali ukweli huu nliokwambia.
 
Nawapenda wanajamii walinishauri vizuri pindi nilipopitia magumu kama yako. Namshukuru Mungu nipo vizuri nafanya yangu kiroho safi nasubiri mume wangu atakayenipangia. Kuna wanadamu hawana huruma hasa hisia za wenzao. Hongeza bidii katika maombi pombe huwa sio solution wala michepuko.
 
Muombe tu mwenyezi Mungu akuondolee roho ya chuki pia sali sana utapata faraja ya moyo wako ktk kila japo ili ulifikie lazima kukutana na changamoto zenye kukatishaaa tamaa.....
 
Hizo chuki na hasira uko sawa. Kunachukizo Kuu kutoka kwa hawa viumbe. Hata Adam alichukizwa sana kwa vituko vya Eva.
Wanavituko sana, Wajue tu kwamba Wanavituko mpaka kaburini.
Sasa utafanya nini kama wapo kwa ajili ya hayo?
Enjoy them and be happy.
 
Kweli ni tatizo sana hasa ukiingia kwenye mahusiano yasiyo faa, wote tunapitia nikushauri kama una watoto wajali sana na kuelekeza mapenzi yako kwao. Lkn mtendee mwenzi wako kama inavyopashwa yaani utimize wajibu wako kama hana habari na wewe usimwache akaenda zake. Wanawake wako hivyo ns unapombembeleza usimtakie ahadi.
 
Back
Top Bottom