Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 15,138
- 16,203
Nina mtoto wa kiume umri ni miaka mitatu na nusu, katika siku tatu mfululizo inapofika saa 6 usiku anashtuka sana anasema ameona majongoo kitandani yanatembea wakati mwingine anasema ameyaona ukutani na kama taa imezimwa ndio kabisa anashtuka sana na kulia, nilijaribu jana kumwamisha kutoka kwa mama yake mdogo nikawa na ninalala pamoja na mama yake lakini hivi ninavyoandika sasa inaingia siku ya tatu mfululizo akiwa analalamika hasa inapofika saa usiku. Kwa mchana hii hali haipo hata akilala mwenyewe na Inafika wakati anaangalia kwenye shuka kama mtu anayetafuta punje ya mchanga/mbegu chini na ni hofu inayompelekea hadi anaomba kukumbatiwa.